Kakobe aitunishia misuli TANESCO

Kakobe aitunishia misuli TANESCO

Soma context ya hoja sio maneno kwenye sentensi. Ukifanya hivyo hutoelewa ninachokikusudia. Huwezi ukafuta hati ya ardhi kwa sababu tu kikundi fulani cha watu kinaprotest jambo fulani. Unless kama kuna jingine ambalo hutuambii hapa.
Usalama wa afya zao uko hatarini kama wanavyodai. Raisi anafuta ile hati kisha wanapewa eneo jingine lililo salama kwao na mradi wa umma unaendelea.
 
Wa TZ tuache kulalamika kila kitu. hivi tunafahamu kuwa katika ujenzi wa barabara hasa highways kuna eneo la barabara, drainage,utilities[bomba maji, umeme nk??]
Hebu tuangalie eneo lilipojengwa kanisa likoje???? Kama kuna lawama pengine ni kwa wanini kanisa liliruhusiwa kujengwa karibu sana na maeneo ambaya huduma hizo zilipaswa kupitisha hapo Jiji linawajibika lakini siyo TANESCO.
Kabla kutoa lawama kwanza tu-analyse situation halafu ndiyo tulalamike.
Tatizo kama hilo lilitokea mtoni mtongani ambapo msikiti ulijengwa kwenye eneo la reserve ya barabara lakini ilibidi ubomolewe na watafutiwe eneo la kujenga
 
Dini wakati mwingine ni kikwazo katika maendeleo, manake kutunishia msuli vitu vyenye kuleta maendeleo kwa watu wengi ndio kikwazo kikubwa cha dini nyingi ni ubinafsi na kutokupenda maslahi ya watu wengine zaidi ya waumini wao.

Manake ingekuwa Rwanda asingethubutu mtu kutunisha msuli katika vitu vyenye maslahi kwa umma. Please maslahi ya umma yawe mbele kwanza
 
ziunganishwwage basi mada hizi za kakobe!!!!!!


QUOTE=Pasco;736862]Saa hizi ni Saa 8:39 za usiku!, yaani usiku wa manane, nimepita nje ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, la Askofu Zakaria Kakobe, nikushuhudia mamia ya waumini wake wamekaa kwenye viti na meza nje ya kanisa hilo huku limepambwa na disco lights zinazobadilika badilika rangi, kwa mgeni aweza dhania ni night club fulani.

QUOTE]

Ndugu yangu inawezekana kakobe akawa na nguvu ...lakini kwa kuwa yeye naye ni mwanadamu anaweza kutumia nguvu au ushawishi wake vibaya....hainiingii akilini kuona kakobe anapingana na serikali..bila sababu za msingi..

umeme unapita ndani ya hifadhi ya barabara ambayo inamilikiwa na TANROAD ..ambao wameshawapa kibali TANESCO...ndani ya hifadhi ya barabara ndipo panapohusu upanuzi wa barabara,mitaro,simu,gesi,umeme,maji etc...zote hizo ni huduma za jamii...ambazo ndugu kakobe hazipiti kwenye eneo la miliki yake....isitoshe hata mabango yake ameweka kwenye eneo la TANROADS tena bila kibali chochote...kimsingi kakobe hana haki yeyote pale zaidi nafikiri anazo hasira ....labda kwa kushindwa kuzuia kisheria wakati eneo lake lote la parking la kanisa alilojengaga barabarani lilipobomolewaga wakati wa kupisha upanuzi wa barabara ya Sam nujoma.........

serikali ya kikwete ina staha sana na huruma nadhani ...nafikiri angekuwa ni mkapa angembomolea kama alivomvunjia parking mwaka 2005.....na kakobe anautumia vibaya upole wa kikwete....

jambo lingine ambalo ni hatari kwa usalama ..linalotokea mara ya pili sasa ni la baadhi ya viongozi wa dini kama hawa kutumia misingi ya imani kuwachochea waumini wao kufanya jambo...tuliona wakati viongozi wa dini walipotumia imani kali ya kikristo kuingiza DECI na kuwafanya waamini kuwa DECI ni mkombozi aliyeletwa na YESU.....sasa kakobe anawafanya watu waache kulala makwao na wake zao au waume zao ...wanakesha wanaumwa na mbu kulinda eneo ambalo si la kwao kisheria ....nafikiri iikiendelea hivi badi anao uwezo wa kuwashawishi wajichome moto kama kibwetere[samahani kwa kufikia hapo]...lakini ndiko tunakoelekea kama tutaruhusu watu watumumie imani za waumini wau ..kuwatumikisha watakavyo!!!......

