LICHA ya mazungumzo ya takribani wiki mbili kati ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zachary Kakobe kuhusu mgogoro uliozuka wa waumini wa kanisa hilo kupinga Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitisha njia ya umeme wa msongo mkubwa wa kilovoti 132 mbele ya kanisa hilo, serikali imejikuta njia panda katika kufikia uamuzi.
Taarifa ambazo zililifikia gazeti hili jana zilieleza kwamba baada ya mazungumzo ya viongozi hao kumalizika wiki iliyopita, wataalamu wa wizara hiyo walikaa pamoja, ili kufikia uamuzi. lakini ukazuka mparaganyiko ambao uliwagawa, wengine wakaishauri serikali iwapuze huku wengine wakiwaunga mkono wakisema wana hoja ya msingi.
Hali hiyo, imempa wakati mgumu Waziri Ngeleja katika kutoa uamuzi, hasa ikizingatiwa kwamba baadhi ya wataalamu wake wanadai kwamba tayari mamilioni ya fedha yametumika katika njia hiyo jambo ambalo litaisababishia serikali hasara na hata kuwakasirisha wafadhili.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, tayari Tanesco wamejenga misingi na kuweka vifaa kwa ajili ya kufunga nguzo upande wa kanisa hilo lililopo barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, jijini Dar es Salaam na kwamba kuhamishia upande wa pili itawagharimu fedha nyingi ambazo kiwango chake hakikutajwa, lakini ikadaiwa ni mamilioni ya fedha.
Wataalamu hao wanadai kuwa hata upande wa pili wa barabara hiyo, kuna ubishi wa kuruhusu njia hiyo kujengwa ingawa ndiko kuna nafasi kubwa iliyobaki kwa hifadhi ya barabara ukilinganisha na upande wa kanisa.
Baadhi ya wataalamu wanaounga mkono msimamo wa waumini hao, wanadai kwamba sababu zilizotolewa na kanisa hilo ni za msingi na zinapaswa kuheshimiwa.
Miongoni mwa hoja za waumini hao ni kwamba kuwepo kwa njia hiyo ya msongo mkubwa kutasababisha muingiliano na mashine za kurekodi na kunasa sauti ndani ya kanisa hilo.
Isitoshe mpango huo utaathiri moja kwa moja mkakati wa kanisa hilo kuwa na kituo cha televisheni kwenye eneo hilo.
Wiki iliyopita Ngeleja alisema atatoa uamuzi wake wiki hii na juhudi za kumpata jana ziligonga ukuta baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana.
Mwananchi liliwasiliana na Naibu wake, Adam Malima, lakini alisema asingeweza kuelezea jambo lolote kuhusu suala hilo na isitoshe alikuwa kwenye kikao.
Mwananchi jana lilishuhudia waumini wa kanisa hilo wakiendelea kutoa ulinzi baada ya Tanesco kuwa na mpango wa kungâoa mabango mawili mbele ya kanisa hilo, ili kupisha njia hiyo ya umeme.
Kakobe aliliambia Mwananchi kwamba baada ya kumaliza mazungumzo na Ngeleja, wanasubiri uamuzi wa serikali baada ya kushauriana na wataalamu wake.
Kutokana na ubabe huo wa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini, kulazimisha kupitisha nguzo za msongo mkubwa katika kanisa hilo na kung''oa mabango ya kanisa hilo, jambo ambalo lilikuwa chukizo kubwa kwa Mungu.
Hivi sasa laana inazidi kuwatafuna serikali ya CCM, sawa sawa kabisa na maono aliyoyaeleza wakati huo, Mtumishi wa Mungu, Zacharia Kakobe, kuwa kutokana na kiburi na ubabe wa hali ya juu ulioonyeshwa na viongozi wa wizara hiyo ya Nishati na Madini dhidi ya kanisa hilo la Mungu, alitabiri mambo mawili makubwa yatatokea.
Mosi, alibainisha kuwa umeme huo wa msongo mkubwa uliopita hapo kanisani, hautakuja kamwe kuja kuwaka, jambo ambalo kweli lilitokea ambapo hadi leo, umeme huo uliopita kanisani hapo haujawahi kuwaka!
Kama kuna ofisa yeyote wa TANESCO atataka kulipinga hilo, ajitokeze hadharani kulikanusha hilo.
Pili, alitabiri kuwa wizara hiyo ya Nishati na Madini, itaendelea kukumbwa na laana kwa viongozi wake wakuu kukumbwa na kashfa mbalimbali, zitakazofanya watimuliwe kwenye nafasi zao.
Utimilifu wa utabiri huo tumeshuhudia tokea mwaka huo wa 2009, wizara hiyo ikijikuta Mawaziri na Makatibu wakuu wake wanashindwa kudumu kwenye wizara hiyo.
Tulishuhudia kipindi hicho, Waziri Ngeleja na Katibu wake mkuu Jairo, wakitimuliwa kwenye nafasi zao.
Hivi sasa tumeshuhudia pia Katibu mkuu Maswi na Waziri wake 'kiporo' Muhongo nao wakilazimika kung'oka toka wizarani hapo.
Ni wazi sasa serikali ya Sisiem itakuwa imepata 'somo' muhimu kuwa siyo jambo jema na la busara kulumbana, kuwanyanyasa na kuwapuuza watumishi wa Mungu, kama walivyofanya kwa huyo Askofu Kakobe.