kama ni wewe ungemuoa? ungemwacha dada wa wa2!

kama ni wewe ungemuoa? ungemwacha dada wa wa2!

Ney maa

Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
95
Reaction score
34
Hii ni realy imetokea kwa familia rafiki na mpaka sasa nafuatilia sijui kaka atafanya nini, dada ni nesi wa hospitali fulani na kaka ni tabibu wa hospitali hiyo walikutana wakapendana bt dada kampita kaka kwa miaka 2 (miaka 30 kwa 32) na hilo halikua tatizo kwao kwa jinsi walivyopendana.

Ikatokea dada akapata ujauzito wa kaka na kwa kua kaka alikua ameishika sana imani ya dini yake hakupenda waendelee kulea mimba kiholela waliamua kwenda kanisani kutangaza ndoa na juma 2 ilopita ilitangazwa kwa mara ya 3 kwa wale wakristo wanaelewa kutangazwa kwa ndoa.

Ndoa inatakiwa kufungwa jmosi ya wiki hii.......lililotokea Mungu saidia!.......dada jumanne ilopita aliugua akalazwa hospitali mume wake mtarajiwa aliomba marafiki waombe kwa ajili ya mkewe apone ili waweze kufanikisha send off iliyokua ifanyike alhamisi hii na ndoa ya jumamosi ambapo tayari walikodi ukumbi na kutoa kadi za mwaliko.

mkewe ilipofika jumatano vipimo vikaonyesha mtoto wa miezi 4 2mboni amefariki akafanyiwa upasuaji akatolewa hali ya dada iliendelea kua mbaya send off imeairishwa leo asubuhi matatizo makubwa yameonekana baada ya vipimo vya doctor kwamba kizazi lazima kitolewe ili kuokoa maisha ya dada.

madactari wamefanya upauaji kwa mara nyingine wameondoa kizazi..............dada mpaka sasa analia sana anamwomba kaka kesho kutwa jmoso i mean wafunge ndoa pale hospitalini kaka amechanganyikiwa hajui afanyeje coz kwa sasa mkewe hana kizazi na bado amelazwa na ndoa inatakiwa kufungwa jmosi ya wiki hii ushauri wenu tafadhalini!
:help::help::help:
 
Anatakiwa amuoe maana hata yeye anaweza akatolewa kizazi chake mara baada ya kuoa.Tatizo kama hilo linamkumba yoyote bila kujali jinsia.Kuna jamaa mmoja alimkimbia mke kisa kajifungua kwa oparation, akaamua kuoa mke mwingine nae akajifungua kwa operation tena yeye akatolewa mpaka na kizazi hivyo ujanja wake ukaishia hapo.Kuna jamaa mwingine alikuwa anajisifu hawezi kuoa mwanamke aliyekuwa na mahusiano na wanaume wengi kwani aliwaita ma screpa yaani second hand.Kitu cha kushangaza kila mchumba aliyekuwa akimpata alikuwa ni second hand hadi mwisho wa siku akamuoa wa namna hiyo.Muache Mungu aitwe Mungu unaweza ukajiona wewe ni mrembo au handsome lakini baadaye ukabadilika, unaweza ukajiona tajiri baadae ukawa masikini.
 
amuoe bwana.Future is uncertainity.No one knows tomorrow only God knows mipango iendelee kama inawezekana hospital wafunge ndoa hapo hapo
 
Mmmh! Kuna mazingira unagundua kabisaa kama hapa hata nikiolewa, lazima nisalitiwe!!!!
...
Hakuna imani hiyo sku hizi! Eti mtu akose mtoto kwa kukabwa na dini! Sahau! Akili kichwani mwenu!!
 
Mungu aepushie mbali!!!
...
Ivi amu hapo kama huyo muoaji ni mwanao wa pekee ungemshauri vipi?

amuoe bwana.Future is uncertainity.No one knows tomorrow only God knows mipango iendelee kama inawezekana hospital wafunge ndoa hapo hapo
 
Hzi story shigongo anazitafuta sana.
 
Wewe kaka unatakiwa umuoe huyo binti,
kuzaa majaliwa bana, mbona wapo wengi hawajatolewa kizazi na hawazai
 
ndoa ifubgwe ila sio hospitalini augue apone na baadaye watengeneze sherehe haki ya mama! ndo upendo
 
Ndio maana ktk mafundisho kabla ya ndoa huwa tunasisitzwa sana kwamba nyie wawili ndio mmependana na kupata watoto ni majaliwa,ingewezekana asitolewe na pia asipate mtoto tena!Sasa la msingi hapo ni yeye kumuomba mungu na kufuata moyo wake unavyomtuma kwani mwisho wa siku ni yeye ndio atakeyeishi nae sio mama,baba,dada wala kaka.Na huyo dada yeye pia naamini hakupenda hayo taliyotokea,hayo ni majaribu tu ambayo tunapaswa kukabiliana nayo na kuyashinda
 
amuoe tu jaman,kumbuka ni mimba yake ndo imesababsha had kizazi chake kitolewe.
 
Mungu aepushie mbali!!!
...
Ivi amu hapo kama huyo muoaji ni mwanao wa pekee ungemshauri vipi?

as a woman and a mother kwa kweli ningemsimamia amuoe.Ha ha najua unamaanisha mjukuu jamani wangekaa mpaka matatizo yaishe afu wenyewe wangeamua kukubaliana.
 
amuoe lakini dada akijua tu mzee kuchapa nje itakuwa part of her life.
 
as a woman and a mother kwa kweli ningemsimamia amuoe.Ha ha najua unamaanisha mjukuu jamani wangekaa mpaka matatizo yaishe afu wenyewe wangeamua kukubaliana.

...
Nadhani umefikiria vizuri sana! Thus why umecheka kidogo!
Kati kati ya ukweli uongo hujitenga.....!
Hiyo ngumu kumesa dada! Mtu anamuacha mke wake kisa haponeshi tu! Uyo hazai kabisaaaa! Na sahau kuhusu miujiza! Mmmh! Ningekua mimi ningemueleza tu hivi: nakuowa but sitosita kutafuta mtoto! Plz sitaki tokorofishane hapo mbele!!! Eee! Nampa za uso kama zilivyo! so, chaguo ni lake!
 
...
Nadhani umefikiria vizuri sana! Thus why umecheka kidogo!
Kati kati ya ukweli uongo hujitenga.....!
Hiyo ngumu kumesa dada! Mtu anamuacha mke wake kisa haponeshi tu! Uyo hazai kabisaaaa! Na sahau kuhusu miujiza! Mmmh! Ningekua mimi ningemueleza tu hivi: nakuowa but sitosita kutafuta mtoto! Plz sitaki tokorofishane hapo mbele!!! Eee! Nampa za uso kama zilivyo! so, chaguo ni lake!

ukimwambia kabla ya ndo di vizuri jamani embu fikiria hali aliyo naye kama ndo wewe ningekushauri usubiri kwanza mpaka akitulia najua ni ngumu itachukua mda afu mtapanga mpaka kufikia hatua ya kuoana ina maana mdada mwelewa ana ufahamu mpana halitokuwa tatizo.
 
Back
Top Bottom