Kakobe aitunishia misuli TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe aitunishia misuli TANESCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, Dec 23, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Askofu Kakobe azuia Tanesco kupitisha nyaya eneo la Kanisa

  [​IMG]

  Askofu mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe kwa kushirikiana na waumini wake amewazuia wafanyakazi wa Shirika la umeme (Tanesco) kupitisha nyaya za umeme eneo la kanisa lakeNa Leon Bahati

  ASKOFU mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe ameligomea Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitisha mbele ya kanisa lake njia ya umeme ya msongo mkubwa wa kilovolti 132.

  Akofu huyo pamoja na mamia ya waumini wake, jana walikusanyika mbele ya kanisa hilo lililo kando ya Barabara ya Sam Nujoma karibu na Mwenge, jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kupambana baada ya kupata taarifa kwamba mafundi wa Tanesco wangewasili kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kupitisha njia hiyo ya umeme.

  "Mimi nimejiandaa kuongoza waumini wangu katika kukabiliana na yeyote. Mimi nipo tayari kufa na nitahakikisha hawapitishi njia hiyo labda wawe wameniua," alilalamika.

  Alilalamika kuwa iwapo umeme wa msongo huo utapitishwa eneo hilo utaathiri mitambo inayosaidia kunasa, kupaza na kurekodi sauti kwenye ibada zinazofanyika kanisani hapo pamoja na mpango wake wa kuanzisha kituo cha televisheni cha kanisa.

  Isitoshe, alisema kwamba tayari Tanesco wamemuarifu kuwa itabidi wayang'oe mabango mawili ambayo yaligharimu Sh120 milioni ili kupisha mradi huo.

  "Kama Watanzania haijatokea vita ya dini, basi ndiyo hii. Ni kubwa kuliko ile ya Wabarbeig," alisema Askofu Kakobe na kuitaka serikali iingilie kati suala hilo ili kuepusha dhahama inayoweza kutokea.

  "Mimi na waumini wangu tumekubaliana tutakesha hapa usiku na mchana. Maana nasikia huwa wanaweza kuja usiku kubomoa mabango haya," alisema Askofu huyo mwenye maelfu ya waumini jijini Dar es Salaam.

  Mwananchi lilipowasili jana eneo hilo ilikuta mamia ya waumini hao pamoja na Askofu Kakobe wakionekana kutokuwa na silaha yoyote lakini wakisisitiza kuwa wako tayari kwa vita dhidi ya mtu yeyote atakayefika eneo hilo kwa lengo la kung'oa mabango yao.

  "Walifikiri kwa kuwa sisi ni walokole tutakaa kimya, lakini sisi tunasema katika hili hakuna cha kusema tutamwachia Mungu. Mungu yuko 'busy' (anakabiliwa na majukumu mengi) ana kazi nyingi, hili ni jukumu letu," alisema Askofu Kakobe.

  Alilalamika kwamba utawala wa Rais Kikwete unalikandamiza kanisa lake huku akidai kuwa kama ingekuwa madhehebu mengine ya dini, kitendo kama hicho kisingetokea.

  "Wanachokifanya hakina adabu! Kwa (askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp) Pengo isingekuwa rahisi. Wanamuonea Kakobe kwa kuwa ni mnyonge," alilalamika Kakobe akisema yuko tayari kufa ili mradi ahakikishe njia hiyo ya umeme haiwekwi karibu na kanisa lake.

  Alibainisha kuwa awali njia hiyo ilikuwa ipite upande wa pili wa barabara mkabala na kanisa hilo, lakini wakazi wengi wa eneo hilo walipinga kitendo hicho hata pale walipoahidiwa kufidiwa.

  "Hawa waliokataa, hata pale walipoahidiwa kufidiwa, wengi ni wasomi wa chuo kikuu. Eneo hilo ndilo lenye nafasi kubwa. Lakini wakaona upande huu hauna wasomi wanaweza kukubali kirahisirahisi tu.

  Mimi katika hili nasema hapana," alisema Kakobe.

  Kakobe alisisitiza kuwa yeye na waumini wake wameamua kuwa watakuwa wakikesha eneo hilo kuhakikisha watapambana na yeyote atakayefika kung'oa mabango yao.

  Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alisema asingeweza kuwasiliana moja kwa moja na mwandishi wa Mwananchi lakini akaahidi kutuma taarifa ambayo hata hivyo haikujibu maswali ya msingi ambayo yanalalamikiwa na Askofu Kakobe.

  Ingawa taarifa hiyo haikugusia sababu za Tanesco kutotumia upande wa barabara ambao una nafasi kubwa na badala yake kubanana na makazi ya watu upande ambao kanisa hilo lipo, alisema Tanesco imefanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kwamba njia hiyo ya umeme haiwezi kumuathiri binadamu wala mazingira yake.

