Kama hivi ndivyo ilivyo muda wowote dr. Ulimboka atatutoka duniani, baba yake aangua kilio. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hivi ndivyo ilivyo muda wowote dr. Ulimboka atatutoka duniani, baba yake aangua kilio.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, Jun 30, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,913
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya
  ya Madaktari, mzee Steven
  Mwaitenda amejikuta akiangua
  kilio kwa uchungu mbele ya
  wanaharakati ambao
  walimtembelea mwanae, Dk.
  Steven Ulimboka kumpa pole
  kufuatia tukio la kutekwa na
  kujeruhiwa vibaya na watu
  wasiojulikana.
  Hali hiyo ilitokea jana jioni katika
  Taasisi ya Tiba ya Mifupa
  Muhimbili (MOI), ambapo
  wanaharakati kutoka taasisi na
  asasi mbalimbali za utetezi wa
  haki za binadamu walifika kwa
  lengo la kumpa pole Dk. Ulimboka
  kufuatia kitendo kilichomfika.
  Mzee Mwaitenda alijikuta
  akibubujikwa na machozi na
  kushindwa kuendelea
  kuzungumza alipokuwa akitoa
  shukrani kwa wanaharakati hao,
  kwa niaba ya mwanaye ambaye
  wanaharakati hao walishindwa
  kumuona wote kutokana na hali
  yake ilivyo sasa.
  “Niseme wazi nimefarijika sana
  kwa ujio wenu kumwona
  mwanangu dhidi ya mambo ya
  kikatili aliyofanyiwa akitetea haki
  za wengine…,” alisema mzee
  Mwaitenda kabla ya kushindwa
  kuendelea na kuangua kilio mbele
  ya wanaharakati.
  Baada ya tukio hilo baadhi ya
  wanaharakati walimshika
  wakishirikiana na wanafamilia ya
  mzee Mwaitenda na kumbebeleza
  kisha kumtoa mbele ya
  mkusanyiko huo wa
  wanaharakati na kumrudisha
  wodini huku wakimfariji.
  Wakizungumza mara baada ya
  tukio hilo wanaharakati
  wameelezea kusikitishwa na
  vitendo vinavyoendelea MOI eneo
  ambalo amelazwa kiongozi huyo
  wa madaktari ambavyo
  vimeendelea kutishia usalama wa
  Dk. Ulimboka.
  Akifafanua zaidi mwakilishi wa
  wanaharakati hao, Markos Albania
  alisema taarifa walizozipata usiku
  wa juzi kuna wagonjwa ‘feki’
  ambao walijitokeza MOI huku
  wakitaka kulazwa wodi ya
  Wagonjwa Mahututi (ICU)
  alipolazwa Dk. Ulimboka lakini
  baadaye waligoma kuingizwa
  wodini.
  “Wapo wagonjwa ambao
  waliletwa na kutaka kupelekwa
  ICU moja kwa moja…kuna watu
  wanakuja usiku wa manane
  wakitaka kumtembelea Dk.
  Ulimboka…matendo
  yanayoendelea kutokea
  ukilinganisha na kauli za Serikali
  zilizotolewa bungeni yanatishia
  usalama na uhai wa mgonjwa,”
  alisema Albania.
  Aidha amesema kitendo cha
  vyombo vya usalama kuendelea
  kumuhoji Dk. Ulimboka akiwa hoi
  hospitalini si vya kiungwana
  kwani tayari muhusika amewataja
  hadi kwa majina watu ambao
  anawashuku lakini hadi sasa
  hakuna aliyechukuliwa hatua
  yoyote.
  Pamoja na hayo wanaharakati
  hao wameitaka Serikali kuunda
  tume huru mchanganyiko na raia
  ambayo itachunguza kiundani
  suala hilo, kwani hawana imani
  na Jeshi la Polisi ambalo limedai
  kuunda timu ambayo
  inachunguza kwa kina suala hilo.
  Dk. Ulimboka ambaye ni kiongozi
  wa madaktari ambao
  wanaendelea na mgomo wan chi
  nzima kuishinikiza Serikali
  kutekeleza madai yao alitekwa
  juzi na watu wasiojulikana na
  kupigwa na kuteswa kikatili kabla
  ya kutelekezwa katika msitu wa
  Mabwepande.
  *Habari hii imeandaliwa na
  kuletwa hapa na Mtandao wa
  Thehabari.com
   
