Kakobe: JK Kavuruga Mchakato wa Katiba, amtaka aombe radhi

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Kakobe amlaumu Kikwete

Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe, amemshambulia Rais Kikwete kwamba ndiye aliyevuruga mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

Kakobe amewataka wajumbe wa UKAWA kutorejea katika Bunge Maalum la Katiba ambalo alidai limejazwa unafiki na endapo wakiamua kurejea watakuwa wamerogwa.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 25 ya kanisa hilo lililoanzishwa mwaka 1989.
Alisema Rais Kikwete, alipolizindua Bunge Maalum la Katiba, alitumia fursa hiyo kutoa hoja za kuvuruga rasimu ya wananchi ambayo iliwasilishwa na Jaji Joseph Warioba.

Askofu Kakobe alisema hoja za Rais Kikwete za kujikanganya alizozitoa siku hiyo, yalikuwa ni majibu ya maombi ya Jumuiya ya Wakristo wa Kipentekoste (PCT) ya kuvuruga mchakato wa katiba baada ya kutoa upendeleo kwa kuwateua baadhi ya wajumbe wakiwamo viongozi wa dini, kupata uwakilishi kwa baadhi ya Wakristo bila kutenda haki kwa wananchi wote.

Alisema katika mambo yanayofanywa makusudi na wanadamu, Mungu amewapa akili ya kuyavuruga, hivyo ndiyo maana wakiwa katika viwanja vya Sabasaba waliamua kufanya maombi na nguvu ya Mungu inatumika sasa kuonyesha kuwa mchakato huu ulianzishwa pasipo haki.

"Namtaka Rais Kikwete akiri hadharani kuwa amekosea na awaombe Watanzania radhi kwa makosa aliyoyafanya hata kusababisha wanasiasa upande wa upinzani kuunda UKAWA ili haki ya wananchi ipatikane, hivyo atumie busara kufanya hivyo kwa kuwa ndiye baba wa taifa hili.

"Kuna kauli za viongozi wa CCM kuwa wanataka kutawala milele… sasa mimi nasema sawa tu wafanye hivyo, lakini kwa kwenda na haki na siyo kwa kulazimisha kama ilivyo sasa katika suala la katiba… hivyo ni katiba ya wananchi wote wa Tanzania ambao wamo vyama vya siasa na wasiokuwemo," alisema.

Askofu Kabobe alisema katika kujikweza kuwa hajahusika kuvuruga, Rais Kikwete, amewatumia vibaya viongozi wa dini aliodai wanaegemea upande wa CCM kuwataka waombee mchakato wa katiba na kuwataka UKAWA warudi bungeni, huku akijua watumishi hao wanapaswa kufanya kazi isiyo na upendeleo.

"Daima nitasimama katika kweli nayo itaniweka huru, hapa nasema wazi kwamba Rais Kikwete ameamua kuwatumia vibaya viongozi wa dini… nao wakaona bora watumike ili kupata mkate na chai Ikulu ambayo majani yake ni ya hapahapa nchini, tena Mufindi, siyo dhahabu, wanachoendelea kukifanya kwa wanachi ni unafiki wala siyo maombi.

"Nilidhani Rais Kikwete atawaambia viongozi hao wamwombee yeye aliyevuruga mchakato huu na siyo kuuombea mchakato wa katiba na amani… mimi najua nchi yetu ina amani na amani itavurugwa na hao wanaong'ang'ania hoja zao, kwani katika hili gumzo la katiba linaloendelea mtu mjinga tu ndiye atakayewalaumu UKAWA.

"Nawaomba viongozi wa dini wasijikombe kombe Ikulu maana wao wanamwakilisha Mungu… siogopi kusema kwa sasa hakuna ninachokosa hapa duniani wala sitaki kupendwa na rais, nitafanya yampendezayo Mungu," alisema.
Huku akirudia rudia neno lake kwamba "sema ukweli ili uwe huru", Askofu Kakobe alisema anawaunga mkono UKAWA kwa hatua yao waliyofikia hadi sasa hadi hapo Rais Kikwete atakapoomba radhi na kukubali wakajadili rasimu ya wananchi, kama watarudi bila makubaliano hayo, basi watakuwa wamerogwa.

