Safi mkuu,umesimamia ulichosema. Hawa jamaa wanatunyanyasa sana na riwaya zao. Ubarikiwe.TAMUTAMU
NYEMO CHILONGANI.
KALAMU YENYE SIRI YA DAMU
0718069269
Sehemu ya 17.
Watu hawakujua kilichokuwa kimetokea, taarifa zilisema kuwa Chuo Kikuu cha Brooklyn kililipuliwa kwa bomu, waliona hujko Uarabuni lakini kwa Marekani na nchi nyingine ambazo hazikuwa Uarabuni, hapakuwa na kitu kama hicho.
Hilo likaibua maswali mengi, watu walitaka kufahamu hasa kilichokuwa kimetokea, kama kwenye televisheni hizo lilionekana tukio hilo na kwingine halikuonekana, kulionekana kuwa na tatizo sehemu.
Mkurugenzi wa CNN, Bwana Stephan Bull akapiga simu mpa huko Uarabuni na kutaka kupata uhakika wa kile kilichotokea, ni kweli aliambiwa kama alivyosikia, alichanganyikiwa kupita kawaida.
Vijana wao wa IT wakaanza kufuatilia kilichokuwa kimetokea, ilikuwa ni lazima wajue ukweli wa kila kitu kwani kama kweli hilo lilitokea, walihisi wangeingia kwenye ugomvi na serikali ya Marekani kwa kuwaambia kulilipuliwa kumbe nchi ilikuwa na amani tele.
Vijana hao wa IT ndiyo waliofuatilia na kugundua kwamba kituo hicho cha habari kilidukuliwa, mbaya zaidi hawakujua ni nani alikuwa nyuma ya tukio hilo.
Kulikuwa na picha zilizoonyeshwa, za watu walioonekana kuwa kwenye tukio hilo, waliwafuatilia watu hao lakini hawakuweza kuwagundua. Bwana Bull na uongozi wake ukakaa kimya kwa kutegemea wangepigiwa simu na kuulizwa kilichotokea lakini kitu cha ajabu hapakuwa na simu yoyote ile iliyoingia.
Hakujua kwamba serikali hiyohiyo kupitia CIA ndiyo waliokuwa wamedukua na kufanya kile walichotaka kufanya, na kweli kilifanikiwa kwa asilimia mia moja.
Wakati hayo yakiendelea, upande wa pili Said alichukuliwa na kupelekwa katika kisiwa kimoja, hakujua kilikuwa wapi lakini aliamini ilikuwa ni mbali kwani hata kusafirishwa kwake ilitumika ndege huku akiwa amefumbwa macho kwa kutumia kitambaa kigumu.
Moyoni mwake alikuwa akijuta kwa kile alichokifanya, alikuwa na lengo la kujitoa mhanga lakini bahati mbaya kwake hakuwa amefanikiwa, aliumia, aliona mataifa yote ya Kiarabu yakimlaumu yeye kwani kila mmoja aliamini angeifanya kazi yake vema kabisa na kuwaliza Wamarekani lakini hakuwa hivyo.
Aliingizwa ndani ya chumba kimoja kilichokuwa kidogo, kilikuwa na maji machafu yaliyomfikia ugokoni, kulikuwa na vyura mbalimbali, kila aina ya uchafu ulikuwa ndani ya chumba hicho. Mbali na hayo pia kulikuwa na nyoka kama sita waliokuwa wakizunguka huku na kule.
Alikuwa akiogopa lakini nyoka hao hawakuwa na sumu, waliondolewa, waliwekwa humo kwa lengo la kumtisha, kumuogopesha siku nzima.
Aliwekwa ndani ya chumba hicho kisichokuwa na kiti wala mkeka, alitakiwa kusimama na kama kweli alitaka kukaa basi akae kwenye maji hayo machafu.
Sehemu yote ilikuwa kimya, hakumsikia mtu yeyote akiongea ama hata kusikia muungurumo wa gari, alizihesabu siku zake ndani ya chumba kile, akagundua alikuwa na siku chache mno na inawezekana baada ya siku kadhaa angekufa huku ndugu zake wakiwa hawajui mahali alipokuwa.
Alikaa siku ya kwanza, ya pili mpaka siku ya tatu huku akipewa chakula ambacho hakikumshibisha na maji ambayo hayakumtosha, baada ya siku hizo, mpango ukafunguliwa na kutolewa nje, akapelekwa katika chumba kingine kabisa.
Watu waliomshika kumpeleka huko walikuwa wanajeshi wa Kimarekani waliovalia magwanda yao, hawakucheka, walinuna muda wote na walivyokuwa wakionekana, walikuwa watu wenye roho mbaya kuliko wote ambao aliwahi kukutana nao kwenye maisha yake.
