Kama in kweli hii story si mchezo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama in kweli hii story si mchezo!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Rubi, Aug 16, 2012.

 1. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mmh. sina cha kuongeza!!!

  Nilienda kumzika ibilisi wangu!
  Ilikuwa ni ajali kubwa na hata mimi sijui niliweza vipi kupona. Dereva na mke wangu walifia pale pale kwenye eneo la tukio. Tulikuwa tukitokea Chalinze kurudi Dar es salaam baaada ya kukagua shamba ambalo ilikuwa tulinunue katika kijiji cha Msata wilayani Bagamoyo. Mbele kidogo ya mji wa Chalinze ndipo ajali hiyo ilipotokea . Dereva wetu alikuwa akijaribu kulipita lori fulani lakini wakati huo huo gurudumu la mbele la gari letu lilipasuka na kusababisha gari kuyumba ambapo lililivaa lile lori. Kufuatia kuligonga huko, gari letu lilirudishwa katikati ya barabara ambapo liligongana uso kwa uso na gari lingine lililokuwa linakuja mbele yetu. Sikujua kilichotokea hadi baada ya siku mbili Muhimbili.

  Nilipopata fahamu ilinichukua muda kukumbuka kidogo kilichotokea. Nilipouliza kuhusu mke wangu hakuna aliyesema kitu kati ya wale ndugu na jamaa zangu waliokuwa pale kando ya kitanda changu. Pamoja na maumivu yangu nilijua kilichokuwa kimetokea. Nilianza kulia, hata kabla hawajaniambia chochote. Kaka yangu aliponiambia “jikaze ni kazi ya Mungu, shemeji mama Rehema ametutoka.” Nilipoteza fahamu. Nilipopata fahanu na kukubali kuipokea taarifa ile, niliambiwa kuwa mke wangu alifia pale kwenye eneo la ajali pamoja na dereva. Mimi nilikuwa nimevunjika mguu wa kushoto, mkono wa kushoto na mbavu mbili na kubanwa kifuani. Hali yangu kwa kweli haikuwa nzuri lakini nililazimika kujikaza. Mke wangu alikuwa amekufa, haikuwa rahisi kukubali.

  Nilikuwa nampenda na yeye pia alikuwa ananipenda. Ukweli ni kwamba tulikuwa tukiaminiana sana na mke wangu ambaye nitamwita Sia {Jina linalokaribiana na jina lake halisi }. Tulikuwa tumeshibana kiasi kwamba, kulikuwa hakuna ambaye alikuwa hajui. Nilikumbuka kwamba kwa miaka minane ya ndoa yetu tulikuwa hatujawahi kukorofishana, ukiacha kusigishana kwa hapa na pale. Nilikuwa sijawahi kumsaliti na hata yeye pia. Nilijaribu kukumbuka ahadi zetu kwa kila mmoja na kuhusu watoto wetu wawili mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Kwa kweli ilinichukuwa muda wa saa kadhaa kukubali kwamba nilikuwa sina mke, mwili wa yule nimpendaye ulikuwa ukiganda mochuari. Nilijikuta nikiinuka kwa nguvu na kupiga yowe nikitaka kwenda kumfufua mke wangu. Nilikuwa nimechanganyikiwa kwa kweli! Ndugu zangu na jamaa waliokuwepo pale wodini walinishika na kunituliza.

  Ilibidi waombe msaada kwa madaktari ambapo nilichomwa sindano iliyonipa utulivu na usingizi. Nilipoamka jioni sana , nilikuwa na utulivu kidogo, kaka yangu aliniomba nijikaze na kumrudia mungu, Aliniambia nijaribu kuukubali ukweli na hali halisi. Nilijikaza na aliniambia kwamba mazishi ya mke wangu ingebidi yafanyike kesho, kwa mujibu wa makubaliano ya ndugu wa pande zote. Aliniambia dereva wangu alikuwa amezikwa tayari na ndugu zake. Nilimwomba kaka wauache mwili wa mke wangu ili niwe nae karibu kwa muda fulani. Kaka alinishawishi sana nikubali kwa sababu, kama mwislamu ninajua inavyokatazwa kuuweka mwili wa marehemu bila kuuzika kwa muda mrefu, bila sababu.

  Hatimaye nilikubaliana naye, lakini nilisema ni lazima nami niende kuzika. Kaka alinimbia kwa hali yangu nisingeruhusiwa na madaktari na wala nisingeweza kumudu kwenda makaburini Kinondoni. Nilimwambia kaka katika yote ningemkubalia lakini sio hilo la kutomzika mke wangu. Nilimwambia, habari ya madaktari aachane nayo na kuhusu mimi kumudu ningemudu tu. Nilikataa katakata hata kusikiliza ilibidi kaka aondoke pale bila muafaka. Walikuja ndugu zangu wengine kunishawishi lakini niligoma kabisa, hadi ikabidi wakubaliane nami.

