Kama hivi ndivyo ilivyo muda wowote dr. Ulimboka atatutoka duniani, baba yake aangua kilio.

Msifurahie ya wenzenu,kuna familia yamewakuta haya aliyofanyiwa Dr.Ulimboka wakati wa awamu ya kwanza kwa kisingizio cha uhujumu uchumi,bila hata kufunguliwa mashtaka ,kuteswa na kutupwa tu gerezani.Baada ya miaka yakutumikia kifungo wanaambiwa walikuwa hawana hatia. Hata siye tulio na wagonjwa majumbani bado hatujatoa laana hiyo.Kisasi ni cha mungu.
Sasa madaktari wamerudi kazini?Je unadhani ni haki kukodisha madaktari wa nje kwa tz.200mil za walipa kodi?Kama wanazo kwa nini wasirekebisha hali za hospitali na kuwalipa hawa watanzania wenzetu vizuri?Kweli ni bora kulipa vizuri mgeni na mwananchi wako kumwacha na njaa?Lazima ziwe ni akili za kichaa.........

Thank you!!!
 
gambaaaa!!!!!!! ila mwka huu kitaeleka tu, mambo yote hadharan cjui mtajificha wap!!!!!!!! mungu amjalie apone. na sio wote tulio hapa ikuru tunafurahishwa na hv vitendo vya kinyama.
 
acheni kulalama na kutafuta huruma za watz,huyo hajafa sisi tumefiwa na ndugu zetu kwa mgomo wao hamkuona kugoma kwao ni kitendo kisicho cha kiungwana? hali ya kuwa wapo wagonjwa mahututi? na tena wanataabika.mbona hamkuwahimiza kuwatibu wagonjwa wanaoteseka.Acheni ahojiwe hata kama anaumwa,ili ajue uchungu wanaopata wale wagonjwa wakati wao wamegoma kuwatibia.Pumbav

Usual ****
 
Acha upuuzi mbona unakuwa fara kama haufikirii. Mwenye kazi ya kuhudumia raia ni hii serikari yenu sikivu inayosikia hata ushauri wa kipuuzi.

Acha bana! Wewe unadhani serikali ni dude fulani? serikali ni binadamu kawa wewe! Eti mwenye kazi ya kuhudumia raia ni serikali! Poor mind!
 
Nilitaka kumgongea mtu thanx lakini mamodi bwana,...ah! Rudisheni bwana.
 
acheni kulalama na kutafuta huruma za watz,huyo hajafa sisi tumefiwa na ndugu zetu kwa mgomo wao hamkuona kugoma kwao ni kitendo kisicho cha kiungwana? hali ya kuwa wapo wagonjwa mahututi? na tena wanataabika.mbona hamkuwahimiza kuwatibu wagonjwa wanaoteseka.Acheni ahojiwe hata kama anaumwa,ili ajue uchungu wanaopata wale wagonjwa wakati wao wamegoma kuwatibia.Pumbav

nashangaa kwa nini hawagomi wakati watanzania maskini wakipelekwa pale wanaangaliwa kama uyoga????
 
Siku moja baada ya Serikali kutangaza kutumia hospitali za Jeshi na madaktari wastaafu kunusuru afya za wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini, juhudi zaidi zimechukuliwa na sasa itatumia pia hospitali binafsi.

Hospitali zilizotajwa kukubali kushirikiana na Serikali kutoa huduma za afya kwa watakaohitaji tiba ya haraka na walio katika tiba isiyoweza kusitishwa ni pamoja na TMJ, Regency, Aga Khan, Hindu Mandal, CCBRT na Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Aidha, nguvu zimeongezwa katika hospitali za Mwananyamala, Amana na Temeke za Dar es Salaam kunakodaiwa hakuna mgomo, ili kutotoa rufaa nyingi kwa wagonjwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kunakodaiwa kuwa na mgomo.
 
hapo kwenye red ni kichaga au lugha gani dogo,unajifanya unahasira kama kweli jisaidie haja kubwa tuone.

Kauli zako hazitofautiani sana na mabosi zako
1. Wasichana wanaopata mimba wakiwa mashuleni ni viherehere vyao
2. Wanaoua albino nao wauwawe
3. Liwalo na liwe
4. Kama upinzani wanasikia uchungu na hii nchi waende leba wakazae
5. Kudadadeki
 
hoja zako ni kama za watoto wadogo! Ndio maana humepandwa na hasira ukatukana kwaajili ya kukosa cha kuandika.

