Kama ni kweli, Freeman Aikael Mbowe usifike huko

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,136
Reaction score
96,161
Anandika Hilda Newton

HUJUMA MSIBA WA MUASISI WA CHADEMA MZEE EDWIN MTEI.

Nimepata taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kwamba Mhe. Mbowe anatumia nafasi yake ya uanafamilia kuihujumu CHADEMA kwenye msiba wa muasisi wetu wa Chama Mzee Edwin Mtei.

Sasa iko hivi, imepangwa ratiba ya msiba siku ya Mazishi ambapo CHADEMA itapewa nafasi ya kutoa salam za rambirambi saa tatu asubuhi wakati ratiba rasmi ya msiba itaanza saa tano asubuhi.

Mhe. Mbowe na watu wake wanafanya haya yote kwasababu wamepanga kumualika Nduli Idd Amin Mama ili aje kutumia msiba wa Mzee Mtei kujisafisha baada ya kuuwa Watanganyika zaidi ya elfu 10 siku ya Oktoba 29.

Yani huyu Nduli Idd Amin Mama ukiachia mbali kwamba ameuwa maelfu ya Watanganyika na kuwazika kwenye makaburi ya halaiki, yeye ndo amembambika kesi ya uhaini Mhe. Lissu ambae ni Mwenyekiti wa Chadema ambayo iliasisisiwa Mzee Mtei, akaona haitoshi akaifungia CHADEMA isifanye Siasa, CHADEMA ambayo muasisi wake ndo huyu huyu Mzee Mtei ambae Idd Amin Mama anataka awe mgeni rasmi kwenye mazishi yake, jambo ambalo naamini hata Mzee Mtei huko aliko hawezi kuunga mkono huu ujinga.

Jambo moja ambalo Mhe. Mbowe na watu wake wanapaswa kujua ni kwamba kwenye huu msiba CHADEMA sisi sio wavamizi, huu msiba unatuhusu asilimia mia moja hivyo hatuwezi kukubaliana na hujumu za aina yoyote.

Mzee Mtei alianzisha hiki Chama, hajawai kukisaliti wala kukiumiza Chama chetu bali alikipigania kwa nguvu zake zote mpaka kimefika hapa kilipofika leo, ambapo CHADEMA imekuwa Tumaini la Watanzania.

Ametangulia mbele za Haki akiwa na ushujaa wake so lazima tumzike kwa hadhi na heshima zote.

Hatuwezi kukubali mtu ambae mikono yake inaninuka damu za Watanganyika aliowauwa kikatili aje kunajisi msiba wa Muasisi wetu wa Chama.
 
1. Hv kati ya chadema wa instagram na mbowe nani mhusika wa ule msiba?

2. Hv kati ya chadema na familia ya mtei nani mhusika mkuu wa huu msiba?

3. Kati ya kuwa gavana wa kwanza wa BOT na kuwa mwanzilishi chadomo kipi chenye heshima katika hili taifa?

ACHENI KUUSUMBUA MWILI WA MAREHEMU MSIJEANZA KUIMBA MARAA OO ICC MARA OO CNN
 
Hilda Newton leo amekuwa na uchungu na msiba huo kuliko Mbowe?

Chadema hapa ni moja tu ya taasisi zilizopata msiba na hawana haki ya kuamrisha familia ya marehemu namna ya kumuomboleza. Na Mbowe ni sehemu ya familia.

Kutaka kuleta vurugu ndio kunajisi msiba wa marehemu.

Newton anatakiwa kutambua kuwa familia ni zaidi ya chama kwenye hili. Chama kinatakiwa kuongozwa na matakwa ya familia na si vingine. Chama hakina mamlaka ya kuamua nani ahudhurie au asihudhuria. Mamlaka waliyo nayo ni ushiriki wao katika mazishi na si vinginevyo.

Stupid is as stupid does.