Akapelekwa kwenye chumba kimoja kikubwa na kuwekwa kwenye kiti, wanajeshi wale wakaondoka na baada ya dakika kadhaa, mlango ukafunguliwa na mwanaume mmoja kuingia huku akionekana kuwa kwenye hali ya kutohitaji urafiki hata kidogo, alikuwa mahali hapo kwa kuwa alihitaji kujua alichotaka kujua.
Mwanaume huyo alikuwa Todd.
Akavuta kiti na kutulia, alimwangalia Said, alionekana kuwa na hofu nzito moyoni mwake, kwa kile alichokuwa akipitia mahali hapo, alikuwa radhi kusema kitu chochote ambacho angeulizwa bila kupewa adhabu yoyote ile.
“Nani yupo nyuma ya mikakati yenu?” aliuliza Todd huku akimwangalia Said.
“Anaitwa Omar!”
“Yupo wapi?” aliuliza.
“Sijui!”
“Kwa nini hujui?”
“Huwa tunapewa maelekezo ya cha kufanya, lakini hatuambiwi mahali alipo,” alisema huku akimwangalia Todd.
“Mnapokea maelezo kutoka kwa nani?”
“Kwa huyo Omar!”
“Namaanisha Omar anampa nani halafu naye anawapa nyie? Nataka kumjua mtu huyo,” alisema Todd.
Saidi akakaa kimya, kumtaja Abdallah lilikuwa suala lisilowezekana hata kidogo, kumchoma mwanaume huyo haikumaanisha angeachwa hai, ilikuwa ni lazima aadhibiwe au hata kufungwa maisha kwenye gereza la Guantanamo.
Pamoja na kufikiria hayo yote lakini alijihakikishia kwamba alikuwa Mwarabu. Waarabu wote ambao waliingia kwenye mambo ya ugaidi waliambiwa ni lazima wawe wavumilivu, watu wenye misimamo, wasiotoa siri zozote zile hata kama wangepewa mateso ya aina gani.
Hilo lilipokuja kichwani mwake, akaamua kunyamaza, alipanga kutoa ushirikiano lakini hakutaka tena kufanya hivyo, hiyo ilikuwa ni sawa na kuwasaliti wenzake, ilikuwa ni sawa na kumsaliti Allah. Akaamua kunyamaza.
“Huwa mnapokea maelekezo kutoka kwa nani?” aliuliza Todd.
“Siwezi kusema!”
“Huwezi kusema, kwa nini?”
“Kwa sababu mimi ni Mwarabu! Si mtu muoga, kama ni kifo, nipo radhi nife lakini si kuzungumza zaidi ya niliyokwambia,” alisema Said huku akionekana kumaanisha alichomwambia.
Maneno hayo yalimtia hasira Todd, akaamua kutoka ndani ya chumba kile na baada ya dakika chache, mlango ukafunguliwa na wanaume wawili kuingia wakiwa na jenereta dogo na nyaya mbalimbali.
Sasa ulikuwa ni muda wa mateso, wakamvua fulana, wakaanza kumchoma na nyaya za umeme lakini bado msimamo wa Saidi ulikuwa uleule, hakutakiwa kuzungumza jambo lolote lile.
Alikuwa na msimamo huo kama Mwarabu, hakutakiwa kuwa mwepesi, alivumilia mateso ya kupigwa na umeme, kukatishwa pumzi kwa kumwagiwa maji usoni lakini msimamo wake ulikuwa uleule.
Hawakuishia hapo, walikata kucha zake, hakusema, walimvua nguo yaka ya ndani, wakachukua waya mwembamba na kuanza kuupitisha katika njia ya mkojo, alisikia maumivu makali mno lakini bado hakusema ni mwanaume gani alikuwa nyum aya mipango hiyo.
Walimfanya kila kitu, wakakata mpaka chuchu zake, walimtoa miguu, walimvunja taya, walilipasua jicho lake moja lakini bado msimamo wake ulikuwa uleule, hakutakiwa kusema.
“You’d rather kill me,” (Ni bora mniue) aliwaambia kwa sauti ya chini, iliyokuwa na maumivu makali.
“You will tell us!” (Utatuambia tu)
“Am an arab! I wont tell you anything! I can’t betray my people, most of all, I can’t betray my Allah! Kill me now,” (Mimi ni Mwarabu! Sitowaambia chochote kile! Siwezi kuwasaliti watu wangu, kubwa zaidi, siwezi kumsaliti Allah) alisema na kutoa tabasamu lake, meno yake yalionekana, yalitapakaa damu.