Sasa umefiwa na nduguzo kwa hiyo una halalisha wengine wauwawe?
Jaribu kufikiri kwa kina kama wewe unaweza kufanya kazi isiyo endana na malipo?

Unatakiwa utumie busara unapo ongea kitu, dr ulimboka alikuwa anatetea hata haki zako za kupata huduma bora.

Halaf hoja yeyote haimalizwi kwa kutukana ni aibu sana.

NB: Nothing goes for nothing

Wengine wametumwa mkuu.
 
siku moja baada ya serikali kutangaza kutumia hospitali za jeshi na madaktari wastaafu kunusuru afya za wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini, juhudi zaidi zimechukuliwa na sasa itatumia pia hospitali binafsi.

Hospitali zilizotajwa kukubali kushirikiana na serikali kutoa huduma za afya kwa watakaohitaji tiba ya haraka na walio katika tiba isiyoweza kusitishwa ni pamoja na tmj, regency, aga khan, hindu mandal, ccbrt na hospitali ya jeshi lugalo.

Aidha, nguvu zimeongezwa katika hospitali za mwananyamala, amana na temeke za dar es salaam kunakodaiwa hakuna mgomo, ili kutotoa rufaa nyingi kwa wagonjwa kwenda hospitali ya taifa muhimbili kunakodaiwa kuwa na mgomo.

ndiyo suluhu?
 
Walipelekwa mabwepande kung'olewa kucha na meno hao waliokufa?

kwa uelewa wngu mdogo kupitia filamu mpaka kung'olewa kucha na meno hiyo ni 'torturing'. bila shaka Dk. alikua subjected to coercive interrogation,may be he was forced to disclose who was the mistermind wa mgomo or nani anawapa back up mpaka kujiamini that much.

'Mkweli yupamoja na mungu'
 
acheni kulalama na kutafuta huruma za watz,huyo hajafa sisi tumefiwa na ndugu zetu kwa mgomo wao hamkuona kugoma kwao ni kitendo kisicho cha kiungwana? hali ya kuwa wapo wagonjwa mahututi? na tena wanataabika.mbona hamkuwahimiza kuwatibu wagonjwa wanaoteseka.Acheni ahojiwe hata kama anaumwa,ili ajue uchungu wanaopata wale wagonjwa wakati wao wamegoma kuwatibia.Pumbav



Hata wagonjwa 1000 wafe,si ndiyo faida ya serikali yako legelege na DHAFU.
 
Damu na mateso ya Dr.Ulimboka, haitapotea bure. Mkono wa Mungu wenye haki unamakusudi katika kunusuru maisha ya Dr.Ulimboka kimiujiza. Wazalendo wa kweli tutamuenzi Dr.Ulimboka kwa namna mbalimbali katika historia na harakati zake zote zake kutetea afya zetu wanyonge. Pole na hongera baba mzazi kwa kumlea vizuri Dr.Uli. Poleni ndugu na jamaa, poleni madaktari wote wenye mtazamo chanya katika jambo hili, poleni wanaharakati na watanzania Wazalendo wote.
 
BABA wa Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Madaktari, mzee Steven
Mwaitenda amejikuta akiangua
kilio kwa uchungu mbele ya
wanaharakati ambao
walimtembelea mwanae, Dk.
Steven Ulimboka kumpa pole
kufuatia tukio la kutekwa na
kujeruhiwa vibaya na watu
wasiojulikana.
Hali hiyo ilitokea jana jioni katika
Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili (MOI), ambapo
wanaharakati kutoka taasisi na
asasi mbalimbali za utetezi wa
haki za binadamu walifika kwa
lengo la kumpa pole Dk. Ulimboka
kufuatia kitendo kilichomfika.
Mzee Mwaitenda alijikuta
akibubujikwa na machozi na
kushindwa kuendelea
kuzungumza alipokuwa akitoa
shukrani kwa wanaharakati hao,
kwa niaba ya mwanaye ambaye
wanaharakati hao walishindwa
kumuona wote kutokana na hali
yake ilivyo sasa.
"Niseme wazi nimefarijika sana
kwa ujio wenu kumwona
mwanangu dhidi ya mambo ya
kikatili aliyofanyiwa akitetea haki
za wengine…," alisema mzee
Mwaitenda kabla ya kushindwa
kuendelea na kuangua kilio mbele
ya wanaharakati.
Baada ya tukio hilo baadhi ya
wanaharakati walimshika
wakishirikiana na wanafamilia ya
mzee Mwaitenda na kumbebeleza
kisha kumtoa mbele ya
mkusanyiko huo wa
wanaharakati na kumrudisha
wodini huku wakimfariji.
Wakizungumza mara baada ya
tukio hilo wanaharakati
wameelezea kusikitishwa na
vitendo vinavyoendelea MOI eneo
ambalo amelazwa kiongozi huyo
wa madaktari ambavyo
vimeendelea kutishia usalama wa
Dk. Ulimboka.
Akifafanua zaidi mwakilishi wa
wanaharakati hao, Markos Albania
alisema taarifa walizozipata usiku
wa juzi kuna wagonjwa ‘feki'
ambao walijitokeza MOI huku
wakitaka kulazwa wodi ya
Wagonjwa Mahututi (ICU)