Amandla...
 
sijawahi kuelewa hizi drama ya misibani tanzagiza huwa ni za nini, mambo ya msiba yanapaswa yawe ya kifamilia (mke na watoto), na familia ndiyo inapaswa kuamua msiba uweje, nani aje, yupi asije, hivyo kama hawataki binadamu xyz awepo hauna sababu ya kuwepo pale pia, period
...
 
Hivi hawa wakina Hilda walikuwa wapi wakati marehemu anaugua? Leo wanataka waubebe msiba lakini hawakudai hilo wakati wa ugonjwa wake. Walichangia nini katika tiba yake? Walikuwa wanamtembelea mara ngapi au hata kuongea nae kumjulia hali?

Hivi wanafikiria familia ya Mtei inafurahishwa na kauli chafu wanazotoa dhidi ya ndugu yao? Kauli ambazo zinaendelezwa na hizi shutuma zisizo na msingi. Ovyo kabisa.

Amandla...
 
Mtawehuka sana nyinyi maccm kwa sababu mnanuka damu za Watanzania
1. Hv kati ya chadema wa instagram na mbowe nani mhusika wa ule msiba?

2. Hv kati ya chadema na familia ya mtei nani mhusika mkuu wa huu msiba?

3. Kati ya kuwa gavana wa kwanza wa BOT na kuwa mwanzilishi chadomo kipi chenye heshima katika hili taifa?

ACHENI KUUSUMBUA MWILI WA MAREHEMU MSIJEANZA KUIMBA MARAA OO ICC MARA OO CNN
 
Anandika Hilda Newton

HUJUMA MSIBA WA MUASISI WA CHADEMA MZEE EDWIN MTEI.

Nimepata taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kwamba Mhe. Mbowe anatumia nafasi yake ya uanafamilia kuihujumu CHADEMA kwenye msiba wa muasisi wetu wa Chama Mzee Edwin Mtei.

Sasa iko hivi, imepangwa ratiba ya msiba siku ya Mazishi ambapo CHADEMA itapewa nafasi ya kutoa salam za rambirambi saa tatu asubuhi wakati ratiba rasmi ya msiba itaanza saa tano asubuhi.

Mhe. Mbowe na watu wake wanafanya haya yote kwasababu wamepanga kumualika Nduli Idd Amin Mama ili aje kutumia msiba wa Mzee Mtei kujisafisha baada ya kuuwa Watanganyika zaidi ya elfu 10 siku ya Oktoba 29.

Yani huyu Nduli Idd Amin Mama ukiachia mbali kwamba ameuwa maelfu ya Watanganyika na kuwazika kwenye makaburi ya halaiki, yeye ndo amembambika kesi ya uhaini Mhe. Lissu ambae ni Mwenyekiti wa Chadema ambayo iliasisisiwa Mzee Mtei, akaona haitoshi akaifungia CHADEMA isifanye Siasa, CHADEMA ambayo muasisi wake ndo huyu huyu Mzee Mtei ambae Idd Amin Mama anataka awe mgeni rasmi kwenye mazishi yake, jambo ambalo naamini hata Mzee Mtei huko aliko hawezi kuunga mkono huu ujinga.

Jambo moja ambalo Mhe. Mbowe na watu wake wanapaswa kujua ni kwamba kwenye huu msiba CHADEMA sisi sio wavamizi, huu msiba unatuhusu asilimia mia moja hivyo hatuwezi kukubaliana na hujumu za aina yoyote.

Mzee Mtei alianzisha hiki Chama, hajawai kukisaliti wala kukiumiza Chama chetu bali alikipigania kwa nguvu zake zote mpaka kimefika hapa kilipofika leo, ambapo CHADEMA imekuwa Tumaini la Watanzania.

Ametangulia mbele za Haki akiwa na ushujaa wake so lazima tumzike kwa hadhi na heshima zote.

