Kakobe Askofu Mkuu wa kudumu FGBF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe Askofu Mkuu wa kudumu FGBF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ESAM, Jul 11, 2011.

 1. E

  ESAM JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Maaskofu na wachungaji 447 wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) kwamba Askofu mkuu wao Zachary Kakobe atakuwa askofu wa kudumu na kila watakapokuwa wanakutana watakuwa wanamptisha bila kupingwa. Msimamo huo waliotuoa jana katika Kanisa la FGBF Mwenge, Dar es Salaam ambapo walikuja kueleza kile kilichojiri katika mkutano wao mkuu huko Dodoma. Maaskofu wote 19 wa FGBF Tanzania nzima walikuwepo na wachungaji zaidi ya 400, isipokuwa 37 ambao pia hawakuhudhuria mkutano wa Dodoma.

  Souce: Mimi mwenyewe nilikuwepo kanisani, lakini nawawekea habari kutoka Mwananchi la leo:

  Kakobe amechaguliwa tena kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

  Kakobe alichaguliwa kwenye mkutano Mkuu wa kanisa hilo uliofanyika mjini Dodoma Julai 4 hadi 9 mwaka huu.

  Akizungumza kwenye ibada maalumu iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana Kakobe aliwaambia waumini wake kuwa alichaguliwa akiwa mgombea pekee katika nafasi hiyo.

  “Katika uchaguzi ule hakuna mtu aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo, hadi tunaanza mkutano hapakuwa na jina, hali hiyo ndivyo ilivyokuwa hata katika mikutano ya uchaguzi katika vipindi vitatu vilivyopita,”alisema Kakobe.

  Kakobe alisema hiyo ni kutokana na kanisa lake pamoja na viongozi kuona suala la uongozi na vyeo siyo kitu cha msingi kwa na badala yake kuhubiri neno la Mungu.

  Akizungumzia uchaguzi alisema ulitimiza vigezo kwa kuhudhuria na wajumbe wote wa mkutano mkuu ambao ni maaskofu na wachungaji.

  “Mkutano ulihudhuriwa na wajumbe 447 ambao kati yao ni maaskofu 19 toka kanda zote za Tanzania na wachungaji wote,”alisema.

  Katiba ya Kanisa
  Alisema uchaguzi ulifanyika Dodoma ulikuwa halali na ulitokana na utaratibu uliowekwa na kanisa hilo kwa mujibu wa sheria na katiba na si shinikizo la watu waliofungua kesi mahakamani.

  Katiba ibada hiyo Askofu Kakobe alitumia muda mwingi kuzungumzia katiba ya kanisa hilo aliyodai wengi wanaipotosha.

  “Watu wengi wanatumia katiba hii ya mwaka 1987, wakati huo kanisa hili halikuwapo na kulikuwa na kikundi cha uinjilishaji kilichojulikana kwa Gospel Evangelist Team.

  Alisema kikundi hico ambacho yeye alifanya nacho kazi kama kiongozi wake kilikuwa na jukumu la kufundisha injili nchi nzima na kulihusisha mkusanyiko wa vijana kutoka makanisa mbalimbali.

  Alisema baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu Kakobe alifanya uchaguzi na kugundua kuwa waumini wake hawakuendelea na imani waliyofundishwa ndipo alipopatwa na maoni ya kuanzaisha kanisa la FGBF.

  Alisema hatua hiyo aliifanywa mwaka 1989 alipowasilisha taarifa wizara ya Mambo ya Ndani ya kutaka kubadilishwa kwa jina la Taasisi ya BET na kuwa FGBF.

  Alisema baada ya hatua hiyo ndipo walipoandika katiba mpya inayotumika hadi sasa.

  Kakobe alifafanua kuwa kwa katiba inampa mamlaka Askofu mkuu kuteua katibu Mkuu, mweka hazina na maaskofu wa majimbo mbalimbali.

  Alisema pia askofu huyo ndiyo mwamuzi wa mwisho kwa mujibu wa katiba juu ya mambo yote yahusuyo kanisa ikiwa ni pamoja na nidhamu pamoja na mafundisho.

  “Katiba inampa mamlaka askofu kuonya na kuwafukuza wanachama au waumini pindi anapoona ipo haja ya kufanya hivyo,”alisema Kakobe.

  Katika ibada hiyo Kakobe huku akinukuu vifungu vya katiba alimteua na kumtangaza Askofu Nathan Meshack kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa hilo na Askofu Jimmy Sekuye kuwa mweka hazina.

   
 2. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Kakobe na FGBF sawa na Messi na Barca, hakuna wa kumweka benchi
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote. Kuna siku waumini wake watadai uhuru na demokrasia katika kanisa lao, maana kanisa lao viongozi wanachaguliwa na sio kuteuliwa. Haiwezekani wachungaji???/maaskofu??? wote wakawa hawataki ulaji!!!!!!!!! Nani asiye na watoto, mke/wake??? ambao wanataka matunzo, elimu etc, nani asiyetaka kujenga nyumba kwa familia yake baadaye waachie watoto in case etc. Kuna siku watadai demokrasia.
   
 4. E

  ESAM JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kanisani huwa hakuna demokrasia, huwa kuna theokrasia. Mambo ya FGBF yanawahusu wao ndiyo maana maaskofu na wachungaji wakafanya hivyo kwani wanajua uzuri na ubora wa Kakobe basi. Na huwezi kusema kadanganya, mtu mmoja atadanganya watu 400+. Wenyewe wamesema FGBF ni ndege ya kuwapeleka mbinguni na rubani wake ni Kakobe tu mpaka atakapokufa Mungu atawapatia mwingine lakini kwa sasa huwaambii kitu bwana hata uje na tuhuma gani wao wanamjua.