alipolazwa Dk. Ulimboka lakini
baadaye waligoma kuingizwa
wodini.
"Wapo wagonjwa ambao
waliletwa na kutaka kupelekwa
ICU moja kwa moja…kuna watu
wanakuja usiku wa manane
wakitaka kumtembelea Dk.
Ulimboka…matendo
yanayoendelea kutokea
ukilinganisha na kauli za Serikali
zilizotolewa bungeni yanatishia
usalama na uhai wa mgonjwa,"
alisema Albania.
Aidha amesema kitendo cha
vyombo vya usalama kuendelea
kumuhoji Dk. Ulimboka akiwa hoi
hospitalini si vya kiungwana
kwani tayari muhusika amewataja
hadi kwa majina watu ambao
anawashuku lakini hadi sasa
hakuna aliyechukuliwa hatua
yoyote.
Pamoja na hayo wanaharakati
hao wameitaka Serikali kuunda
tume huru mchanganyiko na raia
ambayo itachunguza kiundani
suala hilo, kwani hawana imani
na Jeshi la Polisi ambalo limedai
kuunda timu ambayo
inachunguza kwa kina suala hilo.
Dk. Ulimboka ambaye ni kiongozi
wa madaktari ambao
wanaendelea na mgomo wan chi
nzima kuishinikiza Serikali
kutekeleza madai yao alitekwa
juzi na watu wasiojulikana na
kupigwa na kuteswa kikatili kabla
ya kutelekezwa katika msitu wa
Mabwepande.
*Habari hii imeandaliwa na
kuletwa hapa na Mtandao wa
Thehabari.com

aisee huyu doctor yuko hatarini sana maana yeye ndio main witness, kawaona wabaya wake na anaweza kuwatambua na kusema kila kitu walichofanya kwa hiyo panga pangua watataka kummaliza.
 
Kwa sababu ya ulegele wa Mh Jakaya Mrisho Kikwete na ukurutu wa ubongo wake wa uongozi watakufa maelfu kwa maelfu na ndipo watakapojua kuwa Dr Ulimboka ni mkombozi wa kweli
 
Acha bana! Wewe unadhani serikali ni dude fulani? serikali ni binadamu kawa wewe! Eti mwenye kazi ya kuhudumia raia ni serikali! Poor mind!
A government consists of the legislators, administrators, and arbitrators in the administrative bureaucracy who control a state at a given time, and the system by which they are organized. Government is the means by which state policy is enforced, as well as the mechanism for determining the policy of the state.

Naomba niambie binadamu kama mimi (mmachinga) nakuwaje sehemu ya serikali
 
acheni kulalama na kutafuta huruma za watz,huyo hajafa sisi tumefiwa na ndugu zetu kwa mgomo wao hamkuona kugoma kwao ni kitendo kisicho cha kiungwana? hali ya kuwa wapo wagonjwa mahututi? na tena wanataabika.mbona hamkuwahimiza kuwatibu wagonjwa wanaoteseka.Acheni ahojiwe hata kama anaumwa,ili ajue uchungu wanaopata wale wagonjwa wakati wao wamegoma kuwatibia.Pumbav

Mkataba wa wew Mtanzania kutibiwa ni kati yako na serikali, mkataba wa kutibu ni kati ya resikali na Madaktari. Wewe ukipoteza ndugu lalamikia serikali sio madaktari. Kama una elimu japo kiduchu ya sheria utaelewa juu ya hili......LAW OF CONTRACT
 
Back
Top Bottom