Kama kiwango chako cha elimu hakijafikia masters, tusikuone ukileta utafiti wako uchwara humu!

Kazi ya utafiti ni kazi iliyokuwa reserved kwa watu wenye elimu ya kuanzia masters, PhD na kuendelea.
Cha ajabu Kibongo bongo unakuta mtu wa darasa la saba eti naye anakuja na utafiti wake humu! C ni kichekesho..? Kama ulikimbia umande funga 'bakuli' lako.... Au andika kuhusu mambo mengine...
Fanya utafiti kwanza ndipo uje na madafu haya
 
kama Jacob Zuma alikua mwanaharakati mzuri tuu na alikua ana upeo mzuri tuu kuriko hata wenye Elimu kubwa South Africa mpaka kuweza kuwa mwenyekiti wa ANC 1980 na hajasoma hata darasa moja... na mpaka sasa Zuma ana uwezo mkubwa wa kufikiri kuriko wengi mlio na Masters...
 
Hili ndilo tatizo tunaloita la GPA system.....
unajua mtu anaweza kuwa na gpa kubwa ila tunawaona humu vyuoni wanavyopiga chabo katika chumba cha mtihani hivyo usijaribu kujiaminisha kuwa cheti kinareflect uwezo wa mtu.....

Pili; Elimu ipo tu kukusaidia kiutendaji mambo yaende kwa utaratibu....kwa mfano kuna tofauti ya muuza duka ambaye hajawahi kukanyaga shule na yule ambaye amesoma hata course ya book keeping ya muda mfupi.......ila linapokuja swala la utatuzi wa matatizo kwa njia hapo ni zaidi ya akili ya shule......sasa tunatofautiana katika kujiongeza........wengine huwa wanajiweza na wanaweza kutoa solution kwa kutumia akili simple mind thinking......ila kuna ambao hawawezi kabisa ndio hawa ambao hadi waende shule ndio mambo yanakwenda.........

wavumbuzi wengi wa theory na ubunifu wa kisasa hawakuenda shule rasmi ila udadisi wao ndio msingi wa kila unachokiona unakisoma darasani leo.......
kwakifupi.......unavyovisoma darasani ni akili au mawazo ya ambao hawakwenda shule wala kusoma masters......na ndio maana wewe unakwenda darasani kujipandikiza uwezo wao......sasa kwanini useme si sawa kwa wengine kudevelop new ideas kupitia tafiti bila masters.........
 
Kazi ya utafiti ni kazi iliyokuwa reserved kwa watu wenye elimu ya kuanzia masters, PhD na kuendelea.
Cha ajabu Kibongo bongo unakuta mtu wa darasa la saba eti naye anakuja na utafiti wake humu! C ni kichekesho..? Kama ulikimbia umande funga 'bakuli' lako.... Au andika kuhusu mambo mengine...
hivyo vigezo kaweka nani hadi neno lake liwe sheria,naona aibu kuwa na mtanzania mwenzangu mzigo kiasi hiki kama wewe,pole sana kwako na familia yako,kwaio hata ukichapiwa mkeo utasubiri tafiti hadi zifanywe na mtu wa masters,PhD ndio utaamini?
 
Kazi ya utafiti ni kazi iliyokuwa reserved kwa watu wenye elimu ya kuanzia masters, PhD na kuendelea.
Cha ajabu Kibongo bongo unakuta mtu wa darasa la saba eti naye anakuja na utafiti wake humu! C ni kichekesho..? Kama ulikimbia umande funga 'bakuli' lako.... Au andika kuhusu mambo mengine...

Labda kama unamchokoza Majaliwa......kama ni hivyo utajaaliwa Inshallah
 
Asilimia kubwa ya watu wanaotumia kigezo cha elimu(in the form of Form 4,6,BA,BEng or BSc Masters na PhD)kama silaha yao in reality ni v-laza waliopata academic qualifications kwa bahati mbaya.Kibaya zaidi other than papers called certificates THEY HAVE NOTHING!
I love this comment "vilaza walipata academic papers"
 
Mkuu samahani kipe heshima Chuo kikuu Mzumbe.
Kwanza hakuna usikarili kuna usikariri.

Nikikwambia utoe madhaifu ya MU utatokwa udenda. Heshima tafadhali .Heshima narudia tena.
mkuu umetokea mzumbe?
 
Mtoa mada kaandika tu kujifurahisha, na kama kweli alichokiandika anakimaanisha na ni 'msomi' basi ni hatari!
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Kazi ya utafiti ni kazi iliyokuwa reserved kwa watu wenye elimu ya kuanzia masters, PhD na kuendelea.
Cha ajabu Kibongo bongo unakuta mtu wa darasa la saba eti naye anakuja na utafiti wake humu! C ni kichekesho..? Kama ulikimbia umande funga 'bakuli' lako.... Au andika kuhusu mambo mengine...

Dogo umethibitisha dhahiri bin shayiri kwamba "Ulikwepa umande" weye! Kwani utafiti katika kichwa chako hicho ni nini mpaka utwekee kiwango cha elimu?! Una maana hata hawa madokta uchwara na maprofesa "zawadi" wanatosha ili mradi wana parmanent head damage aka Phd?! Una maradhi mabaya wewe, kamuone daktari!
 
mtoa mada naona hata shule ajamaliza hitakuwa maana kama umefika elimu ya juu uwezi kuongea kama mtu ajapita shule kabisa
 
Hata masters za bongo bado ni za uchwara,watu wanadesa mitihani hasa mitihani ya research!
 
Back
Top Bottom