Hatuwezi kukubali mtu ambae mikono yake inaninuka damu za Watanganyika aliowauwa kikatili aje kunajisi msiba wa Muasisi wetu wa Chama.
Kumbuka huyo Mzee ni Baba mkwe wake Mbowe, hata akiweka mbali masuala ya kisiasa bado hawezi kukaa mbali na msiba wenye kumhusu kwa asilimia mia moja.

Halafu nina uhakika CHADEMA wengi wamemfahamu kwanza Mbowe kabla hata hawajamjua Heche, Lissu, Salum Mwalimu, Mnyika, Boni Yai na wengine wengi waliokuzwa kisiasa na Mbowe.

Punguzeni uchawa vijana.
 
1. Hv kati ya chadema wa instagram na mbowe nani mhusika wa ule msiba?

2. Hv kati ya chadema na familia ya mtei nani mhusika mkuu wa huu msiba?

3. Kati ya kuwa gavana wa kwanza wa BOT na kuwa mwanzilishi chadomo kipi chenye heshima katika hili taifa?

ACHENI KUUSUMBUA MWILI WA MAREHEMU MSIJEANZA KUIMBA MARAA OO ICC MARA OO CNN
Umegonga kisiki, hivi hujaumia
 
Ele
Hivi hawa wakina Hilda walikuwa wapi wakati marehemu anaugua? Leo wanataka waubebe msiba lakini hawakudai hilo wakati wa ugonjwa wake. Walichangia nini katika tiba yake? Walikuwa wanamtembelea mara ngapi au hata kuongea nae kumjulia hali?

Hivi wanafikiria familia ya Mtei inafurahishwa na kauli chafu wanazotoa dhidi ya ndugu yao? Kauli ambazo zinaendelezwa na hizi shutuma zisizo na msingi. Ovyo kabisa.

Amandla...
Elewa, huyu ni Mwanzilishi wa chadema. It is not an issue of nani alimuuguza. Issue ni nafasi ya chadema katika msiba wake.
 
Chadema inakuwa kama yule mtoto ambae hakumjali mzazi wake wakati wa uhai wake lakini anataka apewe heshima wakati wa mazishi yake kwa sababu tu marehemu alikuwa baba yake. Atapewa nafasi yake katika mazishi lakini heshima itaenda kwa wale waliomuuguza marehemu.

Hili suala lilipaswa kushughulikiwa kimya kimya pamoja na familia. Lakini wapambe ndio wanataka kuleta mpasuko kati ya Chadema na familia maana Mbowe ni sehemu ya familia. Ukimsemea ovyo Mbowe unaikwaza familia.

Amandla...
 
Kuna watu wanadai kuwa Chadema ni lazima isimamie msiba kwa sababu marehemu alikuwa muasisi wa Chadema. Hivi ikitokea Mungu amchukue Mbowe, Chadema ya Lissu itadai pia isimamie msiba wake kwa sababu alikuwa muasisi wa chama chao?

Amandla...
 
imegeuka kinachozungumzwa na Maria ndio Chadema na sio Chadema dar es Salaam tena

Chadema wapunguze utoto

yaani wanataka wao tu ndio wawe waombolezaji na sio mwanadamu mwingine yeyote

wanataka yaani chadema ipewe exclusivity na sio wananchi wote na taasisi zote zilizofanya kazi na marehemu

yaani chadema kwao utaratibu wa chochote hauwahusu
 
Chadema inakuwa kama yule mtoto ambae hakumjali mzazi wake wakati wa uhai wake lakini anataka apewe heshima wakati wa mazishi yake kwa sababu tu marehemu alikuwa baba yake. Atapewa nafasi yake katika mazishi lakini heshima itaenda kwa wale waliomuuguza marehemu.

Hili suala lilipaswa kushughulikiwa kimya kimya pamoja na familia. Lakini wapambe ndio wanataka kuleta mpasuko kati ya Chadema na familia maana Mbowe ni sehemu ya familia. Ukimsemea ovyo Mbowe unaikwaza familia.

