Kama ni kweli, Yanga mnakera

Ng'egera

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
766
419
Wanajf habari
nikiwa kama mshabiki wa timu ya yanga nimefeheka sana baada ya kumsikia mwenyekiti wa mtani wetu simba akitoa tahadhari namna tutakapomchezesha kessy mimi napata tabu sana inamaana viongozi wanaoshughulikia usajili hawajui sheria na taratibu au walilifanya jambo hili kwa ajili ya kampeni kwenye uchaguzi yaani inakera sana
 
Attachments

  • Yanga.jpg
    Yanga.jpg
    12.6 KB · Views: 75
Mbona ume conclude sasa?

We ulitegemea kiongozi wa Simba angesemaje kwenye sakata la mchezaji wa simba kwenda Yanga?

Hujajua siasa za mpira wa Yanga na Simba tu hadi leo?
 
Wanajf habari
nikiwa kama mshabiki wa timu ya yanga nimefeheka sana baada ya kumsikia mwenyekiti wa mtani wetu simba akitoa tahadhari namna tutakapomchezesha kessy mimi napata tabu sana inamaana viongozi wanaoshughulikia usajili hawajui sheria na taratibu au walilifanya jambo hili kwa ajili ya kampeni kwenye uchaguzi yaani inakera sana
Hujaeleweka unataka nini hasa. Kessy atacheza na huyo kiongozi wa mtaa wenu hatofanya kitu. Pole sana
 
Simba wanaweza kuwa na uungwana wa kuwasihi Yanga kwenda kumalizana nao ili waweze kulisawazisha swala hilo kablaYanga hawajaanza mashindano. Haishangazi sana.Wanaweza kuwa walipitikiwa kwamba swala hilo halikuhitaji mjadala. Ilikuwa ni kiasi cha wao Simba tu kuipeleka TFF barua ya kumwachia Kessy, hasa ukizingatia kauli sahihi ya Hans Poppe kwamba Simba haikuwa ikihitaji pesa hata senti kutoka Yanga, ni uungwana tu. Isingewagharimu Simba chochote, ingebaki Yanga kuamua kukubali uungwana huo au kukataa fadhila hiyo ya mtani wake. Pia haishangazi sana. Kinachoshangaza ni ustahamilivu wa Simba (Manara na Hans Poppe) kutotangaza jamala (offer) hiyo kwa umma, hasa baada ya kujibiwa mbovu na Yanga (Muro) kama Hans Poppe alivyotoboa. Kadhalika ukomavu wa Yanga (Muro) kujibu shombo hilo kwa siri kubwa kiasi cha chombo chochote cha habari kutoambulia hata fununu. Lakini mshangao zaidi ni vipi ustahamilivu huo wa Simba na ukomavu huo wa Yanga vitoweke ghafla baada tu ya kubainika na umma kwamba Kessy hakucheza kwa kukosa barua ya Simba. Inshalla watambuzi mtatambua hoja yangu!
 
Wanajf habari
nikiwa kama mshabiki wa timu ya yanga nimefeheka sana baada ya kumsikia mwenyekiti wa mtani wetu simba akitoa tahadhari namna tutakapomchezesha kessy mimi napata tabu sana inamaana viongozi wanaoshughulikia usajili hawajui sheria na taratibu au walilifanya jambo hili kwa ajili ya kampeni kwenye uchaguzi yaani inakera sana

Samahani sana kama nitakuudhi, kwa namna ulivyoandika hapa inaelekea kuwa wewe ni Simba na wala siyo Yanga...umeliweka andiko hili kinamna kama kebehi...
 
Mimi yanga damu tatizo hata nikiweka ushahidi wa picha niliyopiga na keneth mkapa hamtaamini ila swala hili limenikera kwanini kessy asicheze kisa barua inamaana viongozi hawakujua au ujinga tu
 
Kwa leo nimechoka, ila kesho nitakufahamisha vizuri zaidi, tukiwasiliana kwa njia hii...
 
LABDA UWEKE ULIYOPIGA NA JERRY MURO
Mimi yanga damu tatizo hata nikiweka ushahidi wa picha niliyopiga na keneth mkapa hamtaamini ila swala hili limenikera kwanini kessy asicheze kisa barua inamaana viongozi hawakujua au ujinga tu
 
hapa kiukweli yanga walitakiwa wawandikie simba barua kuomba waridhie kessy achezee yanga lakini ninachokiona kwa sababu ya jeuri na kutokujua sheria za CAF wakataka walete zao za kibongo bongo. na kama kweli walifuata taratibu ninavyomjua jerry muro tungeshaona barua ya yanga kwenda simba kwenye magazeti na mitandaoni.
 
Simba wanaweza kuwa na uungwana wa kuwasihi Yanga kwenda kumalizana nao ili waweze kulisawazisha swala hilo kablaYanga hawajaanza mashindano. Haishangazi sana.Wanaweza kuwa walipitikiwa kwamba swala hilo halikuhitaji mjadala. Ilikuwa ni kiasi cha wao Simba tu kuipeleka TFF barua ya kumwachia Kessy, hasa ukizingatia kauli sahihi ya Hans Poppe kwamba Simba haikuwa ikihitaji pesa hata senti kutoka Yanga, ni uungwana tu. Isingewagharimu Simba chochote, ingebaki Yanga kuamua kukubali uungwana huo au kukataa fadhila hiyo ya mtani wake. Pia haishangazi sana. Kinachoshangaza ni ustahamilivu wa Simba (Manara na Hans Poppe) kutotangaza jamala (offer) hiyo kwa umma, hasa baada ya kujibiwa mbovu na Yanga (Muro) kama Hans Poppe alivyotoboa. Kadhalika ukomavu wa Yanga (Muro) kujibu shombo hilo kwa siri kubwa kiasi cha chombo chochote cha habari kutoambulia hata fununu. Lakini mshangao zaidi ni vipi ustahamilivu huo wa Simba na ukomavu huo wa Yanga vitoweke ghafla baada tu ya kubainika na umma kwamba Kessy hakucheza kwa kukosa barua ya Simba. Inshalla watambuzi mtatambua hoja yangu!

Tatizo hili ni dogo ila ila kitu kinaitwa 'mdomo' ndio kinafanya mambo rahisi yanakuwa magumu. Huyu kijana Kessy mwenyewe angeweza kwenda Simba kuomba barua ya kumalizana kabisa, kila mtu achukue utaratibu wake. Lkn maskini kwa kuwa mambo yanakwenda kishabikishabiki na kinazinazi tu ndio mambo ysnakuwa hivi
 
Nakubaliana sana na wewe kwa hili. Lakini ukizama hasa ndani ya kadhia hii, CAF yenyewe inapaswa kuwa ndio mlaumiwa namba moja. Imekuwaje itoe leseni kwanza ndioo ihoji mengine baadaye? Kama leseni isingetoka bila ya barua ya Simba, Yanga wangeamua mapema kuiomba barua hiyo au kumsamehe Kessy mpaka baada ya kumaliza mkataba wake Simba. Nionavyo, Yanga kutowachezesha wanne hawa kwa indhari hii ya CAF ni kuepuka usumbufu unaoweza kutokea. Lakini naamini mamlaka yoyote ya rufaa ingewapa haki baada ya kuithibitishia kwamba iliwachezesha ikiwa na leseni zao tayari.
 
Back
Top Bottom