Kama madereva wameweza, walimu kinachowashinda ni nini?

Kama madereva wameweza, walimu kinachowashinda ni nini?

Ukikaa na wajanja muda mwingi nawe uyakuwa mjanja!

Ukikaa na kuku muda mwingi nawe utakuwa na akili kama za kuku, mbwa vilevile.

Walimu hawawezi kugoma kwa sababu zifuatazo:-

1. Wanakaa na watoto muda mwingi, akili zao ni za kitoto kitoto.

2. Wengi wao wanatumia vyeti ambavyo siyo vyao.

3. Wakigoma watakosa T-shirts za uchaguzi toka kwa anayewanyonya.

4. Wanaridhika na mishahara yao.

5. Huwa wanatumiwa kwenye uchaguzi na kupewa viposho.

6. Serikali inawalipa vizuri.

7. Jamaa kaoa mwenzao, hivyo kugoma ni kutaka jamaa amfukuze mkewe-wanaogopa kumwalibia ulaji mama Salimer.

8. Wanapewa mshahara wa miezi miwili pasipo kufanya kazi-mwezi wa sita na wa kumi na 2 tofauti n kada nyingine.

9. Hata ada za kulipia masomo yao kwa miaka yote ni za chini sana kuliko hicho kiasi cha madreva kusoma wiki mbili tu.

Wajanja watakuwa wamenielewA
 
Kama hilo la udereva la kusoma kila baada ya miaka wanasiasa watakayotaja likifanikiwa kwa kuwa tu madereva wanaendesha magari na kwamba magari ni chanzo cha agali basi pia hata madaktari nao wawe wanarudi vyuoni kusoma kila baada ya miaka mitano kwa kuwa kuna some circumstances wagonjwa hufa....Polisi nao warudi depo kila baada ya miezi sita kwa kuwa mbinu za kiuhalifu zimekuwa advance kuzidi mafunzo waliyonayo!

ww jamaa unaakili sana.
 
mgomo wowote huwa unaathiri jamii inayopata huduma mfano:-mgonjwa kwa daktari, dreva kwa abira, mwalimu kwa mwanafunzi, baada ya mifano hiyo nadhani majibu unayo, hii inchi kila mtu alishagoma imebaki bora liende. We endelea kusomesha kayumba int, majibu utayapata
 
kama unaishi karb na mwl. angalia mwenendo wake....hawajielew kbsaaa....waoga hadi mtaani...nadhan kisaikolojia wamejengewa shida
 
Mkuu tutajie mgomo wa madaktari ambao umefanikiwa kama wa madereva uliowasifia.
Ule wa mara ya mwisho ulikuwa mkubwa sana ila ulizimika baada ya kiongozi wao kupelekwa Mabwe Pande University College. Viongozi wa madereva nao wawe makini kile chuo bado kipo na rama mkuu wa chuo naye yupo feri white house
 
Umetumia vigezo gan kujua umefanikiwa 98% wakati feedback ya mazungumzo bado mwalimu?
 
Ni Mara ya Kwanza kwa Madreva kujijua na kudai haki zao.

Imezoleka kuwa kada ya madreva ni watu wa kada za chini katka ajira, ambapo wengi wao ni Standard 7 leavers. Mtu aliyekaa darasani miaka saba sio wa kubeza kama elimu ni bora kama Kenya ama UK.

Madereva ni watu muhimu sana katika jamii na wanatoa huduma kwa mapana sana. Cha ajabu madreva hawana chombo imara kama CHODAWU ama CWT.

Kada nyingine yenye watu wengi na huduma pana kwa jamii ni Waalimu. Ila walimu kasoro yao wanakuwa waoga, shangaa madeni yao yanakuwa mpaka mabilioni na Cha kushangaza wanakuja kulipwa mwaka wa Uchaguzi kwa sababu za kisiasa... Walimu MPoooo,, CWT vipi?

Walimu ndo wakukatwa mishahara kuchangia mwenge na maabara.

Kitendo cha Madreva kugoma ni kwamba Watanzania haoooo, wameamkaaa

 
Posho za muda mfupi zinawalaghai waalimu..

