Kama kuna kitu Watanzania tunakihitaji basi ni maarifa

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Naam, wanajamvi siku tatu za maombi zimeisha Jana. Kama maombi ya waombaji yameswihi hilo litajidhihirisha siku si nyingine kuanzia leo.

Ila kwa maoni yangu hayajaswihi au hajapokelewa. Kwanini nasema hivi? Ni ubatili wa maombi yenyewe. Waombaji wengi walimtukuza binadamu badala ya Mungu. Rejea maombi ya RPZ mmoja wa A Town.

Aisha, maombi huhitaji utulivu bwana, mnapata wapi ujasiri wa kuomba huku mnamlikwa na mikamera lukuki?

Kabla ya maombi Mungu anataka tufanye toba ya kweli. Tunajua kuigiza Watanzania sisi! Binafsi nilitamani kabla ya maombi tungewaachia huru Mashehe wa uamsho wote bila masharti, Tumwachie Singasinga na Rugemalila, Tuwaachie wafungwa wote wa kisiasa, Tumwombe radhi Tundu Lissu n.k Ndio twende mbele za Mungu kumuomba huruma yake aiangamize Covid-19.

Kwa niliyo yaona ni kama wengine walikuwa wanamfokea Mungu badala ya kumtukuza. Tumeicha dini kwenye mikono batili isiyo na maarifa.

Hakika tunahitaji maarifa.
 
Kila nimwombalo Mungu hunijibu
Haijalishi najibiwa vipi
Haijalishi najibiwa lini
Sio lazima ajibu ninavyotaka
Mwachie Mungu kazi ya kutujibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAOMBI bila ya TOBA ni ubatili. Hiyo ndiyo hoja ya JERUSALEMU.
Kama yeye hajatubu Ni yeye sio wote
Yeye alikuwa busy kuangalia maigizo. Sisi tulikuwa busy kutubu na kuomba. Tumetubu kwa ajili ya nchi na dunia.

Tumemlilia Mungu atuvushe na hili, Leo aseme hatujatubu?
Mambo ya rohoni awaachie wa rohoniAu alitaka Nani asimame hadharani aseme ametubu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya rohoni awaachie wa rohoniAu alitaka Nani asimame hadharani aseme ametubu?
Kuna dhambi zimetendwa na watanzania wengi wanajua, Toba wanayoitaka watu ni ya kitaifa. Kwa nini watu waambiwe waombe bila ya kuhimizwa kutubu huku wao wanaotaka watu waombe wakisema hadharani kwamba wametubu na wao kwa makosa ya taifa lao?
 
Kuna vitu vinashangaza kweli,mtu unasoma uzi wake unajiuliza huyu anaanzaje kuongea kwa niaba ya Mungu?

Mpuuzi mpuuzi tu
Na nyie nani kawaambia kwamba Mungu kapokea maombi yenu? Mbona na nyie mnaongea kwa niaba ya Mungu kuonesha kwamba maombi yenu yamepokelewa. Mmejuaje?
 
Ndugu yangu
Mungu halazimishwi,,,, huombwa
Mungu hujibu kwa wakati,,, hapangiwi
Mungu ana majibu kabla hatujamwomba
Na sio Tanzania tu
Mungu ataiponya dunia yote
Ukiona wagonjwa wanaongezeka ujue bado muda wa kuachilia
Kuna wale waliopangiwa kufa kwa hili, lazima wafe wote ndo ndo Corona iishe, tuwe na subira
Na nikusaidie tu mkuu
Si kila uombalo jibu Ni ndio
Mimi Nina uhakika hayaja pokelewa. Subiri uone Hospitali ya Amana itakavyo jaa wagonjwa wa Covid-19 by Wednesday. Jana kutwa nzima wagonjwa wanapelekwa unategemea nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma biblia utaelewa kinachotakiwa
Jukumu la kuiombea Toba nchi hii Ni la watanzania wote bila kujali Nani alifanya dhambi
Nikwambie kitu mkuu.

Dhambi (machukizo) zinazifanyika Tanzania Ni nyingi na za kutisha kuliko hizo unazoziona zimefanywa na viongozi wa kitaifa, hizi zimefanywa sirini, kwa nini hamzisemi? Au mnafikiri Mungu hawezi kutupiga kwa dhambi zetu hizi tunazoziona Ni ndogondogo? Hebu tuwe sirious.

Tutoe kwanza maboriti yetu kwenye macho yetu kabla hatujaona vibanzi kwenye macho ya viongozi wetu.

Kumbuka sodoma na gomora unaweza pata picha kidogo. Allen Kilewella,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumeomba sio kwa sababu fulani alisema tuombe, tumeomba kwa kuwa tunaamini Mungu yupo, anasikia na anajibu. Issue ya ni lini atajibu hiyo siyo issue yetu tena, Mungu anajibu kwa majira na nyakati zake mwenyewe sisi tunatimiza wajibu wetu wa kumuomba asamehe, arehemu na kuponya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila Mungu ni wa rehema sana, anatuhurumia tu pamoja na madhaifu utashangaa Covid19 imeyeyuka ghafla sijui utasemaje? God is of impossibles dont you think??

Back
Top Bottom