Kama Mrosso anadai Ole sabaya alitishia kumpa kesi ya Uhujumu uchumi ndipo akatoa tsh 90m, Inawezekana hata kesi ya Mbowe ina mkono wa DC!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,952
141,941
Baada ya kufuatilia kwa makini ushahidi wa Mrosso kwenye kesi ya Sabaya nimegundua inawezekana ni kweli watu huwa wanabambikiwa kesi kwa maslahi binafsi.

Sasa ndio najiuliza ni nani alitoa taarifa polisi kuwa mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe alitaka kumuuwa mkuu wake wa wilaya mh Lengai Ole Sabaya?

Ni tafakari pana sana.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimeidharau sana baadhi ya Majaji, tuna majaji wa kisiasa, wajinga na wasio na huruma kisa kuwafurahisha wakubwa. Dhambi hii itawala wao na vizazi vyao, wajiulize kwanini watoto wao hawakosi changamoto za maisha, ni mashoga, wasagaji, wabwia unga, wengine watoto wao ni wagumba/tasa etc ni kutokana na dhuluma hizi kwa damu zisizo na hatia
 
Hii kesi ilitengenezwa na jambazi Sabaya ikakosa baraka za mwendazake, hivi kweli Mbowe apange ugaidi mwendazake amuache afanye kampeni mpaka afariki bila kumtia nguvuni!!?.
 
Nimeidharau sana baadhi ya Majaji, tuna majaji wa kisiasa, wajinga na wasio na huruma kisa kuwafurahisha wakubwa. Dhambi hii itawala wao na vizazi vyao, wajiulize kwanini watoto wao hawakosi changamoto za maisha, ni mashoga, wasagaji, wabwia unga, wengine watoto wao ni wagumba/tasa etc ni kutokana na dhuluma hizi kwa damu zisizo na hatia
Tulieni Mbowe anyolewe,wembe ni ule ule!!!
 
Changamoto yako weye ni kwamba:
-kuna kipindi unakuwa mtoto
-kuna kipindi unakuwa kivulana
-kuna kipindi unakuwa baba mtu mzima wa afya mwili mzima
-kuna kipindi unakuwa mzee Mgaya
-kuna kipindi unakuwa mpangaji wa "Milembe Hotels"
-kuna kipindi upoupo tu
Tafrani!
Hahahaaaa......!

Mimi huyo?!!!

Acha hizo bwashee!
 
Chadema kama taasisi ya kutetea haki na demokrasia nchini,kama mnavyojinadi.
Mlitakiwa kutetea haki za walio wengi nchini. Na si kukaa kimya na kusubiri yamkute mwenyekiti wenu gaidi mshukiwa.

Sasa mnakosa usingizi, shughuli za chama mmesimama.
Mmebakiza kuhudhuria mahakamani na kwenye kumbukumbu za misiba.

Mbowe ni kiongozi mmoja tu kati ya wengi mlionao,kama taasisi.

Je ikitokea Mbowe akawa hayupo chadema kwa sababu zozote zile za kibinadamu au ki - MUNGU,tuseme ndio itakuwa mwisho wa Chadema?.

Sasa hivi kama taifa, tunaona na kupitia mambo mengi ambayo yanatokana na maamuzi mabaya ya baadhi ya wateule wa Rais samia.

Ambayo kwa hali halisi yanatia shaka na yalipaswa kukemewa hadharani kutokana na kuwa na sura za kifisadi.

Na hii kazi ndio ingefanywa rasmi na uongozi makini wa upinzani nchini.

Zitto na ACT yake yeye tayari tumekwisha muona amechagua upande wa upatu kwa maslahi yake, kama kawaida yake.

Sasa nyinyi Chadema,kina Mnyika kama na katibu mkuu na kundi lenu wote mlioko huru uraiani. Kila uchao mnaimba Mbowe!...Mbowe!...Mbowe!

Je kisa ni kuishiwa ubunifu wa mbinu za kufanya siasa au nini?

Au kisa ni yeye kuwa Signatory wa treasury,wa cheque zote za benki na kutokuwepo kwake kunakwamisha masuala ya kifedha?

Tuliona Enzi za ANC huko south afrika, pamoja na kiongozi wao mkuu Hayati Nelson Madiba Mandela kuwekwa jela na utawala dhalimu wa makaburu.wale makomredi waliobaki huru wakiongozwa na hayati Solomon Mahlangu.Waliendeleza harakati bila kuchoka toka pande zote za africa na dunia.

Sasa nyinyi kaeni mnaimba Mbowe na kuhudhuria Space ya Maria Sarungi na Fatuma karume,(ambao kimsingi tayari wanatumia the space kuingiza kipato.).

huku wenzenu CCM wakichanja mbuga kona zote nchini,halafu 2025 ikizidi kusogea.

Halafu mnakuja kukurupuka kukumbuka shuka Alfajiri,kisha mnaanza kulia mmeibiwa kura.

Ukweli lazima tuwaambie...sijui mnakwama wapi!

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Changamoto yako weye ni kwamba:
-kuna kipindi unakuwa mtoto
-kuna kipindi unakuwa kivulana
-kuna kipindi unakuwa baba mtu mzima wa afya mwili mzima
-kuna kipindi unakuwa mzee Mgaya
-kuna kipindi unakuwa mpangaji wa "Milembe Hotels"
-kuna kipindi upoupo tu
Tafrani!
Malaya Malaya wa kuchangia na kuibua hoja.
 
Baada ya kufuatilia kwa makini ushahidi wa Mrosso kwenye kesi ya Sabaya nimegundua inawezekana ni kweli watu huwa wanabambikiwa kesi kwa maslahi binafsi.

Sasa ndio najiuliza ni nani alitoa taarifa polisi kuwa mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe alitaka kumuuwa mkuu wake wa wilaya mh Lengai Ole Sabaya?

Ni tafakari pana sana.

Maendeleo hayana vyama!
Karibu mashahidi wote waliokwenda RAU kuwakamata wale makomredi wanaulizwa nani alikua msiri wa Mahita lkn hakuna anaetaja
 
Karibu mashahidi wote waliokwenda RAU kuwakamata wale makomredi wanaulizwa nani alikua msiri wa Mahita lkn hakuna anaetaja
Huwezi kumtaja informer,utakuwa umemsaliti na pia ni kinyume cha sheria.
Wewe tulia maana huujui ukachero na kanuni zake.

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kufuatilia kwa makini ushahidi wa Mrosso kwenye kesi ya Sabaya nimegundua inawezekana ni kweli watu huwa wanabambikiwa kesi kwa maslahi binafsi.

Sasa ndio najiuliza ni nani alitoa taarifa polisi kuwa mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe alitaka kumuuwa mkuu wake wa wilaya mh Lengai Ole Sabaya?

Ni tafakari pana sana.

Maendeleo hayana vyama!
Ndiyo kazi kuu ya CCM kubambika watu kesi
 
Back
Top Bottom