MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Tukubali tukatae, upinzani nchini una hali ngumu sana sio kifedha tu bali pia katika uhamasishaji! kwa kifupi, HAUKUJIPANGA VIZURI
Mkutano wa ufunguzi wa CHADEMA umetoa majibu mengi kuhusu mustakabali wa vyama vya upinzani nchini. Kupiga kelele nyingi haina maana kuwa wanaopiga kelele ni wengi! Ufunguzi wa kampeni wa CHADEMA umedhihilisha usemi huu
Pamoja na CHADEMA kuchagua sehemu yenye uwanja mdogo katika ufunguzi wa kampeni lakini hata kuujaza walishindwa
Kama CHADEMA ambayo ''tunaambiwa ina mgombea anayesubiri kuapishwa'' inakuwa katika hali ile kwenye ufunguzi wa Kampeni, vipi itakuwa kwa Bernard Membe ambaye safari yake ya kwenda Ikulu inafifia kabla hata ya kufungua kampeni za ACT-Wazalendo kitaifa
Kwa niliyoyaona kwa CHADEMA, kama wapinzani hawataungana haraka sana kuna hatari ya bunge kuwa na wabunge kutoka CCM zaidi ya asilimia 90!
Ninajua kuna ''manazi'' wa upinzani watakuja hata ''kupiga kelele'' lakini hali halisi itabaki kuwa hali halisi.
Kwa mfano, upinzani utaitishaje maandamano ili kupinga suala fulani na kupata waandamanaji wengi na wenye kukabiliana na lolote wakati vyama vya upinzani vinawekeana mapingamizi NEC.
Tatizo CHADEMA wamewakashfu/kuwatukana CUF na NCCR-Mageuzi wakati hawajaufikia mto achilia mbali kuuvuka! Kwa sasa ninavyodhani itakuwa vigumu CUF na NCCR-Mageuzi kuungana na CHADEMA.
Huu ni ushauri tu kwa sababu ninapenda angalau upinzani uwe na asilimia 30 ya wabunge wa Tanzania!
Kuna msemo usemao, ''Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafula, wala hapati dawa'