Kaini alipata wapi mke wake?

wapi imeandikwa ruksa kumuoa dada yako? na

wapi mungu akazuia?
 
"kuna uwezekano" hizi doubt ndo zinazofanya watu tuconclude ni hadithi tu
 
wapi imeandikwa ruksa kumuoa dada yako? na

wapi mungu akazuia?
Mambo ya Walawi 18:5
Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana.
18:6 Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana.
18:7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.
18:8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.
18:9 Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue.
18:10 Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe.
18:11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake.
18:12 Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu.
18:13 Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu.
18:14 Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako.
18:15 Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo.
18:16 Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.
18:17 Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu.
18:18 Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai.
18:19 Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake.
18:20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.
18:21 Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana.
18:22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
18:23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.
18:24 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote.
 
Sawa mkuu
 
Sawa
 
Adam aliishi miaka 930,sasa ukiangalia hiyo miaka jiulize mtu huyo akiamua kuzaa anaweza zaa watoto wangapi? Na enzi hizo hakukua na hizi mambo za kulea kwa gharama kubwa sana.
Kiasili kabisa mtoto wa kiume alikua anapewa kipaumbele tangu mwanzo na inawezekana adam alikua na watoto wengine wa kike ambao hawajatajwa katika BIBLIA na ndio maana ukifatilia hata katika mila za kiafrika hasa haoa tz kwa makabila mengi wanawake walikuwa hawaruhusiwi kupata urithi wowote ule, so tangu awali wanawke hawakupewa priority sana.
Hata MUNGU mwenyewe sio muumini wa GENDER EQUALITY ingekuwa sivyo asingetangulia kumuumba adamu then hawa baadaye...... Haya mambo ni magumu kuelewa ila yanaeleweka
 
Unamzungumzia adam alaf unaweka ushahidi wa vitabu vya dini vilivyokuja baada ya adam!

Binaadam ni Adam, mwanaume

Lilith, Hawa, huyu kiumbe mwingine kabisa ambaye ame advance! Na ndio maana vitabu vimekuwa vikikimbia kumzungumzia kabisa, kuna utata mkubwa katika kuumbwa ama kutengenezwa kwa Adam na kisha mwanamke, naamini kuna kiumbe jinsia Ke kabla ya Eve, kabla ya Adam pia. Hii siri imebaki kule kwenye maktaba iliyochomwa moto miaka hiyo, dini hizi tunazofuata sasa hivi inawezekana kwa namna moja ama nyingine tunamuabudu Mungu ambaye hatumkusudii kumuabudu (Tunaabudu Miungu ) kama fikra zetu pandikizi zinavyotupelekesha, ukiangalia vizuri hizi imani kuna mambo mengi sana ambayo kwa namna moja ama nyingine zimejitahidi kuficha asili hasa ya mwanaadamu na kulisha matango pori.

Na mwisho zikaweka mwisho wa kuhoji/kufikiri, ukifikia kiwango cha kukaribia kupata majibu, unawehuka, unakufuru, kuna saa huwa naamini hayawani ( wanyama ) wanajua ukweli zaidi yetu.
 
Kitu ninachokisikia kwamba waarabu wanaoana hata ndugu yaweza kua ilianzia huku, mana nasikia hata dini inaruhusu.
 
Simply Kaini alimkula Dada yake
 
Mungu Mwenyewe alipunguza umri wa mwanadamu, Kutoka hiyo miaka hadi Umri wa Mwisho kuwa miaka 120
Mwanzo 5-3.
Bwana akasema ,Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama,
basi siku zitakuwa miaka mia na ishirini.
Ni 6:3
Mwanzo 6:3
Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
 
Hii miaka 900 ya Adam ilikuwa ni hiihii ya mwezi 12, siku 30 kila mwezi au ?
Ndio
Ndio maana hadi leo
Hatuzidishi kuishi zaidi ya miaka 120
Ukivuka hapo huwi Binadamu tena bali Kiumbe tu.
Kutokana na tamko la Mwanzo 6:3
 
Hii miaka 900 ya Adam ilikuwa ni hiihii ya mwezi 12, siku 30 kila mwezi au ?
Mwanzo 5:3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
Mwanzo 5:4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
Mwanzo 5:6 Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.
Mwanzo 5:7 Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:8 Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
Mwanzo 5:9 Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
Mwanzo 5:10 Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:11 Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
Mwanzo 5:12 Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
Mwanzo 5:13 Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:14 Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
Mwanzo 5:15 Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
Mwanzo 5:16 Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:17 Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
Mwanzo 5:18 Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.
Mwanzo 5:19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
Mwanzo 5:21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
Mwanzo 5:22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.
Mwanzo 5:24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
Mwanzo 5:25 Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.
Mwanzo 5:26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:27 Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
Mwanzo 5:28 Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
Mwanzo 5:29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.
Mwanzo 5:30 Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake.
Mwanzo 5:31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
Mwanzo 5:32 Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
 
Ila haya ni mawazo yako si ndio?
 
Ndio.
Ukisoma biblia utanote kitu kimoja, watoto walitajwa wa kiume tu, watoto wa kike hawakutajwa.
Hawa alipata watoto waume kwa wake, lakini watoto wake waliotajwa kwa majina ni watoto wa kiume tu ambao ni WATATU.
Haya mengine umejiongeza mwenyewe maana hujui hata jina mtoto mmoja wa kike wa Hawa
 
Duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…