Kama Chalamila atamwaga utitiri wa Askari siku ya Maandamano ya CHADEMA

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Ikiwa Chalamila atafanya hivyo, tafsiri itakuwa hivi:-

1. Serikali haina nia njema kuelekea chaguzi zinazokuja huko mbeleni kwani kama Serikali ingekuwa na nia njema, badala ya kutumia nguvu nyingi za Askari kuzuia Maandamano, wangetumia nguvu hizo kufanya mazungumzo na CHADEMA.

2. Itaonesha wazi kwamba, Tanzania hakuna tena Demokrasia.

3. Dunia itakuwa upande wa CHADEMA, kwani CHADEMA hawana Jeshi lakini Serikali inatumia Jeshi.

4. Mama atakuwa ameingizwa kwenye mtego ambapo kijinasua kwake ni kwa fedheha.
 
Yaani mmeshindwa kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima mnakuja kujificha kwenye maandamano haramu ya panyarodi 🐒

Kama raia mwema na huru, natoa wito kwa majeshi ya ulinzi na usalama, bila hurumaaaaa na bila kumuonea mtu haya ashukhulikiwe vilivyo kwa kuzurura na kuchafua mazingira ambayo mtakua mnayafanyia usafi tar23 na 24..

Haiwezekani na wala sio ustaarabu yaani nyie msafishe mazingira halafu panyarodi haramu waje wachafue mazingira na kusumbua raia wanaofanya biashara na shughuli zao za kujipatia kipato halali 🐒
 
3.Dunia itakuwa upande wa CHADEMA, kwani CHADEMA hawana Jeshi lakini Serikali inatumia Jeshi.

4. Mama atakuwa ameingizwa kwenye mtego ambapo kijinasua kwake ni kwa fedheha.
Samia ni IOWA IQ hawezi ku reason that much deep!
 
Chadema na nyie mnazingua. Mpo ni kama mnabip. Hamjasimama imara kumtafuta kura kama mlivyokua enzi za 2009 na 2014. Yaan mpompo tu Ili mradi mpo.

Mambo mengi yanatokea ya hivyo mmekaa kimya mara ngojera za maridhiano. Hamkujua kama maridhiano ni kiini macho? Yaan inteligensia yenu umelala usingiz wa pono kwelikweli. Mnaingizwa kwenye mitego kidogo tu mnaingia. Ubinafsi ndio basi. Mie ndio mie.

Simameni imara, acheni ubinafsi, jengeni chama vizuri Kwa hoja. Wananchi tuliowengi CCM ya aina hii tumechoka, Bora CCM Ile ingine ya Mwendazake angalau watu walikua wanazoea uwajibikaji, hamna pesa ya Bure. Hata mwendokasi ya treni tungekua tumeshaanza kupanda na umeme wa bwawa ungekua tayari. Ila hii ya Sasa ngojera tuu mara maji yamechepuka braaa braaa tu.

Wananchi tunaona ni Bora kutokua na chama, kampuni iende tuuu ijuavyo maana hamna Cha maana. Epukeni mitego modogomidogo, inawatia doa kisiasa. Imarisheni inteligensia yenu. Acheni kutumika.
 
Yaani mmeshindwa kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima mnakuja kujificha kwenye maandamano haramu ya panyarodi 🐒

Kama raia mwema na huru, natoa wito kwa majeshi ya ulinzi na usalama, bila hurumaaaaa na bila kumuonea mtu haya ashukhulikiwe vilivyo kwa kuzurura na kuchafua mazingira ambayo mtakua mnayafanyia usafi tar23 na 24..

Haiwezekani na wala sio ustaarabu yaani nyie msafishe mazingira halafu panyarodi haramu waje wachafue mazingira na kusumbua raia wanaofanya biashara na shughuli zao za kujipatia kipato halali 🐒
Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo? Nini maana ya demokrasia kwa tafsiri unayoijua wewe? Unafikiri ni kwa nini wanataka kuandamana? Chanzo cha mawazo ya kuanza maandamano ni nini?
 
unadhani kwa nini vyombo vya ulinzi na usalamaTZ wameamua kufanya usafi tar 23 na 24 ? Chanzo cha kufanya usafi wa mazingira ni nini 🐒

Demokrasia maana yake wao wafanye yao na wengine wafanye yao kwa uhuru kulingana na mipango yao.

sasa sio hawa wanafanya usafi panyarodi haramu wanakuja kuchafua huku wainaomba "no fiya no heti" au "pipozi pawa" huku wanapora na kubugia ndizi kwenye magenge ya watu na maduka ya watu wanaojitaftia kwa bidii 🐒
 
Ikiwa Chalamila atafanya hivyo, tafsiri itakuwa hivi:-

1. Serikali haina nia njema kuelekea chaguzi zinazokuja huko mbeleni kwani kama Serikali ingekuwa na nia njema, badala ya kutumia nguvu nyingi za Askari kuzuia Maandamano, wangetumia nguvu hizo kufanya mazungumzo na CHADEMA.

2. Itaonesha wazi kwamba, Tanzania hakuna tena Demokrasia.

3. Dunia itakuwa upande wa CHADEMA, kwani CHADEMA hawana Jeshi lakini Serikali inatumia Jeshi.

4. Mama atakuwa ameingizwa kwenye mtego ambapo kijinasua kwake ni kwa fedheha.
Mkuu usiwaamsheee.....
 
Yaani kitendo cha Chalamila kuwaamlisha Wanajeshi wetu kufanya Usafi tayari ni dharau kubwa kwa Jeshi ... nafikiri wanajeshi hawatalipokea vizuri hili. I am looking forward to seeing that happening ......!!
 
kwani ujifunzi au kada mtiifu
mfumo wa Jeshi TZ ni mgumu na usiowezekana kuingilika na kuanzisha mapinduzi 🐒o

ni Jeshi la kitofauti mno na nchi karibu zote duniani, hayupo mjeda wa renki yeyote anaeweza kukomandi au kushawishi ata kambi mbili tu ziungane nae na wanasiasa wachache kufanya mapinduzi, atakua kafumuliwa ubongo kabla hata hajatoka kambini 🐒
 
Back
Top Bottom