Kaini alipata wapi mke wake?

Alimuoa dada yake. Na pia ni mojawapo ya chanzo cha ugomvi na mdogo wake abel. Ilikuwa aolewe na abel lakini kaini akawa anamtaka. Soma apocrypha kitabu cha adam, 1-6
 
... sijui lengo lako ni kupotosha au nini kwa sababu Biblia imeeleza vizuri tu. Soma Mwa 5: 1 - 5;

1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.


... kumbe Adam na mkewe walikuwa na wana (wa kike na kiume) zaidi ya Kaini, Abel, na Sethi! Very clear indeed!
 
Hilo ndilo jibu sahihi.

Biblia inaeleza kuhusu uumbaji wa Adam, mtu wa kwanza, na Hawa mkewe aliyetoka ubavuni mwake. Narejea baadhi ya maandiko matakatifu. Kwamba Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi (Mwanzo 1:1).

Baada ya kukamilisha uumbaji huo Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.(Mwanzo 1:26 - 28).

Kutokana makusudi ya uumbaji huo, imeandikwa Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. ((Mwanzo 4:1,2, 25)

Kimsingi Adam na Hawa walizaa watoto wa kiume na kike japo kwenye Biblia wametajwa hao wanaume tu. Kaini na nduguze walioa dada zao kama ambavyo Hawa alivyotolewa kwenye ubavu wa Adam. Imeandikwa Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. (Mwanzo 2:21 - 23)

Hiyo ndio siri ya wake wa watoto wa Adam na Hawa (Kaini, Habili na Sethi), chimbuko la familia za binadamu wa sasa. Kila mtoto wa Adam na Hawa alikwenda kuanzisha Taifa lake (Soma Kitabu Mwanzo, Sura ya 4 na 5, kujua uzao wa Adam na Hawa ambao ndio kizazi cha binadamu kinaendelea), kama ilivyoandikwa Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. (Mwanzo 6:1, 2)
 
Haiwezekani tu watoto wawili, walikuwa na dada yao, na Mungu alihalalisha kaka kuzaa na dada yake.
 
Unawezaje kusema Mungu alikataza ngono kwa watu wa familia moja na wakati sisi sote asili yetu ni watoto wa baba na mama mmoja? Maana yake kwa namna moja ama nyingine bado tuna oana watu kutoka asili ya baba na mama mmoja ( Adam na Hawa)
 
Mimi naamini kuna kizazi ambacho hakijaandikwa kwenye biblia sababu ukisoma ya kwenye bibilia hata sasa hatutakiwi kuoana maana sisi ni damu moja
Kabisa Mkuu..labda wasema si vizuri kuoana ndugu wa karibu...!
 
Kwahiyo tunakubaliana kimsingi kwamba, Adamu na Hawa walizaa watoto wengine wa kike na hawakua recorded sawa na utamaduni wa watu wa mashariki ya kati? Right!?
 
Ndugu hizi informations umezitoa wapi?
 
Kwahiyo tunakubaliana kimsingi kwamba, Adamu na Hawa walizaa watoto wengine wa kike na hawakua recorded sawa na utamaduni wa watu wa mashariki ya kati? Right!?
Ukisoma vizuri kitabu cha mwanzo kimeeleza kuwa Adamu na Eva walipata watoto wakike na kiume., Japo maelezo zaidi ya hao wa kike hayakutolewa hapo.
 
Ndio kwa sababu mimi ni mtoto wa ADAM.
binadamu ni neno la kiarabu.
BIN-ADAM
YAANI MTOTO WA ADAM.
Kwa hyo kila binadamu ni mtoto wa adam.
Kwa hiyo mpaka sasa bado tunaoana ndugu kwa ndugu?
 
Ndio
Ndio maana hadi leo
Hatuzidishi kuishi zaidi ya miaka 120
Ukivuka hapo huwi Binadamu tena bali Kiumbe tu.
Kutokana na tamko la Mwanzo 6:3
Napata taabu kuamini hili. Maana siku Moja kwa Mungu, ni miaka elfu kwetu huku.
 
Na kuna watu ni watalaam wa kuongea nayo. Si wayaulize, ?
 
Zile ni hadithi tu, usipende kuamini sana vitabu vilivyotungwa na binadamu kusingizia ni vya Mungu, ule ni usanii tu mkuu toka kwa Waroma.
Na kitabu cha Ufunuo ni hadithi tu?
 
Naomba nikanushe swali langu ni kupata jibu na sio kupotosha
 
Alimuoa dada yake. Na pia ni mojawapo ya chanzo cha ugomvi na mdogo wake abel. Ilikuwa aolewe na abel lakini kaini akawa anamtaka. Soma apocrypha kitabu cha adam, 1-6
Sawa ngoja nipitie
 
Dah iyo mambo mim ndio inanifanyaga nione biblia ni kama chapisho la wagiriki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…