Ninaomba mwenye namba ya Feleshi ya simu anipatie tafadhali, mtu huyu kanitia kichefu chefu kikuu.
Sijui sheria za jinai Tanzania zimebadilika au haziko sawa na za nchi nyingi au ni Feleshi ndie kilaza.
Bank Fraud, kwanza unamkamata anaye chukua fedha bank, yeye ndiye mtuhumiwa, mtu huyu anawajibu wa kumtaja aliyemtuma au yeye anabebeshwa dhambi nzima na kupewa maximum hukumu bila huruma, kwa makosa mengi sana mojawapo kuficha majambazi, kuiba, na kucheza na nyara za serikali.
Sasa kama DPP anajua nani alichukua fedha zetu halafu leo anasema hawezi mshitaki, sioni kwa nini DPP asiachie ngazi.
wakati umefika kumwomba DPP atoke madarakani au nasi tulete kitim tim kama kile cha Kadhi na misamaha ya kodi, tuandamane usiku nchi nzima hii ndio dawa, ukizingatia nchi yenyewe giza sauti zetu zitasikika kwa umbali unaotakiwa na tutafika tunapotaka.
Wanasheria mnisaidie; fedha za EPA kupitia kagoda zimeibiwa Benki Kuu (BOT). Kisai cha Tsh. 40bil zimeibiwa kwa staili ya kuforgi nyaraka. DPP anasema walikuwa wanazichukua hizo fedha wanajulikana ila hawezi kuwashtaki eti walitumwa tu. Sasa anatafuta waliowatuma.
(a) amejuaje kwamba hao jamaa walitumwa?
(b) kama walitumwa si watakuwa wamewataja mabossi wao?
(c) fedha nyingi kiasi hicho si unaweza ku-trace kwa kuangalia bank transactions na kuzifuatilia akaunti husika?
(d) kama aliyewatuma ni Rais, au CCM, DPP atachukua hatua gani? atawaachia hao jamaa anaodai walitumwa?
Well said, Feleshi anatakiwa awe mzalendo kwa nchi yake aseme ukweli hela zililiwa na CCM full stop!!! siyo anajali tumbo lake tu (Kazi yake), lini tutapata jasiri kutoka kwa viongozi (maofisa) wa serikali kuacha kutumikia wanasiasa badala yake watumikie wananchi??? when?Mambo mengine hata hayahitaji kuyajadili.
Hizo fedha ndizo zimetumika ktk kampeni zao na nyingi wamekula hao waliompa huyu jamaa kazi,sasa mnataka ampeleke nani mahakamani?
MKURUGENZI wa Mashtaka (DDP), Eliezer Feleshi amesema ni vigumu kuwaburuza mahakamani watuhumiwa wanaohusika na kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, akisema kufanya hivyo kunaweza kuiweka serikali mahali pagumu kwani serikali inaweza kuwakamata waliotumwa kuchukua fedha, lakini ikashindwa kuwanasa waliowatuma.
Ama kweli matukio mengi nchini huitwa - ONLY in Tanzania.
Hivi kweli umewahi kusikia askari akishindwa kumkamata mwizi kwa sababu mwizi huyo katumwa..
Wezi wengi Ulaya hata ktk Benk hutumwa, master planner hubakia kutazama mchezo unavyokwenda...Wauza unga toka Columbia hutumwa lakini wote hawa hukamatwa na wakafungwa pamoja na kwamba wametumwa. Leo Tanzania mtu alotumwa kuiba sii mwizi..Basi kama kweli ipo sheria hiyo tutaibiwa sana..Na hakika ya maneno haya itafungua ukurasa mpya wa sheria kiasi kwamba kesho mahakamani wezi watashinda kesi zao, kwa sababu WAMETUMWA.