Kama boss wako ni mwanamke, hii inakuhusu

Kama boss wako ni mwanamke, hii inakuhusu

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,402
Reaction score
1,618
Kama wewe ni mwanaume na unafanya kazi katika ofisi ambayo unatakiwa kuripoti kwa boss mwanamke nisikilize mimi MCHUNGUZI HURU :-

1. Kila akifika kazini asubuhi hata kama hajapendeza msifie, mwambie boss nimekukubali yaani mambo yako ni kama mcharo vile yaani unajua kunyuka balaa.

2. Hata kama kila siku unaona anazidi kuzeeka, mwambie boss unakula nini mbona kila siku naona unazidi kuwa kijana tu. Sijui ndio pesa zimekukubali au ndio nature ya mwili wako.

3. Akija na style mpya ya nywele, mwambie boss yaani wewe kila style ya nywele inakukubali

4. Kila anachokifanya we msifie tu hata kama ni ujinga

MATOKEO YAKE;
1. Kila safari ya kikazi lazima atakupendekeza uende nae
2. Mshahara wako atakuwa anapendekeza uongezewe
Kumbuka, hata ufanye kazi kwa bidii kiasi gani boss wako akisema hufai na akatoa hata sababu za uongo inakula kwako. Boss hanuniwi vijana

NB: Kujipendekeza kupita kiasi ni hatari kwa afya yako

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Lakini pia unatakiwa kuwa makini maana misifa mingi ukitoa utaaribu..Msome nguo gani anapenda kufaa,gari gani anapenda kutumia zaidi..sasa kama siku hiyo akija kivingine basi utamwambia...Bosi ok but unge ingekuwa safi zaidi...hapo mbona wewe ni mshindi.
 
I mean kama bosi wangu ni mdada???? Ataniona lesbo au?
 
Aiseeeeh! Mkuu wa department ni mwanamke, mkuu wa unit ni mwanamke pia.
Ila hiyo mbinu haiaaply , huo mzuka wa hivyo haupo.
 
Duu,mie huo mtihani nimepata zero wakumsifia mtu kama hajapendeza,ntafanya kazi kwa bidii ntazidi kujiendeleza kikazi
lakini kumsifia kama hajapendeza ASAHAU.....
 
kama mimi ndio boss huyo mtu sitakuwa na mda nae kabisa,ni wa kumuangalia tu kwza...fanya kazi kwa bidii bila neno,lazima utaonekana tu
 
Ngugu Associate mama yangu ndo boss wangu na pale ofisini kuna wanaume mashababi...ole wake mtu nisikie anamsifia bi mkubwa ana mguu wa bia wallah nitamtoa hiyo ndude nimtupie paka!
 
Fanya kazi ndugu utaonekana tu...hizo sifa za marehemu hazina nafasi..
 
Hakuongezee mshahara kama kuna scheme na umefika kwenye bar inakuaje hapo?halafu haya maisha ya kujipendekeza pendekeza ndio kila siku nawahasa vijana muepukane nayo maana ndio mtakuja kujikuta mnaongea na umbeya we piga kazi tu na kazi yako itaonekana.....sasa ukirobby robby kwa kumwaga sifa then ukapewa safari ndio nini?
 
Back
Top Bottom