mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Yapo maswali mengi ya kujiuliza kuhusu ufunguzi wa kampeni ya CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu:-Refernce picha ya TBC iliyopigwa saa tatu asubuhi?
1) Japo yawezekana ni picha ya TBC ilikuwa ya asubuhi, hata "video clip" ya msafara kuelekea kwenye ufunguzi wa kampeni ilipigwa na TBC? Je, viongozi wameona umati wa watu barabarani wakiwashangilia?
2) Kwamba CHADEMA haina Idara ya Mawasiliano na Mahusiano imara ya kuandaa kuonesha mubhashara shughuli muhimu kama hiyo?
3) Kwamba CHADEMA haina Ilani ya Uchaguzi ila mwendelezo wa lawama na madai yale yale dhidi ya Serikali?
4) Je, ilikuwa sahihi kupitisha bakuli la msaada bila kuwaambia unaowaomba msaada iwapo wakikipa CHADEMA ridhaa yao ya kuingia Ikulu watarajie nini?
Itoshe kusema kuwa Viongozi wa CHADEMA, wakubali zamu hii wamekosea na hawakuwa na maandalizi ya kutosha. Hivyo basi waombe msamaha ndipo wawe na UHALALI wa kuishutumu Serikali. Pia wasiwaombe wanachama na wafuasi kuandamana kwa hicho wanachoita madai bila kuwambia ni kwa maslahi ya nani kama siyo ya viongozi kupata madaraka.