Kama jambo lolote halieleweki achana nalo

Kama jambo lolote halieleweki achana nalo

Sio rahisi kama unavyodhani, mtoto wa mama mkwe ananitesa ila ndio nampenda na ndiko amani yangu ilipo.
Nawezaje kuachana nae? Acha tu niendelee kuteseka as I love him.
Kama unaona kuteseka ndio furaha yako basi kila la Kheri Mkuu.
 
Watu ukiwashauri wanaona unawaharibia hujui usemacho, imagine mtu ameomba ushauri ukampa ushauri kama huu akaanza kufoka "ina maana niachane na yule mwanamke/mwanaume nitaishije? We hufai nilijua utanishauri kitu cha maana kumbe wale wale"

Unabaki kujiuliza alikuwa anaomba ushauri afu ana majibu yake au ananipima
 
Nateseka kummiss sio vinginevyo. Umewahi kumpenda mtu halafu hapatikani na huna namna ya kumpata unamsubiri akutafute? Ndicho ninachopitia mimi.
Mbaya zaidi uwe umemkosea, Dunia yote chungu.
Basi hujalielewa bandiko langu Mkuu.

Lisome bandiko langu tena.
 
Watu ukiwashauri wanaona unawaharibia hujui usemacho, imagine mtu ameomba ushauri ukampa ushauri kama huu akaanza kufoka "ina maana niachane na yule mwanamme/mwanaume nitaishije? We hufai nilijua utanishauri kitu cha maana kumbe wale wale"

Unabaki kujiuliza alikuwa anaomba ushauri afu ana majibu yake au ananipima
[emoji23]

Kuna watu hawashauriki Mkuu.
 
Basi hujalielewa bandiko langu Mkuu.

Lisome bandiko langu tena.
"Ukiona mahusiano ni jambo gumu basi nakushauri achana nayo kuliko kujitesa kwa jambo ambalo kukaa mbali nalo ndio amani yako."
Hapa ulikuwa unaongelea kilimo Mkuu?
 
"Ukiona mahusiano ni jambo gumu basi nakushauri achana nayo kuliko kujitesa kwa jambo ambalo kukaa mbali nalo ndio amani yako."
Hapa ulikuwa unaongelea kilimo Mkuu?
Ugumu kwenye mahusiano unauelewa kwanza?

Nimesema Kama kuna ugumu na hauna amani/furaha basi chagua furaha kwa kuyaacha hayo maumivu.
 
Nateseka kummiss sio vinginevyo. Umewahi kumpenda mtu halafu hapatikani na huna namna ya kumpata unamsubiri akutafute? Ndicho ninachopitia mimi.
Mbaya zaidi uwe umemkosea, Dunia yote chungu.

Ila mapenzi acha kabisa.

Kama unajua hapatikani kwa sababu ya majukumu hapo amaani kidogo inakuwepo.

Ila kama hapatikani kwa sababu ameamua usimpate hewani inatesaaaa mpaka uzoee sio rahisi.
 
Ugumu kwenye mahusiano unauelewa kwanza?

Nimesema Kama kuna ugumu na hauna amani/furaha basi chagua furaha kwa kuyaacha hayo maumivu.
Sasa kuna mahusiano yasiyokuwa na yote hayo unayoyaongelea? Mahusiano ya furaha kila siku labda udate na mgomba. Hata mgomba wenyewe ukishazaa unanyauka, hakuna kilichokamilika.
 
Ila mapenzi acha kabisa.

Kama unajua hapatikani kwa sababu ya majukumu hapo amaani kidogo inakuwepo.

Ila kama hapatikani kwa sababu ameamua usimpate hewani inatesaaaa mpaka uzoee sio rahisi.
Wewe ndio umenielewa, nimekupenda kweli yani.
Jamani nateseka mno, mno! Unatamani ulie kila mtu asikie, Lol!
Ila nini, nampenda na haya yataisha tu mpenzi.
Asante
 
Habari zenu Wakuu.

Kama kuna jambo halina formula na halieleweki kwa njia yoyote ile eg. Mahusiano, kazi, biashara n.k basi nakushauri achana nalo.

Usijitese akili kwa jambo ambalo haulielewi Mkuu, maana utulivu wa akili ni bora kuliko mawazo yasiyoeleweka.

Ukiona mahusiano ni jambo gumu basi nakushauri achana nayo kuliko kujitesa kwa jambo ambalo kukaa mbali nalo ndio amani yako.

Kitu chochote kinachokunyima amani/furaha nakushauri achana nacho.

NB: Usifanye jambo kwasababu kuna watu wanafanya, angalia amani yako zaidi.
Nilikua na mke wa angu wa kwanza likipita lisaa nikiwa siko hewani, ana haha paka anapigia wazazi wake kuwa taarifu kuhusu, ghafra nikipatikana anaanza kulia tu, kwa kushinda kujizuia ila tuli achana badaye, so dont allow emotions to drive you at any moment.
 
Sasa kuna mahusiano yasiyokuwa na yote hayo unayoyaongelea? Mahusiano ya furaha kila siku labda udate na mgomba. Hata mgomba wenyewe ukishazaa unanyauka, hakuna kilichokamilika.
Soma tena Bandiko langu.
 
Wewe ndio umenielewa, nimekupenda kweli yani.
Jamani nateseka mno, mno! Unatamani ulie kila mtu asikie, Lol!
Ila nini, nampenda na haya yataisha tu mpenzi.
Asante

Kulia tu? Unatamani hata utafute ndugu zake uwaambie wamwambie ndugu yao aache kuutesa moyo wako.

Ila dear Mungu huwa ni mwema, unateseka sanaaaa yaani utakonda sana lakini kuna siku utaamka paaap utajikuta umezoea hadi utashangaa. Halafu ukishazoea zako hiyo hali na yeye huyooo!!
 
Back
Top Bottom