  Alieleza kuwa njia hiyo inapita kwenye eneo la hifadhi ya barabara na tayari wamepata kibali cha Wakala wa Barabara (Tanroads) kujenga njia hiyo ya umeme inayolenga kukidhi mahitaji ya umeme jijini ambayo yameongezeka kutokana na wingi wa shughuli za kibinadamu jijini.

  Alisema mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Japani na unahusisha ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo 132kV kutoka Ubungo mpaka Makumbusho na kituo cha kupozea umeme Makumbusho.

  "Shirika lingependa kuwataarifu wakazi wa maeneo hayo na wananchi kwa ujumla kuelewa kuwa hakuna madhara yoyote watakayopata wananchi wanaoishi na kupita maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme," alisema Badra na kuongeza:

  "
  Shirika la umeme lilifanya utafiti wa kina na wa kitaalamu pamoja na wa kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa mradi huo na Baraza la Taifa za Mazingira (NEMC) lilijiridhisha na kuridhia kuwa ujenzi huo hautakuwa na matatizo au madhara yoyote kwa wakazi au wapita njia wa maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme."

  Katika kufafanua namna njia hiyo itakavyojengwa ili wananchi wasidhurike, alisema nguzo zinazobeba umeme huo zinajengwa kwa urefu unaofuata viwango vya ujenzi wa msongo wa 132kV mijini ambavyo ni mita 23, akisema ndivyo vinavyokubalika kimataifa, na kuhakikisha usalama wa wakazi na wananchi katika maeneo hayo.

  Vile vile alisema mikono inayoshika vikombe vya waya za umeme katika nguzo hizo vitaelekezwa upande wa barabarani kwa umbali wa mita tatu kutoka kwenye nguzo.

  "Shirika lingependa wananchi waelewe kuwa ujenzi wa njia hiyo ya umeme wa namna hiyo katika maeneo ya mijini ni teknolojia inayoendelea kutumika sehemu nyingine duniani mfano, Japani," alisema.

  Source: Mwananchi

  My take:1... Naomba wataalamu wanifafanulie hapo penye maandishi mekundu pls,
  2...Wana JF naomba msaada wenu wa mawazo hapo penye Bluu na Light blue kuhusu huyu bwana mtu wa Mungu kuongelea vita badala ya kuongelea amani.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Persopnally namfahamu Kakobe.
  Ila kwa hili amebadilika sana. Niliamini kwamba angepiga GOTI na kumwomba Mungu (ambaye yupo busy kusikiliza maombi yetu na kuangalia dhambi zetu) ili hawa mabest wa dowans wasiweke nguzo zao hapo yaani wabatilishe njia. Ila hiyo ya kusema kwamba tutapambana na serikali naona amejitwalia mamlaka ya kifikra ya waumini wake kwamba wajae ari na hamasa ya vurugu endapo wazee wa kata umeme wakifika hapo.

  Pia eleweni kwamba Kakobe ana hasira za kubomolewa parking ya magari kupisha ujenzi wa barabara, nakumbuka kabla kanisa halijameguka alikuwa na wataalam wa kila aina ambao ndio waliofanikisha na kusimamia kitaalam kanisa lake kujengwa within 21 days, I mean siku 21 kamili kanisa na upauaji ulifanyika pamoja na ofisi zake zilizopo chini ya kanisa (underground). sasa wataalam hawa (niliongea nao) walishawasiliana na wizara husika na kuwatengenezea plan mbadala kuepuka kumega eneo la maegesho ya magari ya kanisa. Sasa alipowatimua baada ya kujichanganya na siasa (wao walimpinga kwa hilo) akasahau kufuatilia na alikosa watu wenye ushawishi kwani hatua za awali zilishaanza kuchukuliwa kumega eneo la pili (kimchoro) kupisha upanuzi wa sam nujoma road. Sasa baada ya kuliwa eneo lake, jamaa wanakuja wanamwekea Superkilowatts mbele ya uso wake. naamini hasira zake zina msingi ulioanza mbali sana.

  Pili hawa tanesco wapuuzi kweli kweli, huwezi kupitisha msongo mkubwa wa umeme mahala ambapo kuna mkusanyiko na public activities, labda mfikirie kuwahamisha. wanaposema umeme huo hauna madhara mbona wanazuia watu kujenga jirani au chini ya nguzo au lines zenye msongo mkubwa wa umeme??