"Nawaunga mkono UKAWA asilimia 100 kwa 100 na ninawaongeza 50 kwa hatua yao… sasa warudi kwa kauli ya rais kukiri mbele ya wananchi kuwa amekosea, anajirekebisha ili wajadili rasimu ya katiba, wasipofanya hivyo basi watakuwa wamerogwa… hakuna maridhiano hapo maana nimefuatilia na kubaini mazungumzo yanayoendelea yamejawa unafiki.
"Kuwaunga mkono UKAWA kwangu si kwamba nashabikia chama kimojawapo kinachounda umoja huo hapana… nazungumza kama baba wa kiroho mwenye kuwachunga watoto wengi wenye vyama vyote vya siasa ambavyo vipo nchini, ambao wanajua kwamba ninasimamia ukweli tupu," alisema.
attachment.php

 

Attachments

  • kakobe.JPG
    kakobe.JPG
    69.2 KB · Views: 2,291
  • KAKOBE2.JPG
    KAKOBE2.JPG
    44.7 KB · Views: 1,337
  • KAKOBE-2.JPG
    KAKOBE-2.JPG
    58.7 KB · Views: 1,315
Kakobe ni mfuasi wa CDM na anamachungu ya kutoteuliwa kwenye bunge la katiba,lazima aseme chochote
 
Katoa mtazamo wake wa nani alaumie na ninani alie vuruga mchakato.
 
Napenda viongozi wa dini kama Kakobe ambao kwenye mambo muhimu ya Kitaifa huwa wanasema ukweli mtupu si kama wanafiki wengine ambao baada ya kupewa bahasha nene na mpunga basi husimama upande mmoja na chama cha wahuni, majangili, magaidi, mafisadi, wauza unga na wanafiki kwa jina maarufu la Maintarahamwe.
 
Napenda viongozi wa dini kama Kakobe ambao kwenye mambo muhimu ya Kitaifa huwa wanasema ukweli mtupu si kama wanafiki wengine ambao baada ya kupewa bahasha nene na mpunga basi husimama upande mmoja na chama cha wahuni, majangili, magaidi, mafisadi, wauza unga na wanafiki kwa jina maarufu la Maintarahamwe.

Huyu hategemei ruzuku wala fadhila toka serekalini.
 
Kakobe ni mfuasi wa CDM na anamachungu ya kutoteuliwa kwenye bunge la katiba,lazima aseme chochote
Mchakato wa katiba umeanzishwa na mwenyekiti wa CCM Rais JK , harafu akateuwa Wajumbe wa Tume na kumuchagua Jaji Warioba ambaye ni CCM na mtu wa karibu na BABA wa Taifa!!
Sasa KAKOBE anamuunga mkono Jaji Warioba ambaye ni CCM iweje wewe unatuchanganya ???
Kwani Warioba ni CDM??
 
Mchakato wa katiba umeanzishwa na mwenyekiti wa CCM Rais JK , harafu akateuwa Wajumbe wa Tume na kumuchagua Jaji Warioba ambaye ni CCM na mtu wa karibu na BABA wa Taifa!!
Sasa KAKOBE anamuunga mkono Jaji Warioba ambaye ni CCM iweje wewe unatuchanganya ???
Kwani Warioba ni CDM??

Mpuuzie huyo
 
Kakobe ni mfuasi wa CDM na anamachungu ya kutoteuliwa kwenye bunge la katiba,lazima aseme chochote

Mnyika hakukosea kusema kikwete ni dhaifu yaani wajumbe aliwateua yeye tena wanaccm wenzake akawajaza, ukizingatia walikuwa wanampa mtejesho nini kinaendelea baada ya kukamirishwa akaisifia lakini baada ya kupigwa biti na nape akaingia upepo akabadilika...
 
Taifa linahitaji viongozi wa dini, kisiasa, kijamii na serikali wenye uthubutu wa namna hii! Mungu awaangazie wawe na uthubutu huu hao wengine ili wasimamie kweli yake! Amen!
 
Huna kumbukumbu wewe! Kakobe alisimama hadharani pale jangwani akiunga mkono haraksti za cdm,inawezekana ww huna kumbukumbu
 
Back
Top Bottom