linguistics
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 4,701
- 4,325
Agiza unachotaka, nasemaa agiza unachotaka mkuu ntalipa ..Mkuu ulitarajia hao wazungu watalipa chochote? nilipoona akina Kabudi wamekaa na hao wazungu miezi miwili mjadala ulikuwa ni deni $190b, wakatoka bila maelezo ya hilo deni la 190b imekuwaje, wakaiashia kusema sijui $300m goodwill ndio nikajua hakuna mzungu mjinga. Kibaya zaidi hata hawa viongozi wetu hawakuthubutu kuweka hiyo mikataba wazi bungeni. Hapo ndio nilijua hakuna lolote zaidi ya kulishana upepo wa uzalendo uchwara.
Nilichoka nilivyomsikia Prof. Kabudi akitoa ufafanuzi wa marekebisho ya mikataba ya madini, sasa kama prof anatoa ufafanuzi wa jambo na wala hajaeleweka hata na wasomi hapo huoni ni utata mtupu? Ni hivi hakuna chochote tunaowadai hao wazungu bali wabaya wetu ni viongozi wetu walioingia hiyi mikataba ambao wanaitwa makaburi yasiyofukuliwa na kinachowalinda ni kinga yao ya chama twawala. Kumbuka Magu alisema Chenge, Yona, Karamagi and the likes wakamatwe, lakini hawajaguswa mpaka leo. Hapo utasema kuna unayemdai wakati hata hawa tunaowamudu hatujawachukulia hatua?
Acacia tuliambiwa hawajasaliwa hapa nchini wala hawatambuliki, lakini mpaka leo wapo na wanaendelea na shughuli zao. Sana saba tunaona watz wakipoteza ajira zao. Mkuu ukiona hata bei ya sukari, mafuta ya kula yametushinda na sasa mafuta ya taa hamna kwenye petrol station, ndio tutawaweza hao wazungu. Sisi tungojee uchaguzi wa 2020 watu washinde kwa kishindo chini ya uchaguzi wa kikatili na sio kumdai mzungu au kumzuia kuchimba madini.