Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakakuona ameonekana bunju

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, Oct 30, 2012.

  1. t

    thatha JF-Expert Member

    #1
    Oct 30, 2012
    Joined: Apr 29, 2011
    Messages: 15,199
    Likes Received: 123
    Trophy Points: 160
    Jana tarehe 29/10/2012 Mnyama KAKAKUONA ameonekana maeneo BUNJU katika Wilaya ya Kinondoni. Wananchi walimwekea NAFAKA, SILAHA ZA JADI, MAJI na vitu vingine ili aweze kutabiri yapi yatakayo jiri katika nchi yetu katika siku za usoni. Ni bahati mbaya sana na jambo la kusikitisha kuwa mnyama huyo alipita vitu vyote ambavyo kama angevibusu pengine tungechekelea na badala yake alikwenda moja kwa moja na kuegemea silaha ya jadi aina ya PANGA.

    Binafsi sina la kusema, nawaachia wenzangu kwa hekima na busara mlizopewa na Mwenyezi mungu mtoe michango yenu kuhusu hili.

    Nawasilisha.

    Source:Kipindi cha JAHAZI, Redio CLOUDS.
     
  2. Who Cares?

    Who Cares? JF-Expert Member

    #2
    Oct 30, 2012
    Joined: Jul 11, 2008
    Messages: 3,060
    Likes Received: 1,369
    Trophy Points: 280
    hivi kwa akili ndogo tuu ya darasa la nne TUNAHITAJI KAKA KUONA AJE ATUCHAGULIE PANGA BADALA YA AMANI???...MBONA INAJULIKANA TUNAKOE-LEKEA NA SI MUDA MREFU TUNAFIKA HUKO....NA YOTE HAYA NI KWA SABABU ZOOOTE ALIZOTOA MH. JOHN MNYIKA...tumefika hapa kwa sababu ya Udhaifu.........
     
  3. chitambikwa

    chitambikwa JF-Expert Member

    #3
    Oct 30, 2012
    Joined: Nov 8, 2010
    Messages: 3,935
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 135
    Panga la oman au ?
     
  4. s

    sawabho JF-Expert Member

    #4
    Oct 30, 2012
    Joined: Feb 25, 2011
    Messages: 4,125
    Likes Received: 496
    Trophy Points: 180
    Sio kwa bahati mbaya, jiandae kulinda makanisa yenu, hayo majambia hayo.
     
  5. t

    thatha JF-Expert Member

    #5
    Oct 30, 2012
    Joined: Apr 29, 2011
    Messages: 15,199
    Likes Received: 123
    Trophy Points: 160
    Nilianza kwa kuwaomba mtumie busara mlizopewa na Mwenyezi Mungu katika kuchangia, naona wewe hata Mungu wako humuogopi kabisaaa!! Ee Mungu umsamehe kwa vile hajui atendalo.
     
  6. t

    thatha JF-Expert Member

    #6
    Oct 30, 2012
    Joined: Apr 29, 2011
    Messages: 15,199
    Likes Received: 123
    Trophy Points: 160
    Hapa Makanisa yameingiaje mkuu?
     
  7. asigwa

    asigwa JF-Expert Member

    #7
    Oct 30, 2012
    Joined: Sep 21, 2011
    Messages: 11,985
    Likes Received: 7,345
    Trophy Points: 280
    kuna mtu alishawahi kusema humu kuwa mtanzania nayo ni moja ya maajabu ya dunia.. ngoja tusubiri kitakachotokea.....
     
  8. s

    sweke34 JF-Expert Member

    #8
    Oct 30, 2012
    Joined: Sep 28, 2010
    Messages: 2,528
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 135
    Hawakumwekea JAMBIA au MIKANDA YA MABOMU??
     
  9. Baba V

    Baba V JF-Expert Member

    #9
    Oct 30, 2012
    Joined: Dec 29, 2010
    Messages: 19,489
    Likes Received: 119
    Trophy Points: 160
    Litakuwa ndo lile alilokuja nalo mkulu toka oman
     
  10. Baba V

    Baba V JF-Expert Member

    #10
    Oct 30, 2012
    Joined: Dec 29, 2010
    Messages: 19,489
    Likes Received: 119
    Trophy Points: 160
    Unapoweka jambo ili lijadiliwe usitarajie mtazamo wa aina moja tu, tena wa kukupendeza wewe, si ajabu wewe ndo ukawa hujui utendalo!
     
  11. Bujibuji

    Bujibuji JF-Expert Member

    #11
    Oct 30, 2012
    Joined: Feb 4, 2009
    Messages: 27,929
    Likes Received: 6,761
    Trophy Points: 280
    Tatizo la pombe za viroba ndio hili.
    Kakakuona kapigwa viroba ndipo kapewa nafasi ya kutabiri.
    Sijui mlikuwa mnategemea nini
     
  12. Mzee wa Rula

    Mzee wa Rula JF-Expert Member

    #12
    Oct 30, 2012
    Joined: Oct 6, 2010
    Messages: 8,169
    Likes Received: 54
    Trophy Points: 145
    Haya bana lakini huyo mnyama namuona kama mpiga ramri tu.
     
  13. Baba V

    Baba V JF-Expert Member

    #13
    Oct 30, 2012
    Joined: Dec 29, 2010
    Messages: 19,489
    Likes Received: 119
    Trophy Points: 160
    kwa hiyo 'walimtoa lock' kwanza ndo wakamwekea vitu atabiri
     
  14. Swts

    Swts JF-Expert Member

    #14
    Oct 30, 2012
    Joined: Feb 5, 2012
    Messages: 3,071
    Likes Received: 11
    Trophy Points: 135
    Wangemuwekea binti mrembo, Panga angeTUPA KULEE..!
    Sijuw ndo kukata tamaa na mwelekeo wa amani,dah !
     
  15. s

    sawabho JF-Expert Member

    #15
    Oct 30, 2012
    Joined: Feb 25, 2011
    Messages: 4,125
    Likes Received: 496
    Trophy Points: 180
    Panga = Jambia. Jiulize linatumika kwa kazi gani, na siku za hivi karibuni kama sio busara za Serikali na wale wenye makanisa kungetokea nini? Kama wale wenye makanisa wangejitokeza kupinga dhamira ya kuchomwa makanisa yao kungetokea vita .........ukumbuke kuwa majambia katika baadhi ya imani yanatumika kukata..............wakati wa........Sasa. Akili za kuambiwa changanya na zako. Kama unaogopa utabiri wa Kakakuona, linda amani.
     
  16. Watu8

    Watu8 JF-Expert Member

    #16
    Oct 30, 2012
    Joined: Feb 19, 2010
    Messages: 45,903
    Likes Received: 500
    Trophy Points: 180
    huo ni ULOZI...na nchi yetu hatutegemei hatma yake iamuliwe na WALOZI
     
  17. Bujibuji

    Bujibuji JF-Expert Member

    #17
    Oct 30, 2012
    Joined: Feb 4, 2009
    Messages: 27,929
    Likes Received: 6,761
    Trophy Points: 280
    Tena afadhali wangempa kitu cha konyagi, walimpa ile KIROBA ORIGINAL KUTOKA ARUSHA[​IMG]
     
  18. Mwanamayu

    Mwanamayu JF-Expert Member

    #18
    Oct 30, 2012
    Joined: May 7, 2010
    Messages: 6,062
    Likes Received: 716
    Trophy Points: 280
    anawekewa vitu na sio watu!
     
  19. k

    konar JF-Expert Member

    #19
    Oct 30, 2012
    Joined: Jul 20, 2012
    Messages: 238
    Likes Received: 75
    Trophy Points: 45
    Hivi hata wathungu hutegemea kaka muona kutabiri future yao, au ni huku kwetu uswahilini tu? huyu mnyama kama ni kweli basi ana kipaji cha hali ya juu!
     
  20. yatima

    yatima JF-Expert Member

    #20
    Oct 30, 2012
    Joined: Mar 2, 2011
    Messages: 354
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 0
    Watanzania tusiogope - NI KWELI NIA YA SHETANI NI DAMU IMWAGIKE - WATU WACHINJANE NA AMANI ITOWEKE

    LAKINI HUYO NI SHETANI TU .................. WATU WANAFUNGA NA KUOMBA JAMANI ..........MUNGU ANAJIBU MAOMBI ...

    ATATUTETEA NAAMINI - SHETANI AMESHINDWA ....... HAKUTATOKEA VITA ..... MAKANISA HAYATACHOMWA TENA... KWANI TUMEAMUA KUSIMAMA KATIKA ZAMU YETU YA KUOMBA.

    HIVYO WAOMBAJI ...OMBENI ... KAMA ULIKUWA UNAOMBA NUSU SAA - OMBA SAA NZIMA
    KAMA ULIKUWA HUJUI KUFUNGA HUU NDIO WAKATI ...... :drum::drum::drum:
     
Loading...