Hawa TANESCO wanamatatizo sana, kama mtu akijenga karibu na high tension line wanambomolea nyumba yake kwamba anahatarisha usalama wake. Je hili la sasa kupitisha line karibu na kanisa lenye maelfu ya waumini, ikitokea ajali ya waya kukatika hao watu watakaokufa tutasema ni mapenzi ya Mungu? Maswala mengine hayahitaji hata kumaliza shule ya chekechea ili ujue hatari iliyo mbele ya mpango huu wa TANESCO! TANESCO tafuteni mahali pengine pa kupitisha nyaya zenu sio mahali kwenye makazi ya watu.