DR Joshua Lawrence
Member
- Jun 21, 2013
- 21
- 7
Bado naamini kuwa waziri aliyejiuzulu, ni mtu muhimu sana ndani ya mapambano dhidi ya ujangili ulioundiwa ngome imara. Yawezekana Tanzania isimpate shujaa kama huyu milele. Ni shujaa aliyeangamizwa na oparesheni yake mwenyewe. Operesheni tokomeza majangili ikamgeuka na kuwa operesheni tokomeza Kagasheki. Nakutia Moyo shujaa uliyeuawa vitani. Wameua mwili wako lakini naamini wameshindwa kuua uzalendo wako mtukuka! Kwa tafakuri pevu, vita yako takatifu imenajisiwa na kuonekana si kitu. Bunge letu tukufu kwa kusukumwa na upofu wa kura za mwaka 2015 limeshughulikia matawi na sio tatizo lenyewe! Wakati kamati ya uchunguzi ilipaswa kuja na majibu ya kwa nini wale waliotumwa na kagasheki kupigana vita takatifu wameigeuza kuwa vita ya kishetani, tume hiyo imekuja na majibu ya matokeo ya uasi wa vita takatifu iliyoasisiwa na mheshimiwa Kagasheki. Wabuge wetu wakatumia bunge kama eneo la kuhakikishia usalama wa kura zao! Vita takatifu imepoteza udhu!