Kama CCM siyo adui, mchawi wetu ni nani?

Hata hawajielewi

😁😁

IMG_20211024_211719_063.jpg
 
Basi ulikuwa mdogo wakati Wangwe yanamfika pale barabarani mwaka ule

Majukumu ya wote yanafahamika. Wa Mahakamani, polisi hata yako JF.

Uzuri tunawajua. Pelekeni salamu. Nyie siyo CCM wala nini. Taasisi yenu hiyo mliyojifungua tokea awamu ya tano ni batili.

Habari ndiyo hiyo ukipenda peleka salamu kwani list yenu iliyo kubwa inafahamika.
 
Kumbe wewe bado una maziwa kinywani mwako
 
Mchawi ni Katiba tulionayo, Katiba tulionayo inaluhusu mambo mengi ya ovyo kufanyika. Haiwawajibishi viongozi/watawala
 
Mchawi ni Katiba tulionayo, Katiba tulionayo inaluhusu mambo mengi ya ovyo kufanyika. Haiwawajibishi viongozi/watawala

Mchawi si katiba tuliyo nayo, bali anayezuia mchakato wa katiba bora kuendelea. Huyo ndiye mwenye yote zikiwamo hizi kesi na hukumu za kubumba pale law school:

IMG_20210911_000004_180.jpg

Kwenye picha hiyo naye yumo. Majukumu yake aliyojipa ni pamoja na kutupoteza maboya. Kutuonyesha adui wengine wasiohusika ili tusihangaike naye.

Kama paka, anayo kengele shingoni sasa.

Ukimwona usiku umpitie mbali.
 
Kama taifa mpaka Sasa hatuja mfaham adui wetu licha ya kwamba yupo na ana nguvu Sana maana yupo katika sehemu nyeti ambazo ni untouchable wao ndo huamua kila jambo (deep state)

Bujibuji
 
Kama taifa mpaka Sasa hatuja mfaham adui wetu licha ya kwamba yupo na ana nguvu Sana maana yupo katika sehemu nyeti ambazo ni untouchable wao ndo huamua kila jambo (deep state)

Bujibuji

Nchi inapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa katiba. Kwamba tuna untouchables? Hapa ndipo pa kuanzia.

Huyu adui ambaye ni untouchable ambaye huamua kila jambo (deep state) asiyejulikana hayupo kwenye katiba.

Huyu ndiyo parallel power anayeongelewa na pole pole. Anayebambika kesi na hukumu.

Anateka, kujeruhiwa, kuuwa na kutesa.

Bila shaka SABAYA alikuwa mmoja wao na wengine wametajwa kuwa na Lijenje.

Huyu ndiye aliye wa kumulika vinginevyo hakuna kutoboa.
 
Jamii ya watanzania kuanzia kizazi hiki na kijacho vinapaswa kufutika au kuishi kwenye historia fulani mbaya kwa wote au zaidi ya nusu ya population yoote....Hapa watu watajifunza nini maana ya kuwa mtanzania na majukumu yako ni yapi kama mtanzania....

Zaidi ya 80% ya watanzania ni watu wa hovyo waliolelewa na kukuzwa vibaya...
 
Mkuu upo sahihi kabisa hawa untouchable (deep state) ndo huamua nani awe kiongozi na nani asiwe je,kama kiongozi kawekwa na tabaka hili usitegemee atafanya mambo nje na matakwa yao.

Na nani atavaa viatu vya kudeal na tabaka hili ili hali ndo wameshika mpini wa kisu?
 
Nimekuelewa vizuri sana "mshika panga wa kijapan"niliwahi kuongea na Mzee mmoja kuna jambo aliniambia mpaka Sasa nimeamini ni kweli alisema hivi"ili Tanzania iwe na ukombozi wa kweli lazima kizazi hiki kiishe kizazi kitakacho fuata ndo kitakuwa na akili za ukombozi"
 
Hizi ni aina ya semi za wachawi wetu lengo liko wazi:

1. Zaidi ya 80% ya watanzania ni watu wa hovyo waliolelewa na kukuzwa vibaya...
2. Jamii ya watanzania kuanzia kizazi hiki na kijacho vinapaswa kufutika au kuishi kwenye historia fulani mbaya kwa wote au zaidi ya nusu ya population yoote....

Bwana samurai, vipi umewasikia wakisema hivyo au wewe ni mmoja wao?
 