Walitumia kila aina ya mateso lakini Said hakuwaambia walichokitaka, mwili wake ulikuwa na maumivu mpaka sasa akaanza kuhisi ganzi ikiwa imesambaa mwili mzima, yaani hata alipokuwa akichomwachomwa hakuwa akisikia maumivu tena.
Walihangaika naye na baada ya kuona wameshindwa kabisa, wakamchukua na kwenda kumfunga katika Gereza la Guantanamo, gereza lililokuwa likitumika kufungwa kwa magaidi tu, na ndani yake kulikuwa na mateso makali mno.
Walihitaji sana kujua kuhusu mtu huyo aliyekuwa Marekani, ilikuwa ni rahisi kumfuatilia Said hata kwa kupitia simu yake lakini hawakufanikiwa. Magaidi waliokuwa wakiishi Marekani walikuwa na akili mno.
Walijua walikuwa wakitafutwa hivyo hawakutakiwa kufanya matukio mengine ambayo yangewapeleka kituoni ama kuwatilia shaka, waliishi kama watu wema kumbe nyuma ya pazia walikuwa hatari, watu ambao hukutakiwa kabisa kuwakaribisha.
Nchini Afghanistan Omar alichanganyikiwa, tena alichanganyikiwa hasa. Moyo wake ulikuwa ukijiuliza maswali mengi kwamba ni kwa namba gani Wamarekani waligundua kwamba said alikuwa akienda kukilipua Chuo Kikuu cha Brooklyn na kumkamata.
Alihisi kulikuwa na mtu aliyemsaliti! Labda Abdallah? Labda Castro? Aliwafikiria watu hao, alichojijibu ni kwamba haikuwezekana, watu hao alifanya nao kazi kwa kipindi kirefu, waliheshimiana na kuaminiana, lilikuwa jambo gumu sana kuwasaliti kwa kipindi hicho.
Hakulala, alikuwa akifikiria mambo mengi na mwisho kabisa wazo lililomjia ni kuhusu huyo Juma Hiza ambaye Wamarekani walionekana kuwa nao, hakutaka kusbiri, akainuka na kuelekea chumbani kwa Miraji, alihitaji kujua ukweli kuhusu watu hao wawili.
Alimkuta Miraji naye akiwa kitandani, hakuwa amelala, alikuwa na simu mkononi ambapo humo kulikuwa na kile kitabu, alikuwa akisoma, alikuwa akipitia kila neno lililokuwa limeandikwa.
Kila kitu ambacho Chilo alimwambia, kilikuwa humo, kitabu kilijaza codes nyingi ambazo bila msaada wa Chilo hata naye asingeweza kujua hata kidogo. Alishangaa mno ni kwa namna gani mtu kama Chilo aliyajua mambo mengi aliyokuwa ameyaandika.
Baada ya Omar kuingia ndani, akaiweka simu chini na kumwangalia mtu huyo aliyeonekana kuwa na mawazo tele, akaanza kumwambia kuhusu lile lililotokea, kwa nini Wamarekani walimgundua Said? Ni nani alikuwa nyuma ya mpango huo.
“Kuna kitu nahisi!” alisema Miraji.
“Kitu gani?”
“Inawezekana Chilo anamtumia na Juma pia,” alijibu.
Kusikia hivyo Omar akashtuka, hakujua Miraji alikuwa akizungumza kitu gani, alichokuwa akikifahamu ni kwamba huyo aliyekuwa akizungumza naye ndiye alikuwa Juma Hiza, lakini jambo la ajabu kabisa alimwambia kuwa inawezekana Chilo alikuwa akimtumia Juma Hiza.
Hakumjua Chilo, hakuwahi kulisikia jina hilo na hakujua alikuwa akifananaje. Alichokifanya ni kumuuliza kuhusu hilo alilomwambia, na bila kuficha kitu chochite kile, Miraji akaanza kumwambia kuhusu Chilo.
Huyo ndiye mtu aliyekuwa amekiandika kitabu hicho, na alimtumia yeye kwa kuwa hakutakiwa kujificha. Mwandishi wa kitabu hicho hakuwa Williams wala Juma Hiza, alikuwa huyo Chilo ambaye mpaka kipindi hicho hakujua alikuwa wapi.
Omar alimwangalia Miraji, alishindwa kuelewa alichokuwa akiambiwa. Alimwambia yeye hakuwa Juma Hiza, yaani aliyakana maneno yake ya kipindi cha nyuma, alimwambia hivyo kwa kumaanisha Wamarekani walikuwa na Juma Hiza, yule ndiye alikuwa mtu aliyetakiwa kuwa naye.
