Kagasheki aifumua Maliasili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagasheki aifumua Maliasili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 14, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki

  *Amfukuza kazi Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori
  *Maofisa wawili nao wafungashiwa virago rasmi
  *Wengine wapewa onyo kali, uchunguzi unaendelea
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, amemtimua kazi Mkurugenzi wa Wanyamapori, Obeid Mbangwa, kutokana na tukio la kutoroshwa wanyama hai zaidi ya 100 kwenda nchini Qatar.

  Mbali na Mbangwa, wengine waliotimuliwa kazi kuhusiana na tukio hilo ni Ofisa katika Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii CITES na Utalii wa Picha mkoani Arusha, Simon Gwera pamoja na Frank Mremi, ambaye ni Ofisa katika Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii CITES na Utalii wa Picha mkoani Arusha.

  Wakati hao wakitimuliwa kazi, mfanyakazi mmoja, Bonaventura Midala ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Uendelezaji Wanyamapori, ameshushwa cheo kwa sababu hakuchukua hatua zinazostahili wakati wanyama hao wanatoroshwa.

  Kwa mujibu wa Waziri Kagasheki, wakati wanyama hao wanatoroshwa, Midala alikuwa Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya kudhibiti ujangili.

  Taarifa hiyo, ilitangazwa jana na Waziri Kagasheki, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa na kwamba kabla ya kufikia maamuzi hayo, ziliundwa tume huru mbili ambazo zote zilitoa mapendekezo yanayofanana. Pamoja na uamuzi huo, alisema yeyote ambaye hakuridhika anatakiwa kukata rufaa.

  “Ndugu waandishi wa habari, nimewaita hapa leo ili kuwaeleza juu ya hili suala la utoroshwaji wa wanyama hai kwenda nje ya nchi.

  “Hili ni suala ambalo Bunge lililopita la mwaka jana lililizungumzia na baada ya kulifuatilia kumekuwa na sehemu mbili muhimu.

  “Sehemu ya kwanza, ilikuwa inahusu watumishi wa wizara waliohusika katika utoroshaji wa wanyama, lakini sehemu ya pili ni upande wa nchi ya Qatar, ambako ndiko inasemekana wanyama ndiko walikopelekwa na pia kuna watu wengine walioko nje ya wizara, wakiwamo wafanyabiashara kama Ahmed Kamran.

  “Upande wa wizara, tumefanya kila jitihada kuhakikisha wale wote waliohusika katika kadhia hii tunawachukulia hatua, lakini kwa umakini mkubwa sana, kwani hatutaki kumwonea mtu, tunataka haki itendeke na sheria ichukue mkondo wake.

  “Uamuzi tuliochukua siyo wa kufurahisha kwa sababu hakuna anayependa fulani aachishwe kazi, lakini baada ya kulitizama suala hili kwa muda mrefu, wizara imefikia maamuzi yafuatayo na hii ni kutokana na sheria namba 8 ya utumishi wa umma ya mwaka 2002, kifungu 6 (1) ambacho kinampa mamlaka Katibu Mkuu wa Wizara kutekeleza nidhamu katika wizara.

  “Kutokana na hayo, wafanyakazi wafuatao wamefukuzwa kazi na tayari wameshapewa barua za kufukuzwa kazi.

  “Waliofukuzwa kutokana na ukiukwaji wa sheria ni Obeid F Mbangwa, huyu alikuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, lakini wakati wa kadhia hii, alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Matumizi ya Wanyamapori,” alisema Waziri Kagasheki na kuongeza:

  “Mwingine ni Simon Charles Gwera, huyu alikuwa Ofisa, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha, ambaye naye alihusika kwa mujibu wa ushahidi pamoja na Frank Mremi wa Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii CITES na Utalii wa Picha Arusha,” alisema Waziri Kagasheki.

  Wakati hao wakichukuliwa hatua hiyo, alisema maofisa wawili wa wanyamapori daraja la pili, wamepewa onyo kali la maandishi kwa kuwa walitekeleza maagizo haramu ya wakubwa wao wa kazi.

  Aliwataja maofisa hao kuwa ni Martha Msemo, ambaye ni Ofisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha na Anthonia Anthony, ambaye ni Ofisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha jijini Dar es Salaam.

  Mwingine aliyepewa onyo kali la maandishi ni Silvanus Okudo, ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha. Alisema Okudo amechukuliwa hatua hiyo kwa kuwa alishindwa kufuatilia na kupata maelekezo ya Mkurugenzi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka sheria katika utoaji wa vibali.

  Alisema Okudo, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu, taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za kinidhamu.

  Sambamba na hao, Waziri Kagasheki alisema maofisa wawili ambao ni Mohamed Madehele wa Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na Mariam Nyallu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha, wanaendelea kuchunguzwa.

  Akizungumzia Serikali ya Qatar ambayo ndege yake ilitumika kusafirisha wanyama hao kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, alisema Serikali ya nchi hiyo haitaki kutoa ushirikiano wowote, licha ya kuombwa kufanya hivyo.

  Kutokana na hali hiyo, alisema Serikali ya Tanzania haijakata tamaa na kwamba imeunda timu ya watu mbalimbali, wakiwamo kutoka Idara ya Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu (DPP), Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kushughulikia jambo hilo.

  “Baada ya Serikali ya Qatar kukaa kimya, tulilazimika kuandika barua makao makuu CITES kule Geneva, Uswiss kisha Qatar wakatuandikia barua, kwamba wamepata barua kutoka Geneva.

  “Lakini hatujakata tamaa, tutakwenda Qatar, tutawahoji mapailoti wa hiyo ndege pamoja na kuangalia vibali vya kuwachukua hao wanyama ili kujua vilipatikanaje.