  Kakobe na Tanesco wooote mnataka kutuvunjia amani.
  Serikali iache ubabe na Kakobe punguza jazba. kuwa kama Daniel ambae alisugua goti mpaka nebukadreza alisema kuwa Mungu wa danieli ndiye Mungu mkuu.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Kakobe na Waumini Wake Wakesha Kulinda Tanesco Wasipitishe Umeme

  [​IMG]

  January 05, 2010


  Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship lililopo Mwenge jijini Dar es salaam na wauminini wake wameweka kambi nje ya kanisa hilo ili kuishinikiza Tanesco wasipitishe umeme mkubwa karibu na kanisa lao.

  Kakobe na waumini wa kanisa lake wameweka kambi kwa muda usiojulikana wakiwa wamevalia sare ya tisheti zenye maneno ya kuibeza Tanesco na Serikali yenye ujumbe unaosomeka kwa mbele "Tanesco mwogopeni Mungu" na nyuma "Baada ya richmond mmegeukia kanisa!!".

  Askofu mkuu wa kanisa hilo Zacharia Kakobe amesema kuwa endapo umeme huo utapitishwa pale jamii itarajie mpambano baina yao na Tanesco.

  Kakobe aliwataka Tanesco kwenda kujifunza kwake masuala ya umeme kwani amesoma kuliko wao na watarajie kupata upinzani mkubwa kutoka kwa waumini hao wenye uelewa mkubwa wa athari ya ememe huo.

  Alisema kinachofanya waumini hao kukesha hapo kwa muda wote ni kutokana na kutojua ni muda gani nyaya hizo zitapitishwa eneo hilo, hivyo wameona bora waendelee kuwepo kwa muda wote ili kuhakikisha hazipitishwi.

  "Huu ni ufisadi unaofanyika hapa,na tutakuwa hapa mpaka kieleweke hata kama ni mwaka mzima kwani huu umeme chuo kikuu waliukataa kutokana na madhara yake hivyo sisi hatuutaki pia na tutapambana" alisema Askofu Kakobe.

  Aidha alisema kuwa ujumbe katika tisheti hizo utakuwa unabadilika kulingana na matukio yatakayokuwepo kwani hawatojali gharama kwani uhuru ni gharama kubwa kuliko fedha zinazotumika kutengeneza tisheti hizo.

  Aidha Askofu Kakobe aliilaumu Serikali kwa kusema kuwa imekuwa na upendeleo kwa misikiti katika operesheni zake tofauti na inavyofanyika katika makanisa ya kiroho.

  "Serikali inapendelea misikiti zaidi kuliko kanisa,mfano Tabata dampo katika uvunjaji wa nyumba msikiti haukuguswa na zinatumika gharama kubwa na ushirikishwaji unakuwepo" alisema Kakobe.

  Pia Kokobe aliendelea kusema kuwa hayo yanayofanyika hapo Serikali haiwezi wala kuthubutu kuyafanya katika makanisa mengine hasa kwa Kardinal Pengo.

  "Huu ni ujinga mtupu,na kama angekuwa Kardinal Pengo asingethubutu kuuruhusu kufanyika kwake kamwe" alisema.

  Alibainisha kuwa ni juzi tu Serikali imemuita yeye kuwa ni kichuguu tu hivyo anataka kuwadhihirishia kuwa hawawezi kumkanyaga vile wapendavyo na wasitarajie hilo kutokea kamwe.

  Baadhi ya waumini waliokuwepo kanisani hapo wamesema kuwa wanaungana na Askofu wao ili kuhakikisha nyaya hizo hazipitishwi eneo hilo na watakuwepo kwa muda wote.

  "Tupo tayari hata kuzolewa na tinga tinga lakini hawapitishi nyaya hizo hapa na tutakuwepo kwa masaa 24 na tutahakikisha hilo linatekelezeka" walisema waumini.

  Muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Mgesa alisema kuwa wapo kambini hapo kwa hali ya tahadhari na kuishinikiza Tanesco kutopitisha nyaya hizo kwani hazihitajiki kupitishwa eneo hilo kama walivyofanya chuo kikuu cha Dar es salaam.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Siitizami hii kama habari ya kidini. Ingependeza kama habari hii ingekaa kwenye jukwaa la 'Habari Mchanganyiko' au kwengineko lakini sio hapa kweye jukwaa la Dini.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,088
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Pale kwenye kanisa la full gospel kuna vijana kama sabini na nne wamevaa ma tshirt yameandikwa tanesco muogopeni mungu kwa mbele na nyuma yameandikwa Richmond imewashinda mnakimbilia makanisa.

  Wamesema watakaa hapo hadi waje kutolewa kwa bunduki.

  Sababu ya kufanya hivyo ni kugomea kung'olewa kwa mabango ya kanisa lao ili kupisha usimikaji wa nguzo za TANESCO zinazotoka Ubungo kwenda sub station ya Makumbusho.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Tafsiri yake ni mbaya sana!

  Maneno hayo kwenye tshirts yanasikitisha, maana yamekaa kiswahili zaidi, hasa kama kweli yanasema "..Richmond imewashinda...!..

