Ulweso
JF-Expert Member
- May 24, 2016
- 23,119
- 27,934
Hiyo no.2 Adam na Hawa walimzaa mtoto mwingine aitwae Sethi Mwanzo 4:25, yaani hata mie huwa na maswali lukukiNilishwahi uliza swali hili kwa mchungaji wangu mmoja na alinipa majibu haya.
1. Biblia tunayotumia haina rekodi ya kila kitu kilichotokea mwanzo, yaani siyo vyote viliandikwa na inasemekana kuna biblia ambayo ina record ya yote yaliyotokea mwanzo ( binafsi sijawahi kuiona ).
2. Matukio ya kwenye Bible yalikuwa yanaandikwa baada ya kupita muda fulani, yaani utaratibu wa kukusanya mistari ilikuwa ikifanyika ambapo kuna mistari ilibeba rekodi za miaka kadhaa mpaka mstari mwingine kutokea.
Kwa mfano hilo la Kaini, haijulikani ni baada ya miaka mingapi tukio hilo lilitokea na ndani ya huo muda Je, Adam na Hawa hawakufanikiwa kupata watoto wengine ? Ambao nao walitapakaa maeneo tofautitofauti.
3. Kupitia sababu hiyo ya pili ndipo hapo Kaini alipata mke ambaye inaonekana alikuwa ndugu yake either wa damu au alikuwa ndugu yake na ndugu zake wa damu.
Nilimuuliza mchungaji, kwanini sasa kwasasa mtu kumuoa dada yake au ndugu yake ni dhambi ilihali hapo zamani Kaini aliweza kufanya hivyo??
Alinipa jibu hili:
Kwa kipindi kile Mungu aliruhusu iwe hivyo ili watu waendelee kuzaliana na kuijaza dunia hivyo haikuwa dhambi tofauti na inavyotafsirika leo.
Baada ya kunipa ufafanuzi huo nilikuwa na maswali mengi sana ila nilimuaga mchungaji ili nisijeibua maswali yasiyokuwa na majibu
Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app