Uchaguzi 2020 Kagera: Yaliyojiri mkutano wa Tundu Lissu kusaka Urais wa Tanzania 2020-2025

JF kuna homa Kali ya mihemko.Inabidi homa hii itibiwe haraka tarehe 28/10.Yaan ,wakiona umati mkubwa wa kumsikiliza Lissu.Wanahamini kuwa wanamsapoti Lissu.Lakini watu hawahawa walikuwepo kwa Magu.Tuwapongeze tu ,wananchi wa Tanzania kuwa wanapenda kusikia Sera. Kupiga kura in kitu kingine ,kuhudhururia mkutano kitu kingine
Usidanganyike!

Wahudhuriaji wengi wa mikutano ya Magu ni watu waliosombwa toka wilaya na vijiji vya jirani. Husombwa kwa mabasi, malori na matrekta.

Ni watu wachache sana wanaohudhuria mikutano ya Magu ambao ni wakazi wa eneo husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa mapokezi makubwa,
Ila ni.kwamba kwa nini online Chanel yenu chadema mnafunga sehemu ya comment mnaogopa nini kuwaachia wachangiaji tuone wamepokeaje maoni yenu?
Pamoja na kujaza kote bado mnaogopa kusoma maoni ya watu? Hamuoni hili Lina nyuma watu uhuru kama mnavyosema watu wawe huru.
2 nimefatilia mikutano yote y lisu pale anapokuta changamoto ya barabara anaanza kuzungumzia uwanja wa Chato, sasa hiyo pesa ya uwanja unaweza kujenga barabara zote tanzania kila anapoenda?
Mimi nadhani hiyo pesa ya uwanja haiwezi kujenga zaidi ya KLM 40 sasa hizo zitatatua ubovu wa barabara nchini, au siasa tu.

Ni smart move
Kuna jeshi la vijana la CCM na "kitengo" wamepewa kazi ya kutukana na kuponda viongozi wa upinzani wenye nondo kali na pia ili kuinfluence public opinion, kuwakatisha tamaa viongozi wa upinzani. Kwa hiyo akili nzuri ni kufunga comment ili umma wenyewe upokee maudhui bila kuwa influenced na jeshi hilo la mtandaoni
 
Katika lile tulilojua toka mwaka 2017, mkoa wa Kagera una lake jambo juu ya CCM na Rais Magufuli.

Ni mkoa ambao ulipata tetemeko, watu wakahitaji faraja kutoka kwa mfariji mkuu wakaishia kuambulia maneno ya kukereketa na kejeli.

Wana Kagera walipoomba Chakula wakaambiwa serikali haina shamba.

Walipoomba msaada wakaambiwa kwani serikali ndiyo iliyoleta tetemeko?

Kisha wakaishiwa kukejeliwa kuwa kwani huo mkoa una nini, Ukimwi kwao, Tena kuna mto ngono na kijiji kinachoitwa Katerero (yote hii kumaanisha kuwa ni watu wapowapo tu wanaopenda chini).

Sasa kaenda kule mtetezi wa Wanyonge Tundu Lissu, mapokezi aliyoyapata katika vitongoji vya huko ni makubwa ajabu.

Lissu alianzia Nyakanazi, akaja Ngara akaenda Kyerwa.

Kwa kweli mapokezi aliyoyapata huko utadhani ni Jenerali wa Kijeshi aliyeongoza mapambano ya kukomboa maeneo hayo.

Hii ni rasharasha tu bado hajaingia Bukoba mjini.

Kiufupi, kwenye mkoa wa Kagera, CCM hawana chao. Wahaya hawapendi dharau!

Hapa chini ni mapokezi ya Lissu huko Kyerwa!

View attachment 1576849
Kagera wameamua kuonyesha kwa vitendo kwamba tetemeko halikuletwa na jiwe
 
K
Usidanganyike!

Wahudhuriaji wengi wa mikutano ya Magu ni watu waliosombwa toka wilaya na vijiji vya jirani. Husombwa kwa mabasi, malori na matrekta.

Ni watu wachache sana wanaohudhuria mikutano ya Magu ambao ni wakazi wa eneo husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni ww unavyoamini.Siwezi kukupinga.Lakini si kila anayehudhuria anapiga kura.Kwa Na pia Magu anawatu wengi kuliko Lissu
 
Hakuna balaa yoyote Magufuli alijaza uwanja wa Gymcana saa 06:45 asubuhu, huyu jamaaa hadi muda huu Gymcana hakuna kinachoendelea .
 
Watanzania ni Wanafiki sana....Sidhani kama kweli alisema vile kama Chuki ila aliexplain kwamba zile ni natural disasters so huwezi ilaumu serikali, baadhi ya watu ambao hawakua wameathirika walibomoa nyumba zao makusudi ili serikal iwalipe fidia ....Tuache Unafiki na Kusambaza Chuki!!!
 
Aiseeeeee!
Ninachokiona hapo ni "mahaba" yaliyopindukia.
Huo umati si mchezo kwa kweli.
Nimeona clip ya JPM akiwa Tabora leo asubuhi hii,amepaniki balaa.
Yule mzee napendekeza kama anapenda kuendelea kuwa hai,ajitoe tuu kwenye kampeni au asifuatilie kabisa kampeni za Mh. Lissu.
Nimemsikia akisema ilani ya CHADEMA imeandikwa kuwa madini na yatawekwa dhamana,maliasili zetu zitawekwa dhamana na mwisho wa siku hata sisi tunaweza kuwekwa dhamana.
Kweli baba wa uongo ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha Uongo!
IMG_20200921_141608_348.jpg
 
Hivi Magufuli ni wapi alipopata watu wengi walioenda wenyewe? Hakuna hata sehemu moja. Mimi nipo Mwanza. Nguvu iliyotumika kuwapata watu wahudhurie mkutano wa Mwanza, usiambiwe.

Zaidi ya 60% walikuwa wanafunzi waliolazimishwa kuhudhuria wakiwa hawana uniform. Zaidi ya 30% walisombwa toka wilaya zote za mkoa wa Mwanza, hasa maeneno ya vijijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww upo mwanza,lakini tuliona kwenye TV .Wote walikuwa wanafunz?Basi Mwanza ina wanafunz wengi sana.Pia tuliona watu mabarabarani wakimusubri.Kwa hiyo nayo ni nguvu kubwa.Tutumie hoja zaidi.Tusitumie mihemko
 
Hivi Magufuli ni wapi alipopata watu wengi walioenda wenyewe? Hakuna hata sehemu moja. Mimi nipo Mwanza. Nguvu iliyotumika kuwapata watu wahudhurie mkutano wa Mwanza, usiambiwe.

Zaidi ya 60% walikuwa wanafunzi waliolazimishwa kuhudhuria wakiwa hawana uniform. Zaidi ya 30% walisombwa toka wilaya zote za mkoa wa Mwanza, hasa maeneno ya vijijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kupotosha umma wewe na wale waliosimamisha msafara wake kuanzia Kisesa, Igoma, Buzuruga hadi mabatini walisombwa na magari.


Yaani safari CDM jiandaeni kisaikolojia mkipata wabunge zaidi ya 5 itakuwa maajabu sana .
 
Back
Top Bottom