Kahangwa aachana na NCCR! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kahangwa aachana na NCCR!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, Dec 5, 2008.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Aliyekuwa mkuu wa Idara ya Itikadi na Mafunzo ya chama cha NCCR-Mageuzi, leo amejiuzuru rasmi uongozi na uanachama wa chama hicho.

  Habari hizi kanithibitishia mwenyewe kwa njia ya simu, ingawa hakunieleza sababu hasa ya maamuzi yake hayo.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  kafanya vema
  Nakumbuka tulimwambia hapa wakati tunazungumzia role ya NCCR katika uchaguzi wa Tarime. Na alionekana kukitetea sana chama hicho mfu.

  Leo kama kang'amua ni jambo jema. Atafute chama makini ajenge nchi. Ilimradi kisiwe chama cha SISI M........
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyu mtu ndo nani? please
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Amekimbia njaa huko.Kama vp atafute chama bora na si bora chama.
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo yawezekana kujiuzuru kwake ni sehemu ya long-term impact of 2008 Tarime by-elections?
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Dec 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Dah, wakuu hapa walimvaa kwelikweli.

  Kahangwa, c'om brother. Hebu tuabarishe nini kimekusibu! The last topic nakumbuka ilikuwa challenge kubwa kwako ni ile ya NCCR na Maslahi ya Taifa
   
 7. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kichwangumu,
  rejea utambulisho wake nilioutoa hapo juu. Besides, ni mwenzetu hapa JF
   
 8. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,057
  Likes Received: 15,657
  Trophy Points: 280

  Hongera Bwana Kahangwa kwa kuachana na NCCR ingawa sababu unazijua wewe mwenyewe. Suala la kwamba asiingie chama cha SISI M nahisi unaongea CCM. Huo ni uamuzi wake maana hata alivyokwenda NCCR - Mageuzi hukumpangia wewe. Karibu sana Kahangwa ndani ya chama tawala. chama sio kibaya labda kama kuna watendaji wabaya. CCM HOYEEE
   
 9. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mmm, sidhani kama ni njaa,si mtu wa kutegemea siasa kupata mkate wake
   
 10. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  isije ikawa mmempa ngapingapi, kama kawaida yenu
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mhhh.. toka NCCR kwenda CCM?? mbona anakuwa bado yuko pale pale!
   
 12. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #12
  Dec 5, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Invisible
  Ni kwa hiari yangu nilijiunga na chama cha NCCR-Mageuzi, na ni kwa hiari hiyo hiyo nimejiuzuru uongozi.Ahsante kwa kuuliza.
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Una mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa, utabaki independent au una mpango wa kuanzisha chama chako? just curious.
   
 14. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #14
  Dec 5, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Rwabugiri,
  Sijaenda na sina mpango wa kwenda CCM. Aidha, sidhani kwamba CCM na NCCR ni vyama visivyokuwa na tofauti.
   
 15. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #15
  Dec 5, 2008
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mama,
  Sina mpango wowote wa kuanzisha chama, nadhani inawezekana kabisa kulitumikia taifa, kulinda na kutetea maslahi yake bila kuwa kiongozi wa chama. Hata hivyo kuwa kiongozi ndani ya chama cha siasa nako kwafaa hasa hasa kama ni chama kisafi ndani na nje na wewe mwenyewe hali inaruhusu.
   
 16. M

  Mama JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kama nimekuelewa vizuri, utajiunga na chama ambacho ni kisafi ndani na nje, sio?
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ndiyo nilizungumzia SISI M....... nasikia ni pacha wake na huyo mwingine uliyemtaja. Kwa kweli ni kibaya na ubaya ni watendaji ndio. Na kama ujuavyo chama ni watendaji, kama wao ni ovyo na chama ni ovyo. Na hata usiposema Oyeee bado chama ni ovyoooooooo we nyamaza tu msubiri kipigo 2010 mjue kitumbua si andazi.
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mh Kahangwa, tutakuuliza kauli yako hii, siku tutakapokuona unakabidhiwa kadi na kofia za CCM....
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Sawa mkuu tuko pamoja. Kaa tulia chunguza na uone chama gani kitakufaa hapo baadaye ambacho unadhani ni safi ndani na nje.
  Mimi kwa miaka yote hii sina chama lakini naitumikia katika nyanja zote.
  OMBI langu usije jaribu kujiunga chama hiki kinaitwa .........jina lingine DEEP GREEN
   
 20. M

  Mama JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  CHADEMA, kichwa hicho!
   
Loading...