Habari jf ,
Kwanza kabisa ifahamike IGA hii ni MKATABA sio makubaliano ya kawaida kama yanavyosemwa ,sababu ni makubaliano ya kimaandishi na yana ulinzi wa kisheria .
Pili huu Mkataba Una Ukomo lakini huo ukomo unategemea HGA -ukisoma vizuri utagundua umefichwa kwenye HGA ,ambayo ndio mikataba tutakayo ingia na DP WORLD .
Tatu IGA iko very technical hivyo HGA inabidi wahusishwe watu wenye uelewa sana sio wale vilaza kule vinginevyo tutauza mali za Nchi .
MAPUNGUFU nliyoyaona kwenye huu mkataba ambayo kina Mwabukusi na wenzake hawayapigii kelele .
1.Hakuna sehemu ambayo imetuweka wazi kwamba baada ya Kusaini IGA tunaweza kataa HGA kama zitakuwa hazieleweki .
2.Mkataba wa IGA inabidi uweke wazi kwamba tukishindwana na HGA au DP world basi na IGA ife hapo wamekataa kabisa .
3.Mkabata ukiusoma vizuri utagundua kuna maeneo unaonyesha kwamba ukisha saini hii IGA basi umebariki Dp World kuweza kufanya kazi regardless ya HGA .
KWA MAANZA RAHISI KUNA IGA NA HGA kwenye huu mkataba----Hapa wanasheria watanielewa ,nadhani kina Mwabukusi na wenzake waupitie upya kuna mapungufu mengi sana lakini yako more TECHNICAL ,mengi yanayopigiwa kelele yana majibu kwenye huo Mkataba .