Kama ni kweli, Freeman Aikael Mbowe usifike huko

Kama ni kweli, Freeman Aikael Mbowe usifike huko

Unataka kusema chadema hawakumjali ila ccm walimjali hivyo wanastahili kuandaliwa ratiba ya kumzika. Hizo ni vurugu, kwahiyo wewe usipomjali baba yako basi msiba uwe mikononi mwa majirani. Waachwe chadema wamzike founder wao, longolongo zozote hazikubalili
CCM wameingiaje hapa? Walioushika msiba ni ndugu zake akiwemo Mbowe. Naam, usipomjali baba yako ujue jirani ndio watakaomzika.

Amandla...
 
Anandika Hilda Newton

HUJUMA MSIBA WA MUASISI WA CHADEMA MZEE EDWIN MTEI.

Nimepata taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kwamba Mhe. Mbowe anatumia nafasi yake ya uanafamilia kuihujumu CHADEMA kwenye msiba wa muasisi wetu wa Chama Mzee Edwin Mtei.

Sasa iko hivi, imepangwa ratiba ya msiba siku ya Mazishi ambapo CHADEMA itapewa nafasi ya kutoa salam za rambirambi saa tatu asubuhi wakati ratiba rasmi ya msiba itaanza saa tano asubuhi.

Mhe. Mbowe na watu wake wanafanya haya yote kwasababu wamepanga kumualika Nduli Idd Amin Mama ili aje kutumia msiba wa Mzee Mtei kujisafisha baada ya kuuwa Watanganyika zaidi ya elfu 10 siku ya Oktoba 29.

Yani huyu Nduli Idd Amin Mama ukiachia mbali kwamba ameuwa maelfu ya Watanganyika na kuwazika kwenye makaburi ya halaiki, yeye ndo amembambika kesi ya uhaini Mhe. Lissu ambae ni Mwenyekiti wa Chadema ambayo iliasisisiwa Mzee Mtei, akaona haitoshi akaifungia CHADEMA isifanye Siasa, CHADEMA ambayo muasisi wake ndo huyu huyu Mzee Mtei ambae Idd Amin Mama anataka awe mgeni rasmi kwenye mazishi yake, jambo ambalo naamini hata Mzee Mtei huko aliko hawezi kuunga mkono huu ujinga.

Jambo moja ambalo Mhe. Mbowe na watu wake wanapaswa kujua ni kwamba kwenye huu msiba CHADEMA sisi sio wavamizi, huu msiba unatuhusu asilimia mia moja hivyo hatuwezi kukubaliana na hujumu za aina yoyote.

Mzee Mtei alianzisha hiki Chama, hajawai kukisaliti wala kukiumiza Chama chetu bali alikipigania kwa nguvu zake zote mpaka kimefika hapa kilipofika leo, ambapo CHADEMA imekuwa Tumaini la Watanzania.

Ametangulia mbele za Haki akiwa na ushujaa wake so lazima tumzike kwa hadhi na heshima zote.

Hatuwezi kukubali mtu ambae mikono yake inaninuka damu za Watanganyika aliowauwa kikatili aje kunajisi msiba wa Muasisi wetu wa Chama.
Chadema wanakosea sana kuendeleza ugomvi na mbowe kupitia hawa vijana.
 
Back
Top Bottom