  Halafu ndugu yangu kanisani hakuna ulaji. Kwa mfumo wa FGBF waumini wa kanisa la mahali (local church) ndiyo wanahakikisha mchungaji wao anapata mahitaji yote anayotaka. Na kwa kanisa la DSM lazima washirika wa hapa wahakikishe Kakobe kama mchungaji wao anapata mahitaji yote muhimu ili aweze kuwahudumia vizuri, ndiyo maana hana shamba, duka wala akaunti benki
   
 5. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kaka umeweka hii thread kwa ajili ya maoni ya watu sasa unachofanya ni kumtetea kakobe why? ina maana hamna uhuru wa maoni?
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kanisa la kakobe wameamua kumuchagua kakobe , na watu wote wanaakiri timamu, na ndio maana wamehama kutoka kwenye makanisa mengine na kwenda hapo, hata wakaamua kujiwekea kiongozi wao hata kama wataamua atawle milele.

  Sasa kwa nini watu wasio wa fgbf waingilie uchaguzi wa fgbf?

  Kwa nini ccm na mafisadi wanaiingilia uchaguzi wa makanisa??

  Mwaka jana akina lowasa walitaka kuingilia uchaguzi wa kkkt leo watu wanahoji uteuzi wa kakobe wakati hawayatambui mafundisho ya kakobe!!!


  Sasa wewe kama hutambui ulokole kwa nini uhoji uchaguzi wa ulokole???

  Huu ndio udini!!!
  Kuingilia maamuzi ya dini nyingine!!!

  John worsey alipinga mambo ya katoliki akajitoa huko na kuanzisha huduma yake na wala hakuhoji mambo ya katoliki!!!

  Martini ruther aliasi katoliki , na kuanzisha kkkt na hakuwahi kuhoji mambo ya katoliki!!!


  Sasa wewe unahoji uteuzi wa kakobe , je wewe ni fgbf ? Au unatumika na ccm
   
 7. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  cha maana hapa mambo mengi huwa tunayachukulia vijiweni. watanzania tuanze kufuatilia mambo kwa kina sio kwa kusoma vichwa vya magazeti.
   
 8. w

  wyclefmore Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 9. w

  wyclefmore Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani mwamakula muongo kabisa kkkt ilianzishwa na wamishenari wa kilutheri kutoka ujerumani na siyo martin luther.
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Tunapo angalia namna ya hizi chaguzi za makanisa tusisahau pia kwamba RC nayo papa akiisha chaguliwa ni mpaka kifo kimtenganishe nao
  .
   
 11. n

  ng'wandu JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako wewe unawaza ya duniani, wakati watumishi hawa wa Mungu wanawaza ya mbinguni. Hawako pale kwa ajili ya maslahi yao binafsi wala kutafuta ulaji. Wanawaza kumtumikia Bwana usiku na mchana, wametoa maisha yao kwa ajili hiyo tu. Askofu Kakobe mwenyewe pamoja na ukubwa wa kanisal analolichunga hajawahi kujenga nyumba yeyote kwa pesa ya kanisa. Nyumba anayokaa ni nyumba aliyoijenga mwenyewe kabla hajaitwa kuwa mchungaji. Gari analotumia amenunuliwa na watu kwa hiari yao wenyewe bila hata yeye kujua mpaka siku waliyomkabidhi. Hawazi hata siku moja kuweka uwekezaji wowote kwa ajili yake au familia yake. Na hata wachungaji wake wako hivyo hivyo.

  Katika utumishi wa Kristo watu hawakimbilii ukubwa na hakuna kitu kinachoitwa demokrasia kwa sababu ni Mungu mwenyewe ndiye anayewaweka watumishi wake. Mungu ndiye alimchangua Musa, Joshua, Eliya, Elisha, Petro, Paulo na wengine wengi.
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Demokrasia kanisan? Achen utani!
   
 13. w

  werawera Senior Member

  #13
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hii nayo ni POINT OF CONSIDERATION...
   
 14. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  ha haha hahaha wajinga ndio waliwao! ccter upooooo!!!!!!????
   
 15. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2014
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu ! Je, inawezekanaje mtoto kuwa Baba ?
  Ndio maana Askofu Kakobe atakuwa askofu mkuu mpaka kifo;kama papa katoliki.
   
 16. mkafrend

  mkafrend JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2014
  Joined: May 12, 2014
  Messages: 2,086
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Ndo mnaanza kuingia siasa kanisani? UKAWA, ACT na wengineo kule hakuna hoja tena? Mbona Papa anadumu mpaka anapoamua mwenyewe! Tungemlaumu ZAKARIA KAKOBE kama angefanya hujuma kwa wagombea wenza endapo wangejitokeza. Acheni kutembea uchi kichwani!
   
 17. m

  maguzumasese2005 JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2014
  Joined: May 1, 2014
  Messages: 647
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wizi mtupu
   
 18. Tujikomboe Finance

  Tujikomboe Finance JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2014
  Joined: May 8, 2013
  Messages: 213
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  John Huss alijitoa Roman catholic akaanzisha Moravian Church
   
 19. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2014
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Hii ndo jamiiforums
   
 20. Chokochoko

  Chokochoko JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2014
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  hao wengine wakitaka kuwa askofuu mkuu wakafungue makanisa yao lile nila kakobe akifa na huduma yake imekwisha
   
Loading...