ni bora watu wa usalama wakawa makini na kuibuka kwa fundamenalism ...iwe kwenye christian everngelism au muslim ...zote ni sawa ...pamoja na kuwa ndugu zetu yao inatokuwa movements tofauti na ya wakristo ambayo mtu mmoja anaweza kuwakusanya watu kama mazoba na wakasahau kila kitu na kumfuata yeye....badala ya Mungu!!!
 
Kama maslaha ya taifa mbele, zipo mamlaka za kulinda hayo maslaha, hivyo basi hili tuziachie zifanye hiyo kazi, nadhani zipo na zitafanya kazi zao barabara.
 
Usalama wa afya zao uko hatarini kama wanavyodai. Raisi anafuta ile hati kisha wanapewa eneo jingine lililo salama kwao na mradi wa umma unaendelea.

apewe eneo jingine ya nini ...mbona wananchi wengine wote hawakuzuia mradi ..wakijuwa kuwa unapita kwenye eneo la Tanroad road reserve????........nimeona nguzo za umeme zimeshawekwa kote kasoro pale kwake tu..kimsingi kampuni iliyopewa kazi ya ujenzi inaendelea kulipwa huku ikisubiri mgogoro utatuliwe watandaze nyaya.....hatujuwi ni shilingi ngapi za walipa kodi zinatumika kuwalipa hao wenye kampuni kila siku wakisubiri mgogoro utatuliwe wafanye kazi!!
 
Sijui sheria zetu zinasemaje kwa hili ila kwa kawaida sehemu inayopitishwa waya za umeme (waya za simu, mabomba ya maji, mabomba ya maji machafu, waya za fiber optics etc) ni public; mafundi wa umeme wanaweza kufika ndani ya eneo hilo wakati wowote kufanya matengenezohilo bila ya kushtakiwa kwa trespassing. Inapokuwa ni lazima waya hizo zipite kwenye kiwanja cha mtu, basi hilo hufanyika kabla mtu yule hajapewa na kuruhusiwa kujenga kwenye kiwanja hicho, na huambiwa kabisa kuwa ndani ya kiwanja hicho kuna eneo la public kwa ajili ya waya za umeme; asichimbe (kama ni undergraoudn) bila kutaoa taarifa kwa ofisi husika. In fact ujenzi wa nyumba yake utaruhusiwa tu iwapo hauingiliani sana na njia za waya hizo.

Vile vile taratibu nyingi za mipango miji huwa zinatenga eneo la umbali fulani pembeni mwa barabara kwa ajili ya infrastructure, yaani zinamopita waya hizo za umeme, waya za simu, fiber optic cables kwa ajili ya CABLE TV na Broadband internet, mabomba ya maji safi na mabomba ya maji machafu. Ndiyo maana ile Hotel ya Crest kule Arusha ilibomolewa kwa vile ilikuwa inaingia ndani ya eneo hilo.

Wakati mwingine plan za mipangomiji huacha maeneo mengine ya wazi kwa makusudi hata kama hakuna barabara kwa ajili ya future expansions za infrastructure.


Mina naona kama vile kwenye huu ugonvi baina ya Kakobe na TANESCO kuna possibilities tatu.

(1) Kakobe amejenga kwenye eneo la karibu sana na barabara na hivyo kuwa eme-encroach public land ambayo TANESCO wana haki nayo. NI LAZIMA KAKOBE ATII AMRI; Ni lazima asuate fundisho la Yesu kuwa Ya Kaizari mpe Kaizari

(2) Kakobe kajenga ndani ya eneo ambalo lilikuwa limeachwa wazi kwa ajili ya infrastructure, ambalo TANESCO wana haki nalo. NI LAZIMA KAKOBE ATII AMRI; Ni lazima asuate fundisho la Yesu kuwa Ya Kaizari mpe Kaizari

