Kama ni kweli wapinzani wananunuliwa basi tuna Rais fisadi

Alonso14

JF-Expert Member
Aug 6, 2017
1,785
1,817
Amani iwe nanyi wakuu

Napenda niende moja kwa moja kwenye mada siku za karibuni hapa nchini kumetokea wimbi la wanasiasa wa upinzani kujiunga chama tawala kwa kigezo cha kumuunga mkono raisi.

Lakn kwa taarifa za chini chini zinasema kuwa hao wapinzani wananunuliwa na chama tawala.

Na ukiangalia kwa jicho la tatu ni kweli haingii akilini mtu kuacha kazi kwa kigezo cha kumuunga mkono rais mbona NAPE NA BASHE wanapingana na serikali na wapo chama tawala?

Kwan huwezi kumuunga mkono rais ukiwa upinzani?

Ngoja nirudi kwenye kichwa cha habari kama ni kweli viongozi wananunuliwa chini ya udhamini wa chama cha mapinduzi je mnajifanya kukipigigania chama cha mapinduzi hamuoni kuwa ni ufisadi na misue of public fund?

Kwann hiyo pesa isijikite katika kufanya maendeleo ya msingi mfano kuongeza wafanyakazi mishahara au kuboresha miundombinu vijijini?

Conclusion: kama chama cha mipinduzi kinanunua wapinzani basi hakifai kutuongoza na viongozi wake wa juu ni wanafiki wanaojifanya kupinga rushwa huku wakiihalalisha hiyo hiyo rushwa

CCM ACHENI UNAFIKI WA KUJIFANYA WAZARENDO
 
Kwani unafikiri wamenunuliwa? lakini pia kwanini wanunulike? Binafsi naamini kuna mambo yanaendelea CHADEMA ambayo siku yakija kutoka watu wataendelea kumlaumu Magufuli badala ya kuweka vioo mbele yao na kujiangalia...
Mzee mwanakijiji shikamoo habari za siku ndugu yangu! Salama mkuu! Upo ndugu yangu .
 
Naomba kuuliza, hawa wanahama vyama na kuachia ngazi. Je, wanarusiwa kugombea tena wakiwa kwenye chama kingine?
 
Mtu akienda kujiunga na CCM mnasema kanunuliwa, ila akienda Chadema mnakaa kimya au wanaenda Chadema kwa mkopo..?
 
....Ulikuwa zamani but now wewe ni Mzee wa mipasho...
Uzee dawa! Kama hivi kawaambia ukweli mnaanza kumshambulia. Msome kwa utulivu utamuona kwenye uhalisia wa andiko lake kuwa ccm inahubiri tofauti na kutenda kinyume chake!
Ccm haiaminiki na wala kupendwa tena na wanajidnganya kwa kuwanunua baashi ya watu na kusahau kuwa wao sio chama bali wawakilishi tu. Ccm pingeni rushwa kwa vitendo na sio kuitukuza kwa staili hii!
 
Back
Top Bottom