Kama huku ndiyo kufa basi ni hatari

Kama huku ndiyo kufa basi ni hatari

Ilikuwa Alhamisi ya last week nilikuwa nasikia maumivu ya tumbo sana. Familia yangu wakanikimbiza hospitali maana hali yangu ilikuwa siyo nzuri, ndugu na jamaa walikuwa wanasubiri majibu kutoka kwa docters tu maana nilikuwa na hali mbaya.

Nilifika hospitali kwa bahati mbaya kama maelezo yao walivyonisimulia kuwa nilikufa kabisa wakanifunika na shuka. Sasa kilichonishangaza mimi kipindi nipo kitandani pale mimi nilihisi kuwa nimelala, yaani nimepumzika maana akili yangu bado ilikuwa inafanya kazi kabisa.

Nilikuwa nasikia vilio vya watu na kutambua huyu ni mama yangu, huyu ni fulani, ila kule kuongea au kutikisika na kufungua macho ndiyo nilikuwa siwezi kabisa.

Kwa maelezo yao walisema nilifanya kitu cha masaa matatu maiti yangu iko tu kitandani, walikuwa wanafanya utaratibu wakunipeleka mochari ndiyo nikafufuka tena.

Mpaka sasa hivi bado najiuliza kumbe mtu akifa akili yake bado inafanyaga kazi? Kweli ninaamini wangenipeleka udongoni ningejua na pelekwa udongoni, maana nilikuwa nafahamu na nilikuwa nasikia watu wanavyo lia.

Kama ndiyo kufa ni Mungu tu mwanadamu hawezi, watu wanazikwa huku wakijua kabisa wanapelekwa udongoni ila nguvu ya kukataa ndiyo hawana!
Ungekuwa nchi ya kiislam ungeshazikwa,kule ukifa ni nusu saa tu unazikwa
 
Kufa ni kupoteza fahamu, kuto tambua mazingira yanayokuzinguka, viungo vya mwili, pamoja mishipa yote, kuacha kufanya kazi, siyo kusimama, kuacha kufanya kazi.

Sasa kama ulikua unasikia vilio, sioni kufa kwako, ikiwa viungo vya fahamu vilikua vikifanya kazi.
Umewahi kufa? Katika nadharia ya Kisayansi ndo tunasema hivi ulivyosema ila uhalisia halisi hatujui. Huenda maiti huko kaburini roho zao zinapiga story na zinaona yote ila hazina mlango wa kufikia walio hai. Hakuna binadamu aliye hai anaweza thibitisha hili. Tena angalau wale ambao walishakuwa mahututi sana wanaweza sema, na near death experience ukizisikiliza wapo wanaokiri walijua kila kitu kinachoendelea.
 
Wengi hapa wataona kama utani lakini alichozungumza kiliwahi nitokea kabisa, unasikia lakini huwezi fanya lolote, binafsi nashauri mtu anapozima ghafla kuwepo na subira na mazoezi mengine ya kuuamsha mwili, kwa atleast 6 hours, and then Daktari aje approve mambo mengine, hii kukimbiza kuzika ni mbaya Sana.
 
Guys,Guys omba yasikukute,niliwahi pata ajali mbaya sana aisee nilikuwa katika hali kama hyo,Nasikia kila kitu ila siwezi kufanya chochote Daa...kuna mama mmoja huwa simsahau mpaka leo yaan huyo ndo alikuwa anashindilia kabsa.nanukuu"Jamani huyu tayari tuharakishe tuanze taratibu za mazishi"
 
Shukuru mungu sana.kule mochwari ungepelekwa usingetoka salama.
Wana RUNGU kubwa kwa ajili ya marehemu wabishi.daktari amethibitisha umekufa afu uamkie monchwari unapewa moja la utosi unatulia.
Muulize yule JR atakwambia

Hii kweli mkuu?
 
Uliishiwa nguvu tu na ndugu zako walijaa uoga.
Masaa matatu yote kukizuia nini kukupeleka kwenye friji la mortuary?
"Nilifika hospitali kwa bahati mbaya kama maelezo yao walivyonisimulia kuwa nilikufa kabisa wakanifunika na shuka."

Huenda kadanganya, ila hii dunia ina mambo mengi ambayo ni ya ajabu na hatujui ni nn hawa kimetokea pale kinapotokea na unapomsikiliza mtu unaona kabisa huu ni uongo. Tunasahau kuwa hatujui siri zote za huu ulimwengu. Ukikaa na watu wanaofanya huduma za kusafirisha maiti wanasema kuna maiti huwa zinagoma kusafirishwa mpaka mnashusha watu au mtu fulani.
 
Ungekuwa dini fulani tayari leo hii watu wangekula ubwabwa nyumbani kwenu.
Ile dini hawataki masihara kabisa kwenye issue ya kuzikana
 
Mkuu wewe hukufa ila ulikata moto kwa muda!
Mtu aliyefikia stage ya kufa kabisa then kwa bahati mbaya au nzuri akarudiwa na uhai mara nyingi huwa hawezi tena kuongea anakuwa bubu au taahira kabisa ili asiweze kutoa siri!
Kaka Mshana Jr unaweza kuja kutia neno hapa maana haya mambo wengine tunasikiaga tu
 
Shukuru mungu sana.kule mochwari ungepelekwa usingetoka salama.
Wana RUNGU kubwa kwa ajili ya marehemu wabishi.daktari amethibitisha umekufa afu uamkie monchwari unapewa moja la utosi unatulia.
Muulize yule JR atakwambia
Duh.!
 
Ilikuwa Alhamisi ya last week nilikuwa nasikia maumivu ya tumbo sana. Familia yangu wakanikimbiza hospitali maana hali yangu ilikuwa siyo nzuri, ndugu na jamaa walikuwa wanasubiri majibu kutoka kwa docters tu maana nilikuwa na hali mbaya.

Nilifika hospitali kwa bahati mbaya kama maelezo yao walivyonisimulia kuwa nilikufa kabisa wakanifunika na shuka. Sasa kilichonishangaza mimi kipindi nipo kitandani pale mimi nilihisi kuwa nimelala, yaani nimepumzika maana akili yangu bado ilikuwa inafanya kazi kabisa.

Nilikuwa nasikia vilio vya watu na kutambua huyu ni mama yangu, huyu ni fulani, ila kule kuongea au kutikisika na kufungua macho ndiyo nilikuwa siwezi kabisa.

Kwa maelezo yao walisema nilifanya kitu cha masaa matatu maiti yangu iko tu kitandani, walikuwa wanafanya utaratibu wakunipeleka mochari ndiyo nikafufuka tena.

Mpaka sasa hivi bado najiuliza kumbe mtu akifa akili yake bado inafanyaga kazi? Kweli ninaamini wangenipeleka udongoni ningejua na pelekwa udongoni, maana nilikuwa nafahamu na nilikuwa nasikia watu wanavyo lia.

Kama ndiyo kufa ni Mungu tu mwanadamu hawezi, watu wanazikwa huku wakijua kabisa wanapelekwa udongoni ila nguvu ya kukataa ndiyo hawana!
Acha kuvuta makushabu
 
Back
Top Bottom