(3) TANESCO wameona ni convenient kuptisha waya zao ndani ya eneo halali la Kakobe ambalo halikuwa limetengwa kwa ajili ya public infrastructure na city planners. Itabidi TANESCO waache ubabe huo; hawawezi kuamua kuptisha transmission lines mahali popte pale. Namna hiyo wataweza kutupitishia transmission line hizo vyumbani mwetu.
attachment.php

 

Attachments

  • africa2.jpg
    africa2.jpg
    13.9 KB · Views: 152
msikiti wa kilwa road (MTONI) ilitolewa pesa ya kujenga MSIKITI MKUBWA KULIKO ULIOKUWEPO KARIBU KABISA NA ULIOKUWEPO......hii ilikuwa kwa msikiti...je yaweza fanyika hivyo kwa KANISA....?
MAKANISA MANGAPI YAMEVUNJWA BILA CHOCHOTE......(REMEMBER SHEKILANGO NEAR/OPPOSITE LEGHO HOTEL)
 
Kuhusu DECI nipo against na mtazamo wa mtumishi huyu,Ila kuhusu sakata hili la TANESCO am on his side......!
 
wale vijana wanaolinda usiku na mchana hawafanyi kazi kweli au ndio mambo ya kulinda hekalu la bwana
 
Mimi na fikiri kila mwanadamu anayo haki ya msingi ya kutetea uhai wake na usalama wa afya yake. Tumeona watu wanalishwa vyakula vibovu, wengine wanaathirika na mazingira mabaya makazini, au katikati maeneo ya public na watanzania tumezoea apathy. tena wakati mwingine anayekuwa aggressive kudai haki zake anaonekana msumbufu asiyeheshimu viongozi na mpinga maendeleo. Lakini hata kama waya zinapita katika road reserve lakini zina madhara kwa watu walio nje ya hiyo reserve nafikiri ni sahihi watakaoathirika wakawa macho. Tanesco iwaondoe wasi wasi kwa njia za kitaalamu kuwa hawatadhurika period!
 
Pamoja na kutojua sheria, waumini kwanini wanakesha wakilinda pale? Inamaana kuna siku kitu kikitokea ambacho mchungaji hakimpendezi, basi anaweza kuwaamuru kufanya lolote lile na likafanyika. Siamini dawa ya tatizo ni kulinda eneo lile.

Nailinganisha na wakati wa kutengeneza barabara ya Kilwa, pale mtoni mtongani kulikuwa na msikiti basi waumini wao walikuwa wasnashinda pale kuzuia tingatinga lisibomoe msikiti wao mpaka Serikali ilipowapoza kwa kuwajengea msikiti mwingine mzuri pembeni labda kakobe naye anataka afanyiwe hivyo
 
Naaamini umeme unapitishwa eneo la Kakobe ni wa msongo mkubwa. Kwa haraka sana naamini, kakobe akiwa technician wa electronics, atakuwa anafahamu hilo.

Tanesco wana kawaida ya kuzuia ujenzi karibu na nyaya zenye msongo mkubwa wa umeme, iweje sasa wao wanataka kupitisha nyaya hizo karibu na kanisa.

Sihitaji kushabikia suala hili ktk misingi ya imani lakini umeme mkubwa wowote ni hatari. Kisayansi kuna tafioti zinaonyesha uhusiano wa umeme na tatizo la leukemia (simply blood cancer). Ukitaka habari zaidi google maneno; leukemia electric cables.

NI HATARI. Bravo Kakobe!!!
 
TANESCO wamejifunza mengi kutokana na ujenzi wa mtambo wao huko Kihansi kwa hivyo hawawezi kufanya makosa yale yale kwa mara ya pili. Sheria inasema mradi kama ule lazima Environmental Impact Assessment ifanyike, na hilo limefanyika na Certificate imetoka. Wafadhili wako extremely careful na hili na huwa wanahitaji hizo certificates kabla ya kutoa fedha zao.

Analofanya Kakobe kuzuia eneo ambalo ni kwa ajili ya kuweka huduma, ni kuongeza gharama za hiyo kazi. Nani atalipa hiyo gharama ya ziada? - ni Watanzania wote kwa kupitia bili kubwa za umeme.
 
