Kama Hayati Magufuli angekuwa hai, Zitto Kabwe angetuelezea vizuri deni la trilioni 91 limefanya nini Tanzania.

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
KAMA HAYATI MAGUFULI ANGEKUWA HAI,ZITO KABWE ANGETUELEZEA VIZURI DENI LA TRILIONI 91 LIMEFANYA NINI TANZANIA.

Leo 13:15hrs 11/12/2022

Mara ya mwisho kusikia habari ya deni la Taifa ilikuwa kwenye bunge la budget mwaka huu nilipomsikia Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.Dkt. Mwigulu Nchemba alisema hadi Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 69.44 ikilinganishwa na shilingi trilioni 60.72 kipindi kama hicho mwaka 2021."BAJETI 2022/23 :DENI LA TAIFA LIMEPANDA KWA ONGEZEKO LA ASILIMIA 14 na VIDEO-Deni la taifa lafikia Sh69.44 trilioni

Nafahamu deni la Serikali kwa uwiano wa Pato la Taifa ni asilimia 31 ambapo ukomo wa kidunia ni asilimia 55 lakini sijui kati ya asilimia 31 na asilimia 55 kwa sasa Tanzania ipo asilimia ngapi!? Mwaka 2015 akiba (reserve) zilikuwa dola za Marekani bilioni 4.3 wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani, lakini wakati Hayati Rais Magufuli alipofariki na Serikali ya Awamu ya tano wakati inaondoka madarakani akiba ilikuwa Dola za Marekani bilioni 5.03. napenda kufahamu kwa sasa Serikali ina akiba kiasi gani,nilizoea kupata hizi data kutoka kwa Zitto Kabwe ila hivi sasa sizipati,sijui Mh Zitto Kabwe yuko wapi siku hizi,nafurahi Serikali haijawahi kukopa kwa ajili ya kulipa mishahara ama kuweka mafuta kwenye magari ya umma bali ni kwa ajili ya kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo nchini, Nafahamu ipo orodha ya karibu miradi 1,000 ambayo imejengwa kwa kutumia fedha hizo ambayo isingeweza kufanyika katika kipindi hicho kama Serikali isingekopa.Tusifanye tathimini kama tumebambikwa tufanye tathimini ya deni huku tukifanya tathimini ya miradi ambayo imefanywa kutokana na deni hilo,

Ningefurahi kama Zitto Kabwe angetuelezwa wakati deni la Taifa likiwa kiwango cha Sh10 trilioni.Halafu tuanze kuangalia katika mwaka 1995 deni lilikuwaje halafu tuangalie pia na miradi ambayo ililetwa na fedha zilizokopwa,pia ni kipi kilitakiwa kifanyike wakati deni linalotajwa lilikuwa dogo, nakumbuka wakati huo hakukuwa na mikoa ambayo iliunganishwa na barabara za lami jambo ambalo liliwafanya watu kusafiri kwa muda mrefu baada ya Analysis (tathimini) kufanyika je tuchukue makusanyo ya fedha tujenge barabara zetu? Tufungue uchumi na tukishafungua uchumi utuletee fedha.…Je tuendelee na hali kama hii halafu na deni letu liwe dogo au tuchukue fedha tutengeneze miundombinu tufungue nchi yetu halafu miundombinu hiyo ituletee fedha tulipe deni!? Hivi leo kila eneo lina umeme wakati awali eneo kubwa lilikuwa giza na hali ilikuwa hivyo hivyo katika sekta nyingine ikiwemo ya afya, ipo orodha ya karibu miradi 1,000 ambayo imejengwa kwa kutumia fedha hizo ambayo isingeweza kufanyika katika kipindi hicho kama Serikali isingekopa.

Nitafurahi kama "role model" Mh Zitto Kabwe angejitokeza atuelezee kwa takwimu kuhusu deni la taifa la trillioni 91 ninalolisikia uko mitandaoni kwenye webu saiti na mitandao ya kijamii.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Akimaliza kulamba asali atakujibu tu
 
Sasa nae ni mnufaika binafsi wa hiyo mikopo, why apige kelele.
 
Back
Top Bottom