Wanalipwa madai yao ya muda mrefu wakati wa Uchaguzi
 
umesahau ndo kada inayoongoza kwa vyeti vya kughushi??? mtu aliyeghushi anaweza kuwa na msimamo?? au akili za kitu anachoghushia, haiwezekani
 
Haki isipopatikana kwa njia ya majadiliano, basi kuna namna nyingine ya kudai haki hiyo. Jana na leo tumeshuhudia madereva wakigoma na mgomo wao umefanikiwa kwa 98%.

Swali kwa walimu; Kinachowashinda ni nini? Maana migomo yenu imekua na mafanikio 0% na tunaamini nyie ni wasomi zaidi ya madereva, sasa kulikoni mnafeli kudai haki zenu?

Sio uchochezi huu jamani, ila ninahoji failure ya walimu kudai haki zao!!

Kazi njema!!

Zile siku saba za Makonda hazijaisha tu? au wameshatimiziwa madai yao? wale mama lishe wa ubungo maziwa wameshamaliza kuwalipa madeni yao?
 
Walimu mgomo wao wanafanyia kwenye baloti boksi.Wanasubiri viparata vya kumpigia Dr.Slaa
 
Tatizo hawana umoja na kila mmoja yuko bize na tuisheni,
 
Watanzania tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe,,, ni Uogaaa

Maandamano.... Maandamano..

Wafanyakazi wanasema eti mishahara ni midogo.....

Wakulima na wafugaji wamepandishiwa bei ya mafuta taa...

Watanzania tuamke.... Tuendako ni kubaya.... Hawa Madikteta na mafisadi yatakuja kutunyang'anya hata waume ama wake zetu..

Watetezi wetu UKAWA wanatolewa Bungeni halafu tumekaa kimya wananchi..

Ndio Maaana wanafanya ufisadi mchana kweupe na wanarudia tena, Watanzania tunasahau, wanarudia tena..

EPA, Ikaja RICHMOND, IKAJA ESCROW..... na bado.....


Watanzania Tunauzwa.... Miswada ya kutuuza miaka 100 ijayo..

Deni la Taifa Tanzania limekuwa... Tutalipa miaka 50 ijayo

Kodi wanatukamua mpaka mafuta taaa, aargh

Jumatatu ASB... hakuna Dala dala kutembea, hakuna wafanyakazi kwenda kazini, Maduka yote yafungwe....

Jamani, hata kama kwa simu tumeshindwa (sheria) basi kwa Facebook jee, Kwa Twitter je.

Tunashindwa hata na Burundi...

Wakenya walipeleka Damu ya Nguruwe bungeni..... Wakenya wanatucheka....

Watanzania tujitoleee.....
 
The case,siyo kwamba walimu,madaktari,polisi,madereva ama watumishi wa kada mbali*2 za uma ni waoga au hawajitambui.
Tatizo lipo kwa watanzania wenyewe.
Je,waTZ wamesupport harakati za mageuzi mara ngapi?
Mungu Tusaidie waTanzania!
 
Kazi ya ualimu ni wito...wao wanalijua hilo!!ndo mana ni wavumilivu sana!ingawa yoga
wao ndo unawafanya wafe maskini
 
Tatizo la walimu ni c.w.t...ina link name watawala.kassim .mama sitta walipita huko unategemea nini
 
kama unaishi karb na mwl. angalia mwenendo wake....hawajielew kbsaaa....waoga hadi mtaani...nadhan kisaikolojia wamejengewa shida

acha dharau wewe! fikiri kabla hujaandika walimu ni jeshi kubwa huwezi kufanya tathmini kwa mwalimu mmoja na ukatoa majibu
 
Haki isipopatikana kwa njia ya majadiliano, basi kuna namna nyingine ya kudai haki hiyo. Jana na leo tumeshuhudia madereva wakigoma na mgomo wao umefanikiwa kwa 98%.

Swali kwa walimu; Kinachowashinda ni nini? Maana migomo yenu imekua na mafanikio 0% na tunaamini nyie ni wasomi zaidi ya madereva, sasa kulikoni mnafeli kudai haki zenu?

Sio uchochezi huu jamani, ila ninahoji failure ya walimu kudai haki zao!!

Kazi njema!!

Kimtazamo wangu nadhani waalimu wameumbiwa Huruma. Kwasababu wanaowasumbua na hela zao na kazi yao ni wenye pesa. Na sio watoto wa walala hoi. Hizi shule zetu wanasoma watoto wa walala hoi. Mwalimu anapowaza kugoma hupata shida sana
 
Back
Top Bottom