 2. D

  Do santos JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  acheni kulalama na kutafuta huruma za watz,huyo hajafa sisi tumefiwa na ndugu zetu kwa mgomo wao hamkuona kugoma kwao ni kitendo kisicho cha kiungwana? hali ya kuwa wapo wagonjwa mahututi? na tena wanataabika.mbona hamkuwahimiza kuwatibu wagonjwa wanaoteseka.Acheni ahojiwe hata kama anaumwa,ili ajue uchungu wanaopata wale wagonjwa wakati wao wamegoma kuwatibia.Pumbav
   
 3. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,678
  Trophy Points: 280
  Nakupa 100%
   
 4. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  matendo haya ya serikali ya Kikwete yataleta machafuko.
   
 5. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huruma tanzania na simanzi kila kona.
   
 6. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mwenyezi Mungu alikuwa pamoja nawe Dr Ulimboka ucku ule wa tukio, ataendelea kuwa pamoja kupambana ktk kupona kwako, na yupo pamoja na wale wote wapambanaji dhidi ya hao wapinga Haki kwa Watanzania.

  Tupo pamoja Dr Ulimboka, Wanaharakati wote, Madaktari wote, Family ya Dr Ulimboka na Watanzania wote ktk hizi harakati tufanikiwe ktk Tiba ya Dr, na pia kupambana ktk kuleta Ukombozi wa kweli kwa Taifa la Tanzania dhidi ya Udhalimu wa aina yeyote.
   
 7. Miya

  Miya JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 817
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 180
  Kwani hospitali nzima kalazwa Dr.ulimboka peke yake? walizani watamuua kirahisi kaaga kwao huyo hadi awaumbue ndo mkome mmekazana watu wanakufa kwani huwaga hawafi vita ni vita aisee .....serikali imetangaza vita haujui katika kila vita lazima watu wafe...
   
 8. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,548
  Likes Received: 16,521
  Trophy Points: 280
  Msifurahie ya wenzenu,kuna familia yamewakuta haya aliyofanyiwa Dr.Ulimboka wakati wa awamu ya kwanza kwa kisingizio cha uhujumu uchumi,bila hata kufunguliwa mashtaka ,kuteswa na kutupwa tu gerezani.Baada ya miaka yakutumikia kifungo wanaambiwa walikuwa hawana hatia. Hata siye tulio na wagonjwa majumbani bado hatujatoa laana hiyo.Kisasi ni cha mungu.
  Sasa madaktari wamerudi kazini?Je unadhani ni haki kukodisha madaktari wa nje kwa tz.200mil za walipa kodi?Kama wanazo kwa nini wasirekebisha hali za hospitali na kuwalipa hawa watanzania wenzetu vizuri?Kweli ni bora kulipa vizuri mgeni na mwananchi wako kumwacha na njaa?Lazima ziwe ni akili za kichaa.........
   
 9. t

  tocolyitics Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha upuuzi mbona unakuwa fara kama haufikirii. Mwenye kazi ya kuhudumia raia ni hii serikari yenu sikivu inayosikia hata ushauri wa kipuuzi.
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Walipelekwa mabwepande kung'olewa kucha na meno hao waliokufa?
   
 11. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Sisi tumefiwa na vichanga vyetu baada hospitali hapa nchini kukosa vacuum pump ya kuvuta maji machafu ambayo vichanga humeza wakati wa zoezi la mama kujifungua na kuziba njia za hewa. Pampu hiyo huuzwa Shs 5,000/= tu. Posho za kukaa ambazo maafisa waandamizi wa Serikali ya CCM hulipana ya Shs 200,000/= kwa kila kikao, hata kama ni kuhudhuria kikao mlango wa pili toka ofisi zao ingetosha kununua pampu 40 kama hizo na kukoa maisha ya vichanga hizi. Je ni akina mama wangapi wamepoteza vichanga vyao baada ya kubeba mimba miezi 9 kwa kukosekana kifaa hiki?