Amandla...
Unataka kusema chadema hawakumjali ila ccm walimjali hivyo wanastahili kuandaliwa ratiba ya kumzika. Hizo ni vurugu, kwahiyo wewe usipomjali baba yako basi msiba uwe mikononi mwa majirani. Waachwe chadema wamzike founder wao, longolongo zozote hazikubalili
 
Anandika Hilda Newton

HUJUMA MSIBA WA MUASISI WA CHADEMA MZEE EDWIN MTEI.

Nimepata taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kwamba Mhe. Mbowe anatumia nafasi yake ya uanafamilia kuihujumu CHADEMA kwenye msiba wa muasisi wetu wa Chama Mzee Edwin Mtei.

Sasa iko hivi, imepangwa ratiba ya msiba siku ya Mazishi ambapo CHADEMA itapewa nafasi ya kutoa salam za rambirambi saa tatu asubuhi wakati ratiba rasmi ya msiba itaanza saa tano asubuhi.

Mhe. Mbowe na watu wake wanafanya haya yote kwasababu wamepanga kumualika Nduli Idd Amin Mama ili aje kutumia msiba wa Mzee Mtei kujisafisha baada ya kuuwa Watanganyika zaidi ya elfu 10 siku ya Oktoba 29.

Yani huyu Nduli Idd Amin Mama ukiachia mbali kwamba ameuwa maelfu ya Watanganyika na kuwazika kwenye makaburi ya halaiki, yeye ndo amembambika kesi ya uhaini Mhe. Lissu ambae ni Mwenyekiti wa Chadema ambayo iliasisisiwa Mzee Mtei, akaona haitoshi akaifungia CHADEMA isifanye Siasa, CHADEMA ambayo muasisi wake ndo huyu huyu Mzee Mtei ambae Idd Amin Mama anataka awe mgeni rasmi kwenye mazishi yake, jambo ambalo naamini hata Mzee Mtei huko aliko hawezi kuunga mkono huu ujinga.

Jambo moja ambalo Mhe. Mbowe na watu wake wanapaswa kujua ni kwamba kwenye huu msiba CHADEMA sisi sio wavamizi, huu msiba unatuhusu asilimia mia moja hivyo hatuwezi kukubaliana na hujumu za aina yoyote.

Mzee Mtei alianzisha hiki Chama, hajawai kukisaliti wala kukiumiza Chama chetu bali alikipigania kwa nguvu zake zote mpaka kimefika hapa kilipofika leo, ambapo CHADEMA imekuwa Tumaini la Watanzania.

Ametangulia mbele za Haki akiwa na ushujaa wake so lazima tumzike kwa hadhi na heshima zote.

Hatuwezi kukubali mtu ambae mikono yake inaninuka damu za Watanganyika aliowauwa kikatili aje kunajisi msiba wa Muasisi wetu wa Chama.
Hawezi kwenda..

Likely, atamtuma yule roporopo asiye hata na chembe ya soni wala haya, Mwigulu Nchemba kumwakilisha...

Yeye binafsi, sijui kama ataonesha pua yake pale kwa kuwa kuna hatari akaambulia hatari ya kuzomewa...!

Tayari CHADEMA wameshachukua chaji ya kila hatua maana huu ni msiba wao...

Mzee Mtei licha ya kuwa ni mwasisi wa CHADEMA, lakini mpaka anafariki juzi alikuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya chama...

Utakuwa ni ujuha, CCM na serikali kutaka kuingilia protokali ya CHADEMA kumzika mwanachama wao..

Wao waende kama wageni na wahudhuriaji wengine wote wa msiba. Kama wana salamu, watapewa nafasi kutoa salamu zao..

Lakini kamwe wasijaribu kuleta ujinga wao kama wa yule OCD wa Mbeya aliyeamua kuuvaa ujinga kwa makusudi na kushusha bendera ya CHADEMA...
 
Back
Top Bottom