Ni kweli CCM huwa mnaumizana ninyi Kwa ninyi, Mnatoa faida Kwa...

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,504
3,499
Nianze Kwa kusema hivi!! Mimi si mwana CCM Ila ni mshabiki wa kutupwa Kwa JPM na Baadhi ya viongozi katika Chama

Siasa zangu si za kuwa mwanachama wa Chama Fulani, Ila ni mshabiki wa mtu yeyote makini kutoka Chama chochote cha siasa, sifungwi na Chama chochote kile.

Sasa basi, kuna mambo huwa yanafanyika katika Vyama hivi Nayo si ya kuvumilia hata kidogo, kwani ni ya kuumizana pasipo sababu yoyote.

Yanayoendelea Makurunge katika (W) ya Bagamoyo mkoa wa Pwani katika kijiji cha Makurunge ni cha kuumizana tu na sio siasa tena.

Awali kulikuwepo na M/kiti wa kitongoji eneo Hilo, vipindi kama vitatu mfululizo, M/kiti huyo wa kitongoji, amewatumia wananchi wa mahali hapo Kwa namna alivyoweza, alidiriki kuuza hata maeneo ya Chama chake pindi alipokuwa M/kiti wa kitongoji hicho

Uchaguzi uliopita wananchi walimkataa, wakamchagua Mtu mwingine, sasa basi, huyo mtu hakupenda, na Yeye alikuwa na Nguvu Sana Kwa viongozi wa juu, kiasi kwamba alikataa kukabidhi ofsi Kwa M/kiti kitongoji mpya, viongozi wa (W) Walishindwa kuamua, na Jambo Hilo Hadi likafika Kwa Katibu mkuu Bashiru ndipo m/kiti mpya akapewa ofsi

Sasa, imeenda, huyu jamaa aliyekuwa M/kiti wa zamani Makurunge, akomba nafasi ya Udiwani akapewa hiyo nafasi Kwa figisufigisu vilevile,

Sasa vita vimekuwa Kwa huyo m/kiti kitongoji na huyo aliyekuwa m/kiti zamani akiwa kwenye nafasi sasa ya kugombea udiwani, Wakati m/kiti wa zamani na mgombea Udiwani akimsagia Meno m/kiti kitongoji mpya, wananchi wako Kwa m/kiti mpya, na Kwa sababu sasa ni vita, wananchi wameungana na M/kiti mpya kumkataa huyo mgombea Udiwani walioletewa na viongozi (W) Kwa sabb sio chaguo Lao, kwani alipitisha lupia ili apite

Ikumbukwe, huyo mgombea Udiwani aliwahi kuuza maeneo ya viwanja vya CCM na m/kiti kitongoji mpya Kwa juhudi zake ameweza kuvirudisha mikononi mwa Chama

Sasa huyo kitongoji, anachezewa rafu mbaya na ushirika wa viongozi wa juu ngazi ya (W) Kwa sababu anampunga na pengine kuna mkono pia wa wafanya biashara

Kinachofanyika sasa, Kwa kuwa huyu kitongoji mpya Hana kiongozi yeyote wa juu wa kumsikiliza, basi ameamua naye kuungana na mgombea Udiwani Kutokea Chadema ili tu hasimu wake akose hiyo nafasi ya Udiwani, na wananchi wameamua kuwa wamoja, wako pamoja na m/kiti huyo mpya, wananchi mbali na kutokukuibali Chadema wameamua kuikacha CCM Kwa namna hiyo

Inavyoonekana sasa, tayari Uongozi wa juu wameshafahamu Kinachoendelea hapo Makurunge kwamba kukwama Kwa Kampeni za mgombea wao zinasababishwa na M/kiti huyo mpya, wanachokifanya ni kumwonea huyu Kijana, navyozungumza hivi sasa, ni vurugu tu zinazoendelea hapo

Ombi langu, Uongozi wa juu, ingilieni Kati ugomvi huo ili kuepusha mengi, Chunguzeni ili kubaini ukweli na ili yasije Kutokea makubwa na mabaya kuliko yaliyopo leo
 
Mambo nisiyoyapenda kwenye siasa ni kama haya!

Na ndiyo maana wanasiasa wanaongoza kurogana!
 
Back
Top Bottom