KAMATI YA SIASA YA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA NJOMBE YA RIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NJOMBE TC
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi mkoa wa njombe waridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya mji wa njombe katika Miradi ya Shule Sekondari Lunyanywi na Mradi wa Maji uliopo Kata ya Lugenge .
Akizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya ukaguzi wa miradi hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Mhe.Deo Sanga amesema ameridhishwa na na jenzi wa miradi hiyo ambayoitaenda kutatua changamoto ambazo wananchi walikua wakikabiliana nazo kutokana na juhudi kubwa za Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani.
''Nipongeze Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa kusimamia vema fedha za serikali na ufanyajaji wenu wa kazi kwa kiwango kubwa hasa katika utekelezajiwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ''
Aidha akiendelea kuzungumza Mhe.Deo Sanga katika ukaguzi wa Shule Sekondari ya Lunyaywi amesema katika miradi ambayo amepita katika mkoa wa Njombe mradi wa Shule hiyo unatia matumaini kwa namna shule ilivo jengwa kwa kiwango kikubwa na usimamizi ulio bora mpaka kukamilika kwa ujenzi huo.
''Hakika Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe na Mkurugenzi Mtendaji wanafanya kazi kubwa ili kuhakikisha maendeleo yana wafikia wananchi kwa serikali yao mbayo inaongwazwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna wanavyo fanya kazi kwa bidi chini ya usimamizi mathubuti wa Mkuu wa Wilya ya Njombe Mhe.Kissa Kasongwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka''