Kahawa: Tanzania maarufu tena Duniani

Kahawa: Tanzania maarufu tena Duniani

Ngofilo

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Posts
221
Reaction score
66
Habari zenu wakuu, basi leo wakati wa lunch nikasema ngoja leo nikanunue coffee kidogo, kwakweli sipendelei sana kwenda kwenye haya maduka ya rejareja yaliyotapakaa sana hapa Canada na sehemu nyingi duniani. SEVEN ELEVEN ni franchise convenience store zilizotapakaa kila sehemu ya USA na CANADA na kwa Mara ya kwanza wameipitisha kahawa ya Tanzania kama the best coffee in the world na baada ya kuuza sana kahawa ya Indonesia wamegundua kahawa ya Tanzania ni nzuri kuliko hiyo, Kuanzia last month Seven Eleven zote 53,000 ambazo zimetapakaa kote duniani wameanza kuuza kahawa ya Tanzania.

Binafisi naona hiyo ni milango iko wazi kwa mara nyingine tena kwa wakulima wetu wa kahawa, Serikari ingeanzia hapo kuwasaidia wakulima wa kahawa na viwanda vya kahawa kuanza sasa kuchangamkia soko ambalo tayari Seven Eleven wameshalifungua hasa kwa kuanza kuuza kahawa yetu kwenye store kubwa huku North America kama Super store, Walmart, na nyinginezo.

Baada ya kuongea na store manager mmoja wa Seven Eleven hapa jana, ameniambia kwakweli hii kahawa inapendwa sana kwasababu ina kautamu frani tofauti na zingine. Ni kahawa mbili tu zinauzwa Seven Eleve, Tanzanian coffee na Blazilian coffee. Tuchangamkie mapema hili soko kabla watoto wa jirani kwa mama NGINA hawajatuvuruga make hao mshipa wa noma umeshakatika hawachelewi kuuza kahawa yao na kui label made in Tanzania. Source mimi mwenyewe nimenunua Tanzanian coffee hapa CA..
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    91.2 KB · Views: 1,367
  • image.jpg
    image.jpg
    374.7 KB · Views: 1,230
  • image.jpg
    image.jpg
    264.9 KB · Views: 1,162
Mmmmmhhh...... mimi bado sijaona kwenye maduka ya Wal-Mart ila ntacheki wakati mwingine
 
Unajua mkuu hili swala ni kweli kabisa, maana mi mwenyewe huwa siwezi kabisa kunywa kahawa ya nchi nyingine yoyote isipokuwa ya Tanzania. Hivyo huwa naagiza kahawa toka bongo makopo yangu kadhaa, maisha yanaendelea. Niliona kuna mgahawa flani huku, wameandika kabisa Tanzania coffee kwa kweli kikombe kimoja ni bei kubwa kuliko kahawa zote zilizoorodheshwa pale. Yaani nikabaki natumbua macho na kujiuliza "kumbe kahawa yetu inapendwa na bei iko juu namna hii?" Kwa kweli ni muhimu sana kuhakikisha fursa kama hizi zinafanyiwa kazi haraka ili kuongeza soko la bidhaa zetu
 
Mmmmmhhh...... mimi bado sijaona kwenye maduka ya Wal-Mart ila ntacheki wakati mwingine

Mkuu Lamchina, ndiyo maana nimesema sasa ndiyo wakati wakuchangamkia hayo masoko makubwa make huku mtaani watu wanapenda Tanzanian coffee.
 
Huyo wa kuhakikisha fursa zinafanyiwa kazi yuko wapi? Serikali hii iliyooza ya ccm? Labda washinde UKAWA vinginevyo mitoto ya mama ngina kwa jinsi ilivyo mitukutu mtaona imeanza ku label kahawa yao Made in Tanzania,ila kwa jinsi MUNGU alivyo mkubwa atasimama upande wa wakulima wanyonge wa Tanzania,hii mitoto ya mama ngina itashindwa maana kahawa yao haitakuwa tamu kama ya Tanzania,MUNGU ibariki Tanzania,saidia pia ccm iondoke madarakani.
 
angalau WACHAGGA watarudi kwenye CHATI-ya Ulimaji wa Kahawa.....na wakule ROMBO watamudu kuhudumia MAMA yeyoooo
 
Tuwekee hizo picha za packet ya kahawa siyo methermos ya kahawa!
 
Huku Bukoba mibuni ilishatoweka kitambo, tunalima vanilla, wakati huu pia hela ya mboga kutoka kwa ma Tiba inasaidia kidogo, nawaonea wivu watu wa moshi. In fact wahaya nani katuroga?

Ngoja niburudike kidogo na muziki wa jamaa anayejiita "Obugwaizoba"
Bukoba obugwaizoba, kazirooo maweee, Prof. Mukandara, Prof. Rwaitama, .....njoo tujenge Bukoba yetuuuuuu X3....
 
Kahawa ni nzuri sana ila mimi nikinywaga sijui kwanini mapigo ya moyo yanaenda mbio sana na sweat hadi nakosa nguvu.
 
Kahawa yetu ni nzuri sana, na kwa kweli hata ukiwa unatengeneza kikombe chako ile harufu inamvutia alieko karibu, nakumbuka kuna bibi wa kizungu aliniuliza kahawa ya wapi hiyo?
Fursa ni nzuri ingawa jirani wameisha peleka sana ulaya na hawakuanza leo ila na sisi kama serikali itasaidia kwa kuwapa watu export license bila vikwazo vingi nafikiri tungefika huko na bidhaa nyingi tu, pia packaging ndio tatizo kwetu ingawa wapo wafanyabiashara wanaopeleka baadhi ya vitu nje kama Middle East lakini soko la ulaya na America bado sana
 
Wow ni vizuri... Kikombe kimoja bei gani

Tatizo hao wakulima wenyewe basi wanafaidika
HOE, wee wala usisumbuke na wakulima au hata kikombe, wee just kuwa mtu wa kati(midlman) kanunue na kuuza (baada ya kuRepack) !! Ulimwengu wa sasa mambo ni COFFEE-shop...tu !!
Good luck anza mapema !
 
Back
Top Bottom