  Lakini walijua ingekuwa ngumu sana kutokana na hali yangu. Kesho yake walikuwa tayari wamepata ufumbuzi. Walikubaliana na uongozi wa hospitali kwamba nipelekwe makaburini kwa gari la wagonjwa. Ni kweli nilikwenda kuzika. Pamoja na kuwa waislamu huwa hatutoi heshima za mwisho kwa kuuona mwili wa marehemu, mimi nililazimisha hadi nikaonyeshwa mwili wa mke wangu. Alikuwa hana alama hata moja usoni kwani alikuwa ameumia miguuni hadi kifuani. Nilipomwona nilipoteza fahamu………… Tulimzika mke wangu na nikarudishwa hospitalini.

  Nilitoka hospitalini baada ya mwezi mmoja na kurejea nyumbani. Nyumba yangu mwenyewe ilinitisha na nilihisi simanzi kubwa kuwa mle ndani. Watoto wangu walinisikitisha zaidi. Lakini nilishaamua kuikubali hali halisi. Nilikuwa nimekubali kuanza upya maisha. Siku ya Tatu tangu kurejea nyumbani niliamua kupangua ili kuvipanga upya vitu vya marehemu. Nilipanga nguo zake na mapambo mengine ya kike. Halafu ilibidi kupanga vitu vilivyokuwa kwenye droo zake ambazo funguo zake alikuwa nazo mwenyewe marehemu. Kwa sababu sikuwa najua alipokuwa ameweka funguo za droo zile mbili ilibidi nizivunje moja baada ya nyingine.

  Droo ya kwanza ilikuwa na barua na karatasi mbali mbali za mawasiliano na mambo mengine. Hapo nilianza kuzisoma barua. Barua ya kwanza ilikuwa ni kutoka kwa mpenzi wake. Haikuwa ni barua ya zamani, kwani ilikuwa imetumwa kwake miezi minne tu kabla ya kifo chake. Ilitumwa na bwana aliyekuwa ametuuzia ile gari iliyohusika kwenye ajali iliyomuua. Sehemu ya barua ile ilikuwa imeandikwa:

  Kuhusu hilo ni sawa mpenzi wangu.
  Wewe mwambie nitawauzia kwa mkopo, tena kwa bei rahisi sana . Lakini hizo fedha utazichukua wewe. Kuhusu kwenda Harare nitakufahamisha, jaribu kwa upande wako kumwambia kwamba utakuwa na semina huko, April. Najua kufika Aprili tutaelekea huko. Nataka tuwe mahali huru na salama ili niufaidi mwili wako na wewe uumiliki wangu.


  Barua hiyo ilijaa upuuzi mwingi……

  Nilipomaliza kuisoma nilihisi kama ninayeota au ambaye nitaugua kichaa. Ni kweli huyu jamaa ndiye aliyetuuzia lile gari iliyochukua maisha ya mke wangu kwa bei ya chini sana . Gari Nissan Pajero kwa shilingi milioni 7.5 nzuri tu, hata kama imetumika! Kumbe ulikuwa ni mpango wake na mke wangu wa kuipatia familia yangu gari. Nilienda kupekua barua na hati kadhaa. Niligundua hati ya nyumba kwa jina la mke wangu.

  Nyumba hii ilikuwa Kijitonyama. Nilipata barua nyingine. Hii ilikuwa ni ya bwana wake wa zamani lakini ilikuwa imeandikwa mwaka mmoja tu nyuma, ilikuwa ikimlaumu mke wangu kwamba hakuwa mkweli Sehemu muhimu katika barua hiyo ilikuwa imeandikwa:

  Ninajua wazi huyo Rehema ni mwanangu na hata rafiki yangu Mudy amesema tunafanana sana . kama umeamua kunidanganya , ni sawa, lakini kumbuka hiyo ni damu yangu.
  Sitamchukua wala kumdai lakini kujua ukweli ni muhimu kwangu.


  Nilipomaliza kusoma barua ile nilishikwa na kizunguzungu. Nilitulia hapo kitandani kwa muda. Halafu niliendelea kupekua kwenye karatasi hizo. Niliona barua kadhaa na kadi za mapenzi.

  Kadi mbili zilikuwa zinatoka kwa bosi wake. Barua moja ilikuwa ikitoka Uingereza kwa mtu aliyeitwa P Hughes.
  Huyu ni wazi alikuwa ni mpenzi wa mke wangu kwa muda mfupi, alipokwenda Uingereza miaka miwili nyuma kwa kozi fupi ya miezi sita. Barua yake ilikuwa imejaa sifa nyingi, akimsifia mke wangu kwa kuwa na mwili mzuri na kuwa mtaalamu wa mapenzi na ilisifia shanga zake pia.

  Nilihisi nikibana kifua na mapigo ya moyo wangu yalikuwa kama yamesimama. Bila shaka siku ile ndipo yalipoanzia maradhi yangu ya shinikizo la chini la damu, ambayo ninayo hadi sasa. Nilivunja ile droo ya pili ambayo ilikuwa na picha kadhaa. Zote zilikuwa ni picha za mapenzi. Nilitazama mbili za kwanza, nikatoka chumbani mle nikiyumba.