Mbali na kumwambia hivyo, pia suala la kumwambia kuwa Juma Hiza hakuwa mwandishi wa kitabu hicho ilimshangaza sana, aliyajuaje hayo yote? Miraji akaanza kumwambia kila kitu kuhusu Chilo, jinsi alivyomfuata na kumpa yale aliyokuwa amempa.
“Nitampataje huyo Chilo?” aliuliza Omar, alichanganyikiwa.
“Kumpata huwezi!”
“Kwa sababu gani?”
“Ukisoma kitabu utaelewa kwa sababu gani!”
“Kivipi?”
“Ana akili sana!” alimwambia.
“Sasa wewe una umuhimu gani kwangu?” aliuliza Omar huku akimwangalia, kwa kumwambia kuwa Chilo alikuwa mwandishi wa kitabu hicho ilimaanisha hakuwa na sababu ya kuwa na Miraji, hivyo ilikuwa ni lazima amuue.
“Kwa sababu Chilo amenipa majibu yote juu ya kitabu hiki! Kwa maana hiyo, kuwa na mimi ni sawa na kuwa na Chilo,” alijibu huku akiachia tabasamu pana. Omar akashusha pumzi ndefu.
“Nini kinafuata?” aliuliza Omar huku akionekana kuwa na hasira japokuwa sauti yake aliitoa kwa chini.
“Soma ukura wa 130 aya ya 6,” alimwambia, haraka sana Omar akafungua sehemu hiyo na kuanza kuisoma.
“Okonko alisimama bararani huku akiwa na hasira, mikono yake ilikuwa ikitetemeka, moyo wake ulikufa ganzi. Alibaki akiwa anaiangalia saa kubwa ya rangi ya shaba iliyokuwa ukutani, alitamani kuingia ndani ya jengo lile lakini alishindwa, angeanzia wapi na wakati kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiingia mfululizo?”a alipomaliza kusoma, akamwangalia Miraji.
“Nadhani umeshapata jibu ni wapi panafuata!” alisema Miraji, kidogo Omar akashangaa.
“Sijakuelewa!”
“Sehemu ya pili kulipuliwa ni katika kituo cha treni ya umeme cha City Hall,” alijibu.
“Ila hakujaandikwa sehemu yoyote humu!” alisema Omar.
“Najua! Ila umesoma kuhusu Okonko kuangalia saa! Si ndiyo?”
“Ndiyo!”
“Hakuna sehemu inayopatikana saa kubwa ya rangi ya shaba zaidi ya hiyo iliyokuwa kwenye kituo hicho!” alijibu Miraji.
“Kwa maana hiyo?”
“Utaangalia hata Google baadaye! Hiyo ndiyo sehemu inayotakiwa kulipuliwa,” alisema huku akimwangalia Omar.
“Ina watu wengi?”
“Ni zaidi ya watu elfu sabini wanasafiri kwa siku, hakikisha unakwenda na kulipua sehemu hiyo!” alimwambia.
“Ila nataka nikuulize kitu!”
“Kitu gani?”
“Kwa nini Chilo anataka tuzilipue sehemu hizo? Yeye ananufaika na nini? Je, tutaweza kulipua ama napo Wamarekani watatugundua?” aliuliza Omar.
“Sijajua! Ila kwa maelezo ya kitabu hicho utatakiwa kulipua kituo hicho!” alimwambia Omar ambaye hakuwa na shida yoyote ile, akachukua simu yake na kumpigia abdallah na kuanza kumwambia kuhusu suala hilo, ilikuwa ni lazima kituo hicho kilipuliwe, ila kwa sababu gani Chilo aliamua hivyo? Hakuwa na jibu.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane tena baada ya ziara...mwezi wa pili ama wa tatu mwaka kesho.
Tchao!
Vitabu bado vinaendelea kupatikana
yeah niliahidi akiweka kule na mimi naikopi naileta labda aache kuiwekaSafi mkuu,umesimamia ulichosema. Hawa jamaa wanatunyanyasa sana na riwaya zao. Ubarikiwe.
Asante sanaTAMUTAMU

Utamu umezidiMadam S imekuaje tena tumenogewa wenzio
![]()
Viewers 8,212Hii hadithi humu haina wafuatiliaji, acha iishie hapa.
Umeaomeka ndugu naash NashMkuu nyemo wafuatiliaji wako wengi sana JF uzi wako huu una viewers 8,212
Semaa wakuu Tujitaidi kumsupport Chief Nyemo ata kwa Thanks tu sio tunapita kwa speed ya 5G kimya kimya