Kali za mwaka t.b.c

jitu la kale

Member
Dec 29, 2010
77
18
Hii ya akina Kanumba jamani nimeipenda walipofanya ziara Congo DRC na Rwanda,wamepokelewa kama wafalme,kweli nabii akubariki kwao.
 
Tatizo la hawa mabwana wakishakapta kaumaarufu kidogo...wanavimba vichwa na kusahau walikotoka,ndo maana watu wengi wanashindwa kuwapa heko hata pale wanapofanya vyema...tokea nikiwa mtoto till sasa katuni ya Tom na Jerry ni maarufu sana na sikupata kushuhudia majigambo na beef za kijinga jinga km ilivyo kwa kina 'The Great'!
 
Ni bora kuangalia muvi za kinaijeria ambako ndiko wanakokopi kuliko kuangalia zao?
 
Wengi wetu wa JF tunaona kukubali kwamba tunaangalia muvie za kina Kanumba tutachekwa, ila ukweli jamaa wanauza sana kitaani. Ukuitaka kujua nenda kwenye vibanda vya huku kwetu mtaani vya kukodisha movie, ni full Kanumba, Ray et al.

Vile vile ukisikia stori za wamama ambao ndio wanunuaji wa hizi movie wanawakubali jamaa kinoma noma.

Kwa hiyo jamaa wataendelea kuuza kwa sababu wanajua wateja wao wanahitaji nini.

NOTE: waJF style zao kukopi kwenye computa kwa hiyo sio wazuri kwa soko la jamaa hawa wa Bongo Movie.
 
Noma yao kina Kanumba na Ray ni kuachia movie kila wiki! Ubora utapatikana wapi?
 
Wengi wetu wa JF tunaona kukubali kwamba tunaangalia muvie za kina Kanumba tutachekwa, ila ukweli jamaa wanauza sana kitaani. Ukuitaka kujua nenda kwenye vibanda vya huku kwetu mtaani vya kukodisha movie, ni full Kanumba, Ray et al.

Vile vile ukisikia stori za wamama ambao ndio wanunuaji wa hizi movie wanawakubali jamaa kinoma noma.

Kwa hiyo jamaa wataendelea kuuza kwa sababu wanajua wateja wao wanahitaji nini.

NOTE: waJF style zao kukopi kwenye computa kwa hiyo sio wazuri kwa soko la jamaa hawa wa Bongo Movie.

Ni upuuzi wa ari ya juu sana mimi kuanagalia movie ambayo nikianza tu kuiona najua mwisho wake.... nahitaji muvi ya kuumiza kichwa.

Hao wakina mama ndo wanunuzi wazuri wa magazeti ya kiu,ijumaa,ijumaa wikiend,uwazi n.k............. they dont wanna think deeeeeeeeeeeeep kwa picha kama za akina kanumba hufikirii sana mwisho inakuwaje
 
muvi ndani ya 3 days,kamera za basdei,uhalisia hakuna, too much umombo uliovunjika,adisi za kuiga............................aaah
 
mimi binafsi siiangalii movie za kibongo, ni bora niaangalie comedy za majuto na pembe zinauharisia wa vichekesho, ma actor na ma actress wa bongo hawana mpya ni bora wajiunge na maigizo tu.
 
wenzenu wanauza nyie mmekalia maneno tu hapa badala ya kuangalia waboreshe wapi mnaponda wakati mkiwa majumbani kwenu mnaangali

UJUMBE: Sikiliza/angalia wimbo wa UTAIPENDA wa Hussein Machozi ujumbe wako unaenda kwenu

Tujifunze kupenda vya nyumbani
 
Ubora wa hali ya juu wa filamu za nje umetuathiri mno itakuwa ngumu kuvutiwa na hizi za kibongo ambazo zipo kama tamthilia vile.
 
Back
Top Bottom