Kama ni kweli,basi CCM hatuiwezi kamwe

Kama ni kweli,basi CCM hatuiwezi kamwe

Habari wanajamvi,leo nikiwa nimetoka k,koo naelekea zangu makumbusho ofisini kwangu,nilikuwa kwenye daladala.mara kukazuka story kuhusiana na meya wa jiji la DSM,kuna jamaaa kaongea jambo ambalo imenibidi niamini kwa kiasi fulani hasa kutokana na figisufigisu zilizotokea.jamaa anadai ya kwamba ccm wana mpango wa kuwanunua madiwani 11kutoka ukaww ili wampigie kura mgombea wa ccm.jamaa akaenda mbali zaidi na kusema hadi sasa wamefanikiwa kurubuni na kuwapa pesa madiwani 6 bado wa5 ili kazi iishe na ndipo waitishe uchaguzi,inasemekana wanachelewesha kwa sababu wanataka wahakikishe wamewapata hao wajumbe 11 na ndipo waitishe uchaguzi,,sasa kama ni kweli hizo habari basi ccm hawawezekani na ni bora mtu ufanye shughuri zako za kimaisha kuliko kufuatilia siasa za africa maba zote zipo sawa,laaana hii sijui tuliachiwa na nani ya kutofuata democracy

JUU YA KUROGWA, MTU WA KWANZA KULILIA AFRICA NI MWANA MUZIKI WA CONGO BRAZAVILLE, FRANKLIN BOKAKA.
Le Bucheron
 
Ccm wanamtegemea Manji katika mipango yao ya kushinda umeya,but ushindi kwa UKAWA ni dhahiri maana UkAWA kushindwa watakuwa wamejihujumu wenyewe maana wananchi wa Dar es salaam tumeshamaliza kazi yetu.
 
jamaa anadai ya kwamba ccm wana mpango wa kuwanunua madiwani 11kutoka ukaww ili wampigie kura mgombea wa ccm.jamaa akaenda mbali zaidi na kusema hadi sasa wamefanikiwa kurubuni na kuwapa pesa madiwani 6 bado wa5 ili kazi iishe na ndipo waitishe uchaguzi,inasemekana wanachelewesha kwa sababu wanataka wahakikishe wamewapata hao wajumbe 11 na ndipo waitishe uchaguzi,

Hofu zako tu, CCM hatuna mpango huo hatutakuwa na mpango huo na ushindi wa meya ni lazima kwa kuwa kila mmoja anaona au kusikia matunda ya CCM kupitia viongozi wetu
 
hamuiwezi ccm kwa sababu hamna watu wanaojua siasa, mageuzi ni safari ndefu siyo swala la kuamka na kuchukua nchi.wakati wananchi wameanza kupata mwamko wa mageuzi kwa kauli mbiu ya vita vya ufisadi ghafla mkawasaliti wananchi na kumchukua fisadi nkuwa mgombea wenu wa urais,kitendo hicho si tu kiliwachanganya wananchi bali kilirudisha nyuma mageuzi ya ukweli na kuwapa nafasi ccm ya kujisahihisha kwani wametambua wananchi wanataka mabadiliko na hawataki ufisadi sasa hivi kila mtu anaongelea kutumbua majipu na sio tena ufisadi kwani kiongozi wa mafisadi tayari amehamia kule walikoanza kumwita fisadi
 
Badala ya kupeleka pesa mashuleni watoto hawna chakula unaenda kununua kura. Ujinga huu unazidi viwango vyote vya ujinga. Na kwa kweli chama cha aina hii ni decadent and moribund. Its days for existence are numbered.
 
woga wa nini wakati ukawa mnazile kalamu zenye kamera...
 
Sio umeya tu,hata Zanzibar mpaka sasa CCM ndio washindi.
Tutakapoweza kuing'oa CCM madarakani,na ni baada ya kupata katiba mpya pendekezwa ndipo tutakapoweza kufanya ya maana,tofauti na hapo ni ngumu kuzuia figisu figisu za CCM.
Mkuu Nifah nawe umekata tamaa? Kama ni kweli hao watu wamenunuliwa basi hata ije katiba mpya usitegemee chochote maana hawa wanaonunuliwa ndio hao hao tutakuwa nao kwenye katiba mpya
 
hamuiwezi ccm kwa sababu hamna watu wanaojua siasa, mageuzi ni safari ndefu siyo swala la kuamka na kuchukua nchi.wakati wananchi wameanza kupata mwamko wa mageuzi kwa kauli mbiu ya vita vya ufisadi ghafla mkawasaliti wananchi na kumchukua fisadi nkuwa mgombea wenu wa urais,kitendo hicho si tu kiliwachanganya wananchi bali kilirudisha nyuma mageuzi ya ukweli na kuwapa nafasi ccm ya kujisahihisha kwani wametambua wananchi wanataka mabadiliko na hawataki ufisadi sasa hivi kila mtu anaongelea kutumbua majipu na sio tena ufisadi kwani kiongozi wa mafisadi tayari amehamia kule walikoanza kumwita fisadi
Huku kuwanunua watu ndio kujisahihisha? Basi shughuli bado pevu
 
Kumbe nipo jukwaa la polifix....sorry ni siasa
Ngoja nipite fasta
[emoji102] [emoji102] [emoji102] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Hakuna lolote litakalotokea , acha wasiwasi mkuu , tumewashika bapaya sana , hakuna mwenye uwezo wa kununua hata diwani mmoja wa UKAWA .
 
Huyo ni kada wa ccm tu alikuwa anapima kina cha maji na kusikia ya upande
mwingine hana lolote! Kawakuta nyie wasikilizaji wa mabadiliko mkaogopa; wangekuwepo makamanda wa kweli angewataja hao anaojidai
wameshanunuliwa; vinginevyo wangekiona kilichomnyoa kanga manyoya!
ccm ina mbinu za kishamba sana !
 
Sio umeya tu,hata Zanzibar mpaka sasa CCM ndio washindi.
Tutakapoweza kuing'oa CCM madarakani,na ni baada ya kupata katiba mpya pendekezwa ndipo tutakapoweza kufanya ya maana,tofauti na hapo ni ngumu kuzuia figisu figisu za CCM.
Hivi Ni Kweli tunaweza kuzeeka bila Kuona MABADILIKO yeyote? Hii kitu inauma sana, binafsi nilikua naamini kizazi chetu Ndio Muda muafaka wa kufanya MABADILIKO ya Kweli Kama kizazi cha Miaka ya 1950s-1960s.. Ila kwa jinsi upepo unavyovuma Ni Kama vile Hakuna lolote litakalofanyika, hii kitu inaniuma sana sio Siri.
 
Back
Top Bottom