Kakobe - Ishu nzima na wapi hela zinaenda yawekwa peupe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe - Ishu nzima na wapi hela zinaenda yawekwa peupe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by werawera, Jun 30, 2011.

 1. w

  werawera Senior Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ahsante kwa ufafanuzi wenu na wenzako filadelfia na smirna.

  Ila mumshauri Askofu wenu ajitahidim kufanya mambo yake barazani, hii ya kufanya mambo makubwa na mazuri kifichoni sio nzuri, ndipo hapo wabaya wake wanapata nafasi ya kueneza uoingo dhidi yake.
   
 3. n

  njija Senior Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mwita, umesema vizuri kuwa askofu kakobe aweke mambo mazuri barazani,ila mimi najua kuwa Kakobe huwa anafanya hivyo kwa washirika wake yaani kuwashirikisha,hawezi kufanya kitu bila kuwashirikisha washirika.Sasa kwa mfano anaposaidia Yatima na Wajane au kujenga kanisa n.k watu wa nje inawahusu nini? mimi binafsi sioni haja ya kuweka hadharani kwani kwetu sisi wakristo tunapofanya jambo tuna hitaji Mungu atukuzwe na sio sisi kutukuzwa na kusifiwa na watu,tatizo kubwa lililopo kwetu waafrika wengi huwa tunapenda kuongelea jambo la mtu bila kuwa na uthibitisho, hivyo huwa nashangaa sana mtu mwingine anaweza kuongelea jambo la mtu ukimwuliza umejuaje anasema niliambiwa na mtu lakini the way anavyo eleza utafikiri alikuwepo na analielewa vizuri jambo husika, ndio maana ndugu zangu tuwe makini katika kutafuta ukweli wa jambo, tupende kutafuta ukweli kabla ya kumzungumzia mtu kwa ubaya tutajipatia dhambi zisizo na sababu.
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe, mojawapo ya majukumu ya kanisa ni kutembelea wagonjwa na kuwafariji na kuwqasaidia wanajamii, sasa kama nyie mnafanya kazi hizo kwa kuwalenga waumini wenu tu, mtakuwa mnakosea kidogo. Hata hivyo mkifanya kitu mkaita waandishi wa habari wakashuhudia mlichokifanya haiondoi ukweli kwamba dhamira yenu ni kumtukuza Mungu. Mbona mlikuwa mnatuonyesha saa ya maajabu kupitia start tv tukawa tunashuhudia watu wengi wakitoa ushuhuda, sasa kama ukiicchukua kwa mtazamo hasi utaona kwamba mlikuwa mnafanya makosa. Ama mlipotuonyesha ziara ya Askofu Kakobe kule korea, DRC, Burundi na Zambia mbona haikuonekana kwamba mnajiinua lakini jina la Mungu ndiye aliinuliwa kupitia kwenu. Kakobe ni mtumishi wa Mungu kwahiyo jina la Mungu anainuliwa kupitia kwake.

  Mimi ushauri wangu ni kwamba kwakuwa mmezungukwa na watu wa jamii mchanganyiko na wasiojua mnachokifanya na ili mkupunguza hizi speculations, jitahidini kufanya mambo yenu barazani. Vinginevyo muwe tayari kuja kujibu tuhuma hapa kila kukicha.
   
 5. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  .Mimi nakubaliana na Kakobe kwa njia aliyokuwa anaitumia kuwahudumia wajane, yatima na maskini. Hii ni kulingana na biblia mia kwa mia. Kwa sababu biblia inaelekeza kutoa sadaka kuwe kwa siri. Siri hii inawajumuisha wote wanaotoa na wanaogawiwa. Hukuna haja ya kupiga panda, kwa sababu thawabu haitolewi na watu bali Mungu wa sirini ajuae pia nia ya ndani ya mtoaji. Kanisa linalazimishwa kuendeshwa kama vyama vya kijamii au vya siasa. Sii haki hata kidogo, kwani katiba za tawala hizi mbili ni tofauti. Cha msingi ni uwazi wa kilicholetwa kwa siri(sadaka) kujulikana kwa walengwa na pia matumizi kujulikana na walengwa na sii hata siku moja kwa walimwengu. Kumpa masikini kiroba cha unga na kumpiga picha kuionyesha dunia ni unyanyapaa uliozoeleka kufanya na watu wenye nia ya kujinufaisha na misaada watowayo. Kwingineko wafanye hivyo lakini sii kanisa, maana Mungu amelikataza kufanya hivyo..
   
 7. n

  njija Senior Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ulichokisema kuhusu utoaji ni sahihi kabisa bilblia inasema katika Mathayo 6:3-4 sadaka ni jambo la siri, tena imekazia zaidi kuwa utoapo hata mkono wako wa kushoto usijue, mstari wa nne inasema SADAKA YAKO IWE KWA SIRI NA BABA YAKO AONAYE SIRINI ATAKUJAZI. Katika hilo kanisa lilijua kuwa linafanya hivyo kwa upendo kuwasaidia YATIMA , WAJANE NA MASIKINI sawa sawa na Neno la MUNGU LINAVYO AGIZA, NASIO KATIKA HILO TUU NA MENGINE MENGI IMEKUWA NI SEHEMU YA MAISHA KATIKA KANISA WAKIJUA YUPO MUNGU ANAYEONA SIRINI MWENYE KUTOA BARAKA.
   
 8. g

  great vision Senior Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Mimi nami ninakubaliana na wewe mkuu,nachofanya ni sahihi kabisa kulingana na Biblia "real Bishop" like Kakobe anapaswa kufanya hivyo kwa sababu ni muongozo anaopewa na Mungu
   
 9. g

  great vision Senior Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
 11. n

  njija Senior Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Link imekataa kufunguka nadhani wengi tungependa kujua kilichomo kuhusu MTUMISHI WA MUNGU KAKOBE, msaada zaidi kama inawezekana.
   
Loading...