  “Kuhusu huyu mfanyabiashara Ahmed Kamran, ambaye alihusika katika suala hili, yeye ushahidi upo na wakati wowote atafikishwa mahakamani,” alisema.

  Novemba 24 mwaka juzi, wanyama hai 116, wakiwamo twiga wanne na ndege 16, walitoroshwa nchini kwa kupakiwa kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Qatar kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupelekwa nchini Qatar kinyume cha sheria.

  Baada ya tukio hilo, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyamapori, Obeid Mbangwa, ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.

  Wakati Maige anatoa uamuzi huo katika Bunge la Bajeti, Mbangwa alikuwapo bungeni na baada ya kusikia hivyo, alitoroka bungeni akipitia mlango wa nyuma ili kuwakwepa waandishi wa habari pamoja na wapiga picha waliokuwa wakimfuatilia.

  Hata hivyo, wapiga picha ambao walikuwa wamejipanga katika milango yote ya kuingia katika ukumbi wa Bunge, walifanikiwa kumpiga picha, ingawa yeye na wapambe wake hawakutaka apigwe picha.

  Kutokana na uzito wa suala hilo la kusafirisha wanyama hai, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema Serikali imesitisha utoaji wa vibali vya kusafirisha wanyama hai kwenda nje ya nchi, hadi itakapotangazwa tena.
  SAAAFI SAANA KAGASHEKI UMEANZA VIZURI MALIZA VIZUURI KILA LAHERRI TUKO NYUMA YAKO!!
   
 2. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitu ni mfumo mzima wa ajira umeoza na waajiriwa wa kubebana ndio kifo cha Taifa na uzalendo wetu.
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Amng'oe na msekwa bodi ya ngorongoro (NCAA)..HUYU VETERANI ANA DILI ZAKE NA KIBAYA ZAIDI ANASINZIA KTK VIKAO VYA BODI.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Ahmed Kamran, who this chap is?
   
 5. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  sitatoa pongezi kwa hili, maana tumekuwa mabingwa sana wa kushughulikia matatizo yakitokea badala ya kuzuia yasitokee.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  I hear he is a businessman from Pakistani.
   
 7. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h] SERIKALI imemfukuza kazi Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Obeid Mbangwa na watumishi wengine wawili wa baada ya kukiuka sheria katika utekelezaji wa majukumu yao na kuchangia kuibuka kwa sakata la usafirishaji wa wanyama kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alisema watumishi hao wamefukuzwa kazi , yupo aliyeondolewa madaraka na wengine wamepewa onyo kali.
  “Upande wa Wizara tumefanya kila jitihada, lengo likiwa kutomwonea mtu yoyote, lakini pia sheria ichukue mkondo wake. Wizara imefikia uamuzi ufuatao; wafanyakazi watatu wamefukuzwa kazi na tayari wameshapata barua,” alisema Waziri Kagasheki huku akiongeza ushahidi wa suala hilo umekusanywa wa kutosha.
  Aliwataja watumishi hao kuwa ni Mkurugenzi wa Wanyampori, Obeid Mbangwa ambaye wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya Wanayamapori, Simon Gwera na Frank Mremi wote wanatoka Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.
  Waziri Kagasheki alimtaja mtumishi aliyeondolewa madaraka kuwa kutokana na kutochuku hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama kuwa ni Bonaventura Midala, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Uendelezaji Wanyamapori, wakati wa uhalifu huo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Kuzuia Ujangili.

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Safi sana huu ndo uzuri wa kuwa na serikali imara inayoongozwa na chama makini na si majukwaa na kukurupuka
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hana ubavu wa kumg'oa Msekwa uenyekiti wa Ngorongoro kwani Msekwa yupo pale kulinda maslahi ya mkweree!! We ngoja utaona atateuliwa tena kuwa Mwenyekiti na Kagasheki yupo hapo hapo!! Mafisadi lazima walindane; mama anafisadi Korosho na baba anafisadi wanyamapori!!!
   
 10. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa umakini unatoka wapi?mkurugenzi wa wanyama pori na ndege ya jeshi,tena jeshi la nje vinaendana kweli???kwanini na waziri wa ulinzi na waliyoko chini yake nao wasiwajibike?
   
 11. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sisi ni wa kuzama tu, kwanini wengine wafukuzwe wengine waonywe? hakuna kitu hapo zaidi ya siasa pendwa na kutoana kafara.kwangu mimi bado wanatubabaisha tu lakini yana mwisho tu haya kama sio kesho basi keshokutwa na kama sio basi hata mtondogoo.tutaooooooooooooooooona.
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0


  Kumbe serikali yenyewe ndio hutoa vibali vya kusafirisha wanyama hai? Hivi havipaswi sio tu kusimamishwa bali kufutwa kabisa. Wanyama pekee wakuruhusiwa wawe ni mbwa na paka (sio kwa kuwadharau, lakini hawatoki kwenye mbuga zetu).

  Kinachonishangaza ni kuwa "ndege inaingia nchini, inachukua wanyama 116 wakiwemo twiga wanne, serikali ilikuwa wapi - hasa Jeshi la Wananchi la Tanzania na TISS? Baada ya mwaka mmoja ndio tunaambiwa

  Tuacheni tupumue! Tumechoshwa na sakarakasi zenu! Hakyanani, sijawahi kuona serikali ya vichekesho, zembe na dhaifu kama hii!!!
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Chama cha Mabwepande?
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Another silly showoff!!! Huu ni upuuzi tu kama kuna madudu tunataka kuona watu wakila mvua za kutosha Segerea
   
Loading...