  Anyway ni ukweli, lakini hatua ya kuprint tshirts maalum za ishu hiyo ni ya mwelekeo hasi sana.

  SASA hao vijana wana nia gani...wana mpango wowote wa kupingana na dola katika zoezi hilo, au wamejiandaa kwa maombi?
   
 7. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  ningekuwa kamanda Kova,ningemkamata Kakobe kwa uchochezi na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani......
   
 8. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mimi nilitegemea Bwana Askofu Kakobe angekuwa msitari wa mbele kumaliza matatizo kama haya kwa njia za amani zenye kuonyesha UWEPO WA MUNGU badala yake yeye anatumia njia za kibabe, vitisho vya mapambano bila silaha ambayo mwisho wa siku ni uvunjifu wa amani na kumwagika damu isiyo na hatia kwa ajili ya ubinafsi wa kutaka kuzuia swala muhimu lenye maslahi ya taifa. Ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko mwenye dhambi kufika mbinguni.
   
 9. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi nilishasema mtu huwezi kuibuka tu ktk karne hii na kujiita askofu bila kupitia chuo chochote cha kiuchungaji,lazima huyo mtu anamatatizo na hili la kakobe ni mfano halisi tshirts za richmondi wapi na wapi na wanacho kidai huu ni upuuzi na uchochezi,eti kasema ingekuwa ni msikiti usingeguswa au kanisa la pengo hivi kweli huyu jamaa ana akili sawa sawa kweli? na huu si uchochezi? mi ningekuwa kova saa nyingi nilishatuma vijana wa kazi kufanya mambo yao
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mwisho wa utapeli wa Kakobe unakaribia.
  Kama anataka siasa aingie tu mzima mzima kama Mtikila.Hao vijana 70 woote wanaingia selo moja tu!!
  Tanesco ni shirika la serikali na si la mtu na kujidai kupambana na Tanesco ni kuvua shati ili upambane na serikali.
  Kanisa la Kakobe liko barabarani, halina parking wala sidhani kama lina kibali cha kukalisha waumini wengi katika confined space.
  Hili suala la Kakobe Vs Tanesco litamuumbua.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  sad story
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Yaani imani ni kitu kibaya sana hebu fikiria hao wote wameacha kwenda makazini kizitafutia familia zao mlo wanalinda mabango ambayo yangeweza wekwa vizuri upya baada ya nyaya kupita au wanalipwa na Kakobe??

  Hivyo tu ni mabango je angeambiwa abomoe sehemu ya jengo hilo la kanisa si wangelala barabarani! samaki wekundu kabisa!!! Mxsixiis
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Kakobe anastahili kuwekwa kwenye lile kundi la Mapapa la mzee Mengi kwa sababu anafanya watu waache shughuli zao kulinda kanisa kwa ajili ya maslahi yake mwenyewe huku akitumia jina la Mungu.
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  [​IMG]
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Why is Kakobe Protesting? Kabla ya kutoa allegations tungejadili sababu zinazomfanya mtumishi huyu wa Bwana apinge Tanesco kupitisha Power Transmission facility karibu na Kanisa lake
   
 16. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Nafikiri tunahitaji maelezo zaidi kabla ya kumshutumu Kakobe. Je hayo mabongo yapo ndani ya road reserve, or power supply reserve?, Kama hayapo kwenye reserve kuna makubaliano yoyote ya kulipana fidia yaliyofikiwa na maamuzi yake yalikuwaje? Nafikiri tukipata majibu haya tutajua nani mkorofi. Kimsingi hata kama lile ni eneo halali la Kakobe, TANESCO wakilitaka lazima walipate lakini wanastahili kufuata taratibu.
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hivi na hizi Tshirt zimechapishiwa wapi? Aliyefanya kazi hii haweziwekwa matatani? au sheria zinasemaje hapa?
   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kuna habari hii imenukuliwa kutoka Nifahamishe.com inatoa mwanga juu ya malalamiko yake.

   
 19. k

  kisikichampingo Senior Member

  #19
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Printer ni mfanyabiashara. Hata ukimpelekea 'art work' iliyoandikwa 'Yesu si Mungu' ata print. Mbona magazeti yetu, hasa NIPASHE yana print matangazo ya waganga wa jadi wanaodai wanazo dawa za mapenzi, za kurefusha uume, n.k? wala hawashtakiwi?
  Kuhusu Kakobe, nina wasiwasi kwamba anapokwenda sipo!!
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  huyu mzee hiyo pesa ya ku print hizo tshirt c angeenda kusaidia hos/yatima? halafu wanashinda hapo cku nzima? familia zinaishije...bwana weee kazi ipo.
   
Loading...