Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Basi la abiria linalomilikiwa na Kampuni ya Arusha Express lenye namba za usajili T 222 ABF, aina ya Scania Marcopolo, ambalo linafanya safari zake kati ya Bukoba kuelekea Arusha, limepata ajali ya kuwaka moto na kuteketea kabisa.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya asubuhi eneo la Kibeta maarufu kwa Kagambo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Taarifa zinasema kuwa abiria wote waliokuwemo kwenye basi hilo wamefanikiwa kutoka salama bila madhara, hata hivyo chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika mara moja!