  Naomba nisiseme sana kuhusu picha hizi, kwa sababu, hata kama mtu sio mke wako, ni mwanamke unayemfahamu tu, ukiona picha zake akiwa kwenye hali kama ile, utatahayari sana . Picha unazoziona kwenye mikanda ya ibilisi au kwenye mtandao wa inteneti ndizo zilizokuwa pale kwenye droo, zikiwa ni za mke wangu na wanaume watatu tofauti.

  Yule aliyejifanya kutuuzia gari na nyingine za wanaume wawili ambao sikuweza kuwafahamu. Baadae mchana baada ya kupata nguvu nilimpigia simu kaka mkubwa wa marehemu na kumwomba apite nyumbani. Huyu ni mtu wa hekima sana na hadi sasa tunaelewana sana.Alipofika nyumbani nilimwomba radhi na kumwonyesha barua na picha zile. Alizitazama kidogo na kunirudishia, alikaa kwa muda na kusema,
  “Huyu sio dada yangu niliyekuwa namfahamu mimi, hii ni aibu kubwa sana shemeji.” Hakuweza kusema chochote baada ya hapo, Alipoondoka kwa huzuni kubwa nilichukua nguo zote za mke wangu, barua, picha na vitu vingine vyote ambavyo vingenipa kumbukumbu yake na kwenda kuvichoma moto.

  Nilivichomea moto shambani kwangu, Kiwangwa Bagamoyo na kufukia majivu yake. Tangu siku ile hadi leo sijakanyaga kaburini kwake, watoto wake wanakwenda na huwa nawahimiza kufanya hivyo. Yule mkubwa anajua mengi hivi sasa baada ya kusimuliwa na baadhi ya ndugu. Nilimwambia kwamba maneno yale hayana ukweli.

  Lakini najua anafahamu kuwa yana ukweli, kwani kuna siku aliniiuliza, mbona haoni picha za mama yake ukutani. Nilimwambia, zinanitia uchungu zaidi. Ilibidi niende Afrika Kusini kupima DNA, ili kujua kama yule mtoto mdogo ni wangu kweli.

  Bahati nzuri ilionesha kwamba ni wangu kwa asilimia kubwa sana. Hii ilinipa moyo sana . Kilichonitokea kimenifanya nisiwe na hamu hata ya kuwa karibu na mwanamke, achilia mbali kuoa.

  Mtu ambaye umemuamini kuliko binadamu mwingine, kumbe ndiye anayefanya uasi usio na kipimo gizani. Nasema hivi mnapaswa kuwaamini wapenzi au wake zenu. Kilichonitokea mimi ni bahati mbaya na ninaamini kama marehemu angeendelea kuishi ni lazima ningekuja kumnasa.
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,182
  Likes Received: 10,534
  Trophy Points: 280
  Dahhhh!!! nimesoma yote ngoja nipate lunch kwanza. kama ni kweli, hii ni balaa.

  wanaume tumeumbwa (matesoo) x 2 kuangaika.
   
 3. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,451
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  dah...hii inagusa...:sad:
   
 4. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  babu Mtambuzi alishailetaga hii! inasikitisha wallah! wanawake they can b devils sometimes! lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Arabela

  Arabela JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 3,253
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Dah yaumiza. Jaman mambo magumu
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  inaumiza sana hii kitu!
   
 7. d

  danizzo JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh! Kichwa kinaniuma
   
 8. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Inauma sana. Yaani hata la kusema sina!!!!!!!!!!
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Du Shigongo @ work
   
 10. B

  Bi nyakomba JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 387
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ixeee.... Pole sn
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Umeogopa au? Ila híi makitu ilishaletwaga hapa na mzee mwenzangu Mtambuzi. Jamaa sijui kaenda kuyachoropoa wapi tena.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Oooooh imerudi tena na nimesikitika tena!
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mkeo sio mama yako,kama ni kukutana mmekutana ukubwani.
   
 14. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  Life without wife is not life, but some time wife is a knife to cut your life!!!
   
 15. DULLAH B.

  DULLAH B. JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 674
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Shemejiiii!
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Misemo ya form one au two! Mshafunga shule?
   
 17. beibe nasty

  beibe nasty JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 1,648
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mmmmmmmmh ts painful
   
 18. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ni kweli sio mama yako lakini pingu zinazowaunganisha anakuwa zaidi ya mama yako na baba yako. Ndio maana unaita baba, unaita mama na uonapoona baba na mama yako wanatengana nafikiri unaumia sana sasa inakuwaje kwa mkeo mliyeahidiana kufa na kuzikana ukagundua usaliti huu.

  nafikiri unaweza kufa wewe kwa shinikizo kama sio kuua. so sad.
   
 19. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hahaha @ Asprin hiyo ya mwanzo nilikuwa sijaiona, hii nimeipata kwnye inbox yangu bila shaka ningeiona mwazo nisingepata shock maana mimi nilibaki mdomo wazi.
   
 20. Joseverest

  Joseverest Verified User

  #20
  Oct 30, 2017
  Joined: Sep 25, 2013
  Messages: 36,189
  Likes Received: 41,360
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Daaaah
   
Loading...