Naaamini umeme unapitishwa eneo la Kakobe ni wa msongo mkubwa. Kwa haraka sana naamini, kakobe akiwa technician wa electronics, atakuwa anafahamu hilo.

Tanesco wana kawaida ya kuzuia ujenzi karibu na nyaya zenye msongo mkubwa wa umeme, iweje sasa wao wanataka kupitisha nyaya hizo karibu na kanisa.

Sihitaji kushabikia suala hili ktk misingi ya imani lakini umeme mkubwa wowote ni hatari. Kisayansi kuna tafioti zinaonyesha uhusiano wa umeme na tatizo la leukemia (simply blood cancer). Ukitaka habari zaidi google maneno; leukemia electric cables.

NI HATARI. Bravo Kakobe!!!

kama umeme ni hatari kwa kanisa na waumini ..kanisa liondoke watafutiwe sehemu nyingine wajenge kanisa kwa usalama wao

Kanisa haliwezi kuzuia kupitishwa umeme..kwakuwa umeme unaende kusaidia waumini wa kakobe walioko sehemu zingine na watanzania wengine

issue labda ni bargain power kati ya tanesco na kakobe...kama ni malipo wampe malipo halali kabisa kabisa...wasitake kumlipa kiduchu kisa mradi...apewe haki yake umeme upite.
 
Hakuna haja ya kujenga mambo haya ya umeme kwa watu au halaiki ya watu wengi kama hivi lakini kama wanaona kuna haja ya kulinda basi wafanye hivyo na si kujenga umeme mkubwa kama hivi
 
kama umeme ni hatari kwa kanisa na waumini ..kanisa liondoke watafutiwe sehemu nyingine wajenge kanisa kwa usalama wao

Kanisa haliwezi kuzuia kupitishwa umeme..kwakuwa umeme unaende kusaidia waumini wa kakobe walioko sehemu zingine na watanzania wengine

issue labda ni bargain power kati ya tanesco na kakobe...kama ni malipo wampe malipo halali kabisa kabisa...wasitake kumlipa kiduchu kisa mradi...apewe haki yake umeme upite.

Nakubaliana nawe katika hayo hapo juu,haki inabidi itendeke
 
Hivi huku kuonyeshana ubabe kati ya TANESCO na Mchungaji Kakobe na waumini wa kanisa lake sijui nani mwenye haki na nisingependa kutaka ku argue ili hali sina facts zote

Je sheria inasemaje?

Na kama TANESCO wana makosa kwa nini wanawasumbua hawa waumini? Kama ni kweli kwa nini wanatumia tactics za kibabe kufanya kazi yao nje ya sheria kama wanavyotuhumiwa?


Na kama KAKOBE na kanisa lake wana makosa kwenye hili kwa nini wasi kae pembeni na kuacha TANESCO wafuate sheria ili watu na zahanati zipate umeme ambao utaokoa maisha ya wengi na kuleta unafuu wa hali zao?


Jamani nimeuliza Sheria inasemaje na kama hakuna mwenye kujua basi tuache speculations na si vibaya kama Badra akafikishiwa ujumbe kuwa this doesnt look good on TANESCO na aje aweke wazi msimamo wao kwa public

Lakini mbona mimi naona ishu yenyewe ni ndogo tu. Ninachojua ni kwamba Tanesco wanataka yale mabango mawili yapigwe chini then hizo nguzo zao zipite, so naona kama wangekaa meza moja ingekuwa ni busara zaidi ili kuwawezesha wale kina mama na akina baba kama sisi kaka wanaokesha pale waweze kuendelea na shughuli ya ujenzi wa Taifa.
 
sheria inasemaje?

Hivi JF hatuna mtu ambaye anaweza kuongea na wanasheria wakatuambia sheria inasemaje kuhusu hili?
 
Kuhusu DECI nipo against na mtazamo wa mtumishi huyu,Ila kuhusu sakata hili la TANESCO am on his side......!

on his side vipi?

ile service road ni public lakini wakati wa ibada ya kakobe inaleta usumbufu mkubwa hilo tu huwa linanitia kinyaa. lazima aheshimu maeneo ya public na awatafutie waumini wake parking hata kwa kuwanunua majirani
 
Back
Top Bottom