  Sisi tumefiwa na ndugu zetu kwa kukosekana sindano ya kuingiza maji ya dripu mwilini inayouzwa shs 250/= tu.

  Jana katika tarifa ya habari ya ITV akina wawili waliopata ajali ya pikipiki na kukanyagwa na gari kubwa wametelekezwa katika vitanda vya hospitali ya Bombo Tanga wakingoja kupoteza maisha kwa sababu hospitai hiyo haina kifaa cha kupiga picha za X-ray, madakatari walikuwepo lakini hawakuweza kuwapatia huduma kwa wagonjwa wanalazimka kuwa na fedha za kuhamishiwa katika hospitali binafsi kupiga picha hizo. Gharama ya shangingi moja wanalopanda maafisa waandamizi wa CCM na Serikali yake zingetosha kuzipatia hospitali 3 vifaa vya aina hiyo. Je ni watanzania wangapi hupoteza maisha kila siku kwa kukosekana vifaa vya X-ray, Ultra sound, CT scan n.k katika hospitalia ilihali mashangingi yanannunuliwa kila mwaka na fedha Serikali ya CCM hutenge mabilioni kwa ajili ya kulipana posho za kukaa na safari zisizo na tija?

  Katika madai yao madakatari wamesema wamechoka kuwaona watanzania wenzao wakipoteza maisha kimya kimya kwa kukosekana vifaa muhimu vya matibabu ilihali nchi ikisamehe Dola Bilioni kama kosi. Kuanzia sasa ni vyema idadi ya watanzania wanaopoteza maisha ikaanza kuwekwa wazi na sababu zake,
   
 12. m

  mamajack JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  unahaki ya kuilalamikia serikali na sio madaktali maana wewe mwananchi huna mkataba nao.wewe kama umefiwa lia na sserikali yako na wala sio madaktari maana mkata upo kati yako na serikali kwa kula yako ya ndiyo.lakini mkata wa serikali na daktari ni wa ajira.pole kwa kufiwa na sababu ya serlikali dhaifu.
   
 13. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  huyo dokta ulimboka akipoteza uhai serekali na ccm mtapitia kwenye wakati mgumu ambao hamjawahi pitia tangu kuumbwa kwa tanganyika
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  hoja zako ni kama za watoto wadogo! Ndio maana humepandwa na hasira ukatukana kwaajili ya kukosa cha kuandika.

  Sasa umefiwa na nduguzo kwa hiyo una halalisha wengine wauwawe?
  Jaribu kufikiri kwa kina kama wewe unaweza kufanya kazi isiyo endana na malipo?

  Unatakiwa utumie busara unapo ongea kitu, dr ulimboka alikuwa anatetea hata haki zako za kupata huduma bora.

  Halaf hoja yeyote haimalizwi kwa kutukana ni aibu sana.

  NB: Nothing goes for nothing
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we punguwani nini?sasa ndugu zako wanatuhusu nini sisi?
   
 16. D

  Do santos JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hapo kwenye red ni kichaga au lugha gani dogo,unajifanya unahasira kama kweli jisaidie haja kubwa tuone.
   
 17. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  dos santos umevurugwa kwa kuhemewa ,paka jike wewe
   
 18. r

  reformer JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu kama nyie you deserve to die and burn in hell.
   
 19. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kufa kila mtu atakufa na Dr. Ulimboka si mtu wa kwanza kulazwa Icu sababu iliyofanywa alazwe icu haifanani na sababu iliyofanya hao ndugu zako kufa.Kwahiyo mkimuua ulimboka ndiyo itatuliza machungu yako na wenzio?
   
 20. d

  dguyana JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ahata mimi nikiiumwa leo na nikakosa huduma sitawalaumu Madokta kwani sina Mkataba nao. Mimi najua serikali yangu ndio yenye jukumu la kunihudumia. Kila la kheri Tanzania.
   
Loading...