Mkuu upo sahihi kabisa hawa untouchable (deep state) ndo huamua nani awe kiongozi na nani asiwe je,kama kiongozi kawekwa na tabaka hili usitegemee atafanya mambo nje na matakwa yao.

Na nani atavaa viatu vya kudeal na tabaka hili ili hali ndo wameshika mpini wa kisu?

Mkuu ni hatua njema kwanza kujua mzizi wa fitina ni upi.

Hatua inayofuata ni kuitumia katiba iliyopo kuwakataa. Wana uhalali gani katika katiba ipi hawa kuendelea na ufedhuli wao?

Hawapo popote kwenye katiba watu hawa kuwa wamepewa mamlaka ya kutesa, kuuwa, kupoteza, kubambika kesi au kubambika hukumu.

Kwamba?

"Na nani atavaa viatu vya kudeal na tabaka hili ili hali ndo wameshika mpini wa kisu?"

Hawa tunawamudu.

Kwa kuanzia kama paka wana kengele zao mashingoni mwao.

Kwa vitendo, maneno na hata mabandiko yao hawapaswi kututoa kwenye reli.
 
Nimekuelewa vizuri sana "mshika panga wa kijapan"niliwahi kuongea na Mzee mmoja kuna jambo aliniambia mpaka Sasa nimeamini ni kweli alisema hivi"ili Tanzania iwe na ukombozi wa kweli lazima kizazi hiki kiishe kizazi kitakacho fuata ndo kitakuwa na akili za ukombozi"

Kwamba?

"ili Tanzania iwe na ukombozi wa kweli lazima kizazi hiki kiishe kizazi kitakacho fuata ndo kitakuwa na akili za ukombozi"

Ni kauli ya kinyonge sana wachawi wetu wangependelea mno tuikumbatie 😁😁.

Hiiiiii bagosha!

Si mbaya wakajua huko tumetoka haturudi tena Misri.
 
Kataa 2 ILA UKISHAKUA CCM AKILI INAHAMA ..Mimi nilikua uko na nina uzoefu...nifuate nikuambie namna ya kujitoa .CCM ndio adui wa watanzania .Acheni kua na imani potofu wakuu sitegemei hilo

1st Katiba mpya...kwani kuna tatizo!?? Why Not
 
5E0F6D64-554F-4CC3-994F-964A5AA022DB.jpeg

Tufike mahali tuwe tayari hata kumfunga paka kengele.

Tanzania ni nchi nzuri sana yenye kila kitu watu, madini, ardhi, mafuta, gesi, mito, maziwa hadi bahari.

Mvua za uhakika na urithi mkubwa wote bure toka kwa Mola. Iweje tufikie kufarakana kwa sababu za kisiasa?

Kwamba ni CCM, Chadema, ACT, NCCR au CUF? Aah wapi! Mbona kote ni manung'uniko tu? Ni Pole pole, Vicky Kamata au Bashiru?

Watoto mezani hawaachi kushtakiana mbele za mama zao. Huyu kanifanya hiki, huyu kanifanya vile. Mambo ya kawaida.

"Wajibu wa mama mwema ni kuwaweka wanawe pamoja na maisha ya furaha yakaendelea." -- Askofu Bagonza.

"Yupo mbaya wetu mahala anaye tugombanisha. Siku tukimpata zitakuwa ama zetu ama zake." -- Jabali la Muziki.

View attachment 1985419

Kwenye angle pale anaonekana mtu mwingine nyuma ya usukani. Pole pole anamwita "parallel power." Hao wanalazimisha rais kuwajibika kwao.

Wana ujasiri wa kudai, rais ni taasisi. Taasisi hii imetajwa wapi katiba? Ina kampeni vipi? Wajumbe wake wanapatikana je? Wajumbe wao leo ni kina nani? Au ndiyo hawa wasiojulikana, tukapate kujua waliko kina Moses Lijenje?

Inasemekana wajumbe wake hao wako kila mahali na katika kila idara wanayoita nyeti. Si mahakamani, polisi hadi JF. Kina Sabaya ni baadhi yao. Wameigeuza nchi kuwa yenye huzuni na vilio badala ya kuwa yenye furaha na bashasha.

Hawa ndiyo wenye kukaanga mbuyu na kutuachia wenye meno kutafuna.

Hawa si wa kuwaacha. Hawa ndiyo walio wabaya wetu. Katiba mpya ndiyo dawa yao.

Maudhui ya uzi huu kwa sehemu kubwa yangali yanaishi:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa
 
Back
Top Bottom