Kaka zetu, hayo mabegi ni vipi kwani?

Joannah

JF-Expert Member
May 8, 2020
18,453
42,574
Jamani najua mko poa!

Hivi siku hizi kila kaka huku mjini naona kabeba begi mgongoni, hayo mabebi ni makubwaa sana, na yamekaa kishamba shamba hivi. Mengi Yao yameandikwa Biowang mengine Marcello, yaani unakuta mkaka mzuri, msafii kapendeza halafu kabeba li Biowang mgongoni, hivi mnawekaga nini humo jamani?

Itoshe kusema tu hayawapendezi, mnaharibu Sana muonekano wenu na hayo ma Biowang mnakuwa kama mmetoka Mbwinde bwana.

Hata kama ni laptops tafuteni mabegi mazuri, kwanza wengine hamna hata laptops kuna makaratasi tu humo, basi tu Tanzania likizuka Jambo basi ni nongwa kama wadada na vijora.

Acheni kumtajirisha Biowang na Marcello.

Asante kwa kuelewa
 
Tukitembea na bahasha mkononi pia mnatusema kuonekana jobless!

Mtu nna bahasha 10 zenye CV natembeza sehemu tofauti tofauti unataka niweke kwenye sandarusi!?..

Wenye gari hua wanaweka tu pale kiti cha kushoto documents zao au PC nk ila mi nilie apeche alolo wataka niweke wapi!?.

Hebu mtuache kwanza.

Umenikumbusha sijaanua begi, ili j3 kwenye interview niende likiwa safi.
 
Nikiwa nanunua bag

Naangalia Space na arrangement yake ya ndani kama itafaa kwa size ya pc yangu, mifuko mingi ya kuwekea vitu kama vidokyumenti, chenchi chenchi na hata wallet sometimes

Naangalia pia rangi na muonekano wa nje kissi tena kama hizo marcello ndio zipo basic kwa kazi kazi,

So ukiniona nimevaa ujue nina mambo yangu kichwani Ila kama akili ikitulia kiofisho utaniona na laptop bag classic kidogo

Maelezo ni marefu kiasi Ila ni kwa ajili ya kukuonesha Tu kuwa unachokiomba kwa baadhi yetu HAKIWEZEKANI
 
Jamani najua mko poa!

Hivi siku hizi kila Kaka huku mjini naona kabeba begi mgongoni,hayo mabebi Ni makubwaa Sana,na yamekaa kishamba shamba hivi,mengi Yao yameandikwa Biowang mengine Marcello,yaani unakuta mkaka mzuri,msafii kapendeza halafu kabeba li Biowang mgongoni,hivi mnawekaga nini humo jamaniiiiiiii?

Itoshe kusema tu hayawapendezi,mnaharibu Sana muonekano wenu na hayo ma Biowang mnakuwa Kama mmetoka Mbwinde bwana....hata Kama Ni laptops tafuteni mabegi mazuri,kwanza wengine hamna hata laptops Kuna makaratasi tu humo,Basi tu Tanzania likizuka Jambo basi Ni nongwa Kama wadada na vijora....
Acheni kumtajirisha Biowang na Marcello.
Asante kwa kuelewa
Kama nanyi mnavyokuwa na mabegi makuubwa hayana nauri yamejaa tissue tu.
 
Tukitembea na bahasha mkononi pia mnatusema kuonekana jobless!

Mtu nna bahasha 10 zenye CV natembeza sehemu tofauti tofauti unataka niweke kwenye sandarusi!?..

Wenye gari hua wanaweka tu pale kiti cha kushoto documents zao au PC nk ila mi nilie apeche alolo wataka niweke wapi!?.

Hebu mtuache kwanza.

Umenikumbusha sijaanua begi, ili j3 kwenye interview niende likiwa safi.

mkuu punguza hasira

Naona mtoa mada haelewi kadhia za kuwa apeche alolo
 
Tukitembea na bahasha mkononi pia mnatusema kuonekana jobless!

Mtu nna bahasha 10 zenye CV natembeza sehemu tofauti tofauti unataka niweke kwenye sandarusi!?..

Wenye gari hua wanaweka tu pale kiti cha kushoto documents zao au PC nk ila mi nilie apeche alolo wataka niweke wapi!?.

Hebu mtuache kwanza.

Umenikumbusha sijaanua begi, ili j3 kwenye interview niende likiwa safi.
Dah!kwa hiyo zile Ni bahasha?Ok,nunua hata Yale Jansport Basi...Achana na Biowang
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom