Kama madereva wameweza, walimu kinachowashinda ni nini?

Kama madereva wameweza, walimu kinachowashinda ni nini?

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,494
Reaction score
12,462
Haki isipopatikana kwa njia ya majadiliano, basi kuna namna nyingine ya kudai haki hiyo. Jana na leo tumeshuhudia madereva wakigoma na mgomo wao umefanikiwa kwa 98%.

Swali kwa walimu; Kinachowashinda ni nini? Maana migomo yenu imekua na mafanikio 0% na tunaamini nyie ni wasomi zaidi ya madereva, sasa kulikoni mnafeli kudai haki zenu?

Sio uchochezi huu jamani, ila ninahoji failure ya walimu kudai haki zao!!

Kazi njema!!
 
Tatizo njaa halafu hawana umoja kama ukawa!
 
Haki isipopatikana kwa njia ya majadiliano, basi kuna namna nyingine ya kudai haki hiyo. Jana na leo tumeshuhudia madereva wakigoma na mgomo wao umefanikiwa kwa 98%.

Swali kwa walimu; Kinachowashinda ni nini? Maana migomo yenu imekua na mafanikio 0% na tunaamini nyie ni wasomi zaidi ya madereva, sasa kulikoni mnafeli kudai haki zenu?

Sio uchochezi huu jamani, ila ninahoji failure ya walimu kudai haki zao!!

Kazi njema!!
Wamefanikiwa nini sasa.., eenh.., em' tueleze kiundani walichofanikiwa..!

1.)Je, wamefanikiwa kuwakosesha watoto wao mitihani ya kidato cha 6?
2.)Je, wamefanikiwa kupoteza kipato chao binafsi kwa kutofanya kazi?
3.)Je, wamefanikiwa kuwatia ndugu zao hasara kwa kushindwa kwenda kwenye mihangaiko yao?
4.)Je, wamefanikiwa kushusha shillingi zaidi kwa kusimamisha shughuli za uzalishaji huduma na bidhaa?
 
Walimu muajiri wao ni serikali ila madereva wa mabasi sio waajiriwa wa serikali, pia walimu wakitaka kugoma wangeunganisha madai na makundi mengine sio wao peke yao mfano ungekuwa wakati mzuri kwa makundi yanayonyanyasika kimaslahi kama walimu, madaktari, na madereva kukaa pamoja na kuungana wakati kama huu na kujadiliana namna ya kudai maslahi yao kwa serikali mpaka akili iikae sawa sawa, na kuheshimu kazi na maslahi ya makundi mengine, ni mtazamo wangu tu.
 
"shemeji unatuachaje"?

CWT huwa

au ngoja niache sheria ya mitandao itaninaniliu
 
waalimu wanatakiwa wasiwe waoga mbele ya serikali yao watashinda tu
 
waalimu waoga sana na huyo raisi waaaoooo wa cwt ndo kapata uraisi wa tucta ndo kabisaaaaaaaa
 
Kama hilo la udereva la kusoma kila baada ya miaka wanasiasa watakayotaja likifanikiwa kwa kuwa tu madereva wanaendesha magari na kwamba magari ni chanzo cha agali basi pia hata madaktari nao wawe wanarudi vyuoni kusoma kila baada ya miaka mitano kwa kuwa kuna some circumstances wagonjwa hufa....Polisi nao warudi depo kila baada ya miezi sita kwa kuwa mbinu za kiuhalifu zimekuwa advance kuzidi mafunzo waliyonayo!
 
Kazi tu kumsifia shemejii ona madereva walivyokuwa na msimamo mpaka viongozi wanahaha kila kona nyie mmebweteka mnasubiri vi inclimental tu mna madai ya msingi viongozi wenu wamelala usingizi wa pono tu.
 
Huyu naye!

Mshahara wenyewe napewa tarehe 45, hapo ni bila mgomo!

Hivi unadhani mpaka sasa, nigome au nisigome, nitapunguza ama kuongezea nini taifa?

Niache kama nilivyo..

''Mwalimu wa la saba C''!:becky::becky:
 
walimu wengi ni wanawake tena wamama watu wazima. hawana mbinu mbadala ya maisha, na wengi wapo vijijin. lakini pia wana uhakika kwa asilimia fulani kwamba mwisho wa mwezi akaunti inasoma. Ukimwambia agome hakuelewi.
Madereva 99.99% kama sio wote ni wanaume. Wengi wao wanapatikana au kuishi mijini. hawana uhakika na ajira zao. hawana cha kupoteza kwa hiyo ni rahisi kugoma
 
Kiongozi gani anahaha? Mbna Pinda naskiaa yupo kwenye kikao cha send- off ya mtoto wa dada ake!
 
Broo Chinga One mwalimu ni muajiriwa serikalini, ili agome, kuna taratibu za kisheria kufikia huo mgomo, hususan chama chao cha waalimu, sasa hawa madereva hawako hivyo..!!!
 
Last edited by a moderator:
Mbona wewe hujagoma.?

QUOTE=Chinga One;12643871]Haki isipopatikana kwa njia ya majadiliano, basi kuna namna nyingine ya kudai haki hiyo. Jana na leo tumeshuhudia madereva wakigoma na mgomo wao we mbona hugomiumefanikiwa kwa 98%.

Swali kwa walimu; Kinachowashinda ni nini? Maana migomo yenu imekua na mafanikio 0% na tunaamini nyie ni wasomi zaidi ya madereva, sasa kulikoni mnafeli kudai haki zenu?

Sio uchochezi huu jamani, ila ninahoji failure ya walimu kudai haki zao!!

Kazi njema!!
[/QUOTE]
 
Kama hilo la udereva la kusoma kila baada ya miaka wanasiasa watakayotaja likifanikiwa kwa kuwa tu madereva wanaendesha magari na kwamba magari ni chanzo cha agali basi pia hata madaktari nao wawe wanarudi vyuoni kusoma kila baada ya miaka mitano kwa kuwa kuna some circumstances wagonjwa hufa....Polisi nao warudi depo kila baada ya miezi sita kwa kuwa mbinu za kiuhalifu zimekuwa advance kuzidi mafunzo waliyonayo!

nimeipenda sana....
power 2u.
 
Back
Top Bottom