Hii cha mtoto, sisi tulikuwa tunachukua tairi la lori au trekta unaingia hapo katikati unajikunja then wenzio wanakusukuma! Siku ingine wanakusukuma wanapoteza muelekeo wanakuacha upambane na hali yako!
View attachment 1101131
Ahahahhaa aiseeeeee umenikumbusha mbali sana.
Umeshawahi kukalia kuti alafu kuti linakaa juu ya kisuguu unawekea na nyasi kidogo sehemu ambazo litapita lile kuti ili kuwe la low friction alafu unaachia kuti(gubi zima lile la mnazi)basi unaseleleka nalo linaenda mpaka chini.huu mchezo huko kusini tumeucheza sana na yulishachana sana suruali engo za matakoni ila tunashkuru hakuna ambae alikosa njugu(pumbuh)
Ungine ni sarakasi kwa wale wanachingwea watakumbuka kwa mzee namadila kuna makana mengi tunaweka tairi kubwa la gari alafu tunaruka sarakasi hapo,siku moja kichwa choye kilizama kwenye makana hatari.
Tulikuwa tunaenda kuogelea kwenye sehemu flani flani hivi huko home sasa ikawa tunakunya humo humo yaaani staili ya kunya ni moja tuu.
Yaani unazama majini alafu unakunyaa ukiwa chini ya maji sasa mavi hayazami yanaelea na kutawanyika flani hivi..sasa kifuatachooo
unatakiwa upige chini kwa chini ukaibukee penginee kwa sababu ukiibuka hapo hapo unayavaa mavi yako yaani yanakua kofia(yapo kichwani) na kipindu pindu tulikuwa tunakiskia kwa jirani tu,rafiki zako wwoteeee tuliokuwa tunaoga nao hakuna hata mmoja aliekufa kwa kipindu pindu Mungu ashukuriwe sanaa
Enzi hizo wadada wakubwa bhana walikuwa wananimaindi sana mpaka ikafkia hatua wananiiba wanajigegedesha kwangu,ila saivi wakiniona wananisalimia tuu.
Waliiii wa sherehe tulikuwa tukitia mifukoni kabisaa unaepa nao huyooooo.
Nimecheza sana rede na mdako al manusra nigeuke shogaa ila washkaji wakanitonya mana nilikuwa najifanya mwana falsafa tokea utotoni,wakiniambia michezo nayocheza ya kike nawaambia hapana hakuna mchezo wa kike wala wa kiumee kwani kunya mchezo wa kike au wa kiume? Basi wanaduwaa ila baadaae nikaona mchezo hauna wanaume kabisa nikaacha falsafa zangu za kifwala.