juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,463
Habari wanajamvi,leo nikiwa nimetoka k,koo naelekea zangu makumbusho ofisini kwangu,nilikuwa kwenye daladala.mara kukazuka story kuhusiana na meya wa jiji la DSM,kuna jamaaa kaongea jambo ambalo imenibidi niamini kwa kiasi fulani hasa kutokana na figisufigisu zilizotokea.jamaa anadai ya kwamba ccm wana mpango wa kuwanunua madiwani 11kutoka ukaww ili wampigie kura mgombea wa ccm.jamaa akaenda mbali zaidi na kusema hadi sasa wamefanikiwa kurubuni na kuwapa pesa madiwani 6 bado wa5 ili kazi iishe na ndipo waitishe uchaguzi,inasemekana wanachelewesha kwa sababu wanataka wahakikishe wamewapata hao wajumbe 11 na ndipo waitishe uchaguzi,,sasa kama ni kweli hizo habari basi ccm hawawezekani na ni bora mtu ufanye shughuri zako za kimaisha kuliko kufuatilia siasa za africa maba zote zipo sawa,laaana hii sijui tuliachiwa na nani ya kutofuata democracy