Ilikuwa siku ya jumamosi nikiwa sina hili wala lile, nikasema acha nishike simu niingie kwenye contact list yangu mana kuna upwiru ulikuwa unanikaba koo.
Baada ya kushusha shusha nikakutana na number yake Jesca, huyu dada alikuwa akitesa sana akili yangu siku nyingi nilikuwa nakesha nikimtafuta mpaka usiku wa manane lakini alikuwa akijibu message zangu kifupi.
Huyu alifanya nipate maumivu makali yaliyoitafuna akili yangu na kuufanya moyo usinyae pale tu ntakapolikumbuka jina lake.
Lakini hii siku sasa nikasema acha nijinywee walau Safari Lager kadhaa nilipozimaliza ndio akili ikaelekea katika kushusha number za simu kwenye simu yangu.
Number ambazo niliapa kutofuta hata nini kitokee, mana alishakuwa akizunguka kwenye barabara ya ubongo wangu kila wakati, nikiwa na imani iko siku atakubali ombi langu.
Sasa baada ya kuona number yake ilibidi nianze tena upya kumweleza jinsi gani nilikuwa nikimuwaza na natamani awe mtu wa muhimu kwenye maisha yangu.
Mwamba nikajitusua huku nishafikisha chupa kadhaa za Safari Lager.
Nikamtext mida kama ya saa sita usiku hivi bahati nzuri huyu mlimbwende alikuwa bado hajalala.
Mimi: Jesca mambo
Jesca: Poa, vipi.
Mimi: Safi kabisa, za masiku mengi.
Jesca: Nzuri tu, nani mwenzangu?
Mimi: Jamani Kumbe ulishafuta na number zangu ?
Jesca: Ndio number za nini na sina mawasiliano na wewe?
Mimi: Ahaa, basi mimi ni Kijana Mpole naamini utakuwa umenikumbuka.
Jesca: Aaaah jamani, samahani sana Kijana ndio nishakukumbuka.
Mimi: Sawa, naomba kidogo kesho tutawasiliana.
Jesca: Sawa, usijiskie vibaya lakini.
Mimi: Usijali.
Jesca: Usiku mwema.
Mimi: